Waberoya
Wewe mpe hiyo misifa tu Jiwe ambayo hana.........
Hivi kuwa madarakani na kuvimiliki vyombo vya dola ndiyo huwezi fanwa chochote na wananchi?
Hebu jiulize Al-Bashir hakuwa na vyombo vya dola?
Yuko wapi sasa hivi?
Hebu jiulize tena, hivi Mugabe hakuwa na vyombo vya dola?
Lakini aling'olewa madarakani, huku haamini yanayotokea
Hebu jiulize pia Mobutu hakuwa na vyombo vya dola alivyoona yeye mwenyewe ndiye anayevimiliki?
Naye si aling'olewa madarakani bila kupenda?
Huyu Jiwe kama anataka kudumu madarakani, basi "asijimwambafai" na kuamini kuwa hapa TZ kawaweka wananchi wote mfukoni mwake, Bali ajinyenyekeze na atekeleze majukumu yake kwa mujibu wa Katiba yake ya Chama na Katiba ya nchi, kinyume cha hivyo nakuapia kuwa hatadumu madarakani!