Tetesi: Mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM

Hata wakati wa Lowasa, haya unayoyasema kwa Membe yalisemwa pia
 
Yeye Membe aliguswa hajanuka! Anuke kwanza!
 
Wewe dogo, hapo mpasuko uko wapi? Hujui kuwa ukimya nao ni jibu tosha? Wewe ni chadema kindakindaki, pilipili usokula....
 
Sijui kwa nini hawakusomi wakakuelewa, huku unawaambia ukweli ulio wazi kabisa.

Nadhani kwa mara ya kwanza ninakubaliana nawe katika mabo mengi nisiyokubaliana na wewe juu ya haya unayoandika hapa; isipokuwa hii sehemu ndogo hii..."it is happening in every political parties duniani..." You are trying to justify the unjustifiable.

Jikite tu kushangilia dikteta tuliye naye. Usitafute kuunga mkono kwa mambo ambayo si 'universal' kama unavyotaka kuaminisha watu..

Ndani ya CCM hakuna mtu yeyote anayeweza kumzuia Magufuli asifanye chochote anachotaka kukifanya, for the simple reason kwamba anavyo vyombo vyote vya kumkandamiza yeyote atakayejitokeza mbele, na wanalijua hilo, na wanaogopa sana. Hawana namna bali kuingia mstalini.
 
Membe anakwenda kuichana chana vipande CCM, kama ambavyo Magufuli alivyoichana Katiba vipande vipande.
Membe kesha fukuzwa ataichanachanaje CCM. Sasaivi Membe ni kama Tundu Lissu! Wote siyo wanachama wa CCM, wanajiamini, hawaogopi kitu au mtu, lakini siyo wanachama wa CCM.
Hivyo hawezi kuichana CCM.
 
Mtizamo wako!
 


Sasa kama hawamwogopi kwanini wanasita katika kufuata katiba kukamilisha kumtoa?
 
Vyama vyetu vina shida sana, yaani katiba zinavunjwa sana sio ccm wala upinzanj.Ni aibu Sana chama kama ccm kuvunja katibà yake waziwazi hivi
 
Ya Ccm tuachieni cc wenywe shughulikeni na chama chenu kinachoelekea kufa
 
Ni kwanini swala la Membe halikufika katika kikao cha Halmashauri kuu ya chama?
Umesoma katiba ya chama, au mnafuata tu kile membe anasema.

BTW acha abweke hapo keshafika tamati uchaguzi utafanyika na fomu moja imetoka na inatosha ila kama anajiona anaweza akachukue fomu ACT agombee
 
Membe aliyoyasema kwenye mkutano wake na wanakijiji pamoja na majirani zake, huko kwao - yalikuwa yamelenga kuwafurahisha hao wanakijiji tu.

Na yeye mwenyewe kujisikia bado anapendwa na wanakijiji. Si vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…