Mpe ushauri kijana huyu

Mpe ushauri kijana huyu

lunogelo

Member
Joined
Oct 9, 2011
Posts
46
Reaction score
5
BASE ON TRUE STORY.

Ilikua mida ya saa 10 alasiri baada ya kujikuta amemmiss mpenzi wake ndipo akaamua kumpigia simu ambayo iliita zaidi ya mara 3 bira ya kupokelewa. Alijaribu tena kupiga baada ya lisaa limoja lakini hali ikawa ile ile ingawa sasa iliita kwa mara 2 tu alipojaribu kupiga mara ya 3 akakutana na ujumbe wa sauti kua namba ya simu anayopiga haipatikani. Hakuhisi jambo lolote lile ingawa halikua suala la kawaida hata kidogo..............

Yalipotimia majira ya saa 2 kasoro usiku ndipo alipoamua kumpigia tena mpenzi wake wakati huu haikuchukua mda ikapokelewa kabla ya kuzungumza jambo lolote lile akaambiwa "honey nitakutafuta badae kuna kazi nafanya".........

Baada ya kuona kimya sana na muda kusogea akaamua kumpigia simu tena safari hii ilikua mida ya saa 4 usiku, alipopiga simu akakutana na ujumbe wa sauti kuwa "simu anayopiga inaongea na simu nyingine hivyo asubiri au akate ajaribu tena baadae" akakata na kujaribu tena baada ya dakika 15 ila akakutana na ujumbe ule ule. Alipojaribu kupiga tena simu kwa mara 3 baada ya dakika kama 6 hivi simu iliita na kupokelewa baada ya salamu ambazo zilidumu kwa sekunde zisizozidi 28 ndipo akaamua kumuuliza kulikoni mbona amemtafuta tangia jioni bila mafanikio? Cha kusikitisha baada ya kukumbana na swali la aina hiyo ndipo akalegeza sauti na kumuambia "swty nimechoka kweli please naomba nilale".........

Baada ya kukata simu kwa hasira huku akitafakari mtiririko wa matukio ndipo alipoamua kumpigia simu tena baada ya dakika kama 12 hivi. Jambo ambalo hakuamini baada ya simu kuita hakakutana tena na ujumbe wa sauti wa sauti kuwa simu anayopiga inatumika ndipo akaamua kukata simu ila alojaribu tena baada ya kama 2 hivi akakutana ujumbe "simu unayopiga haipatikani haipatikani hivyo ajaribu tena badae"

Msaada wako tafadhari
 
Aisee hapo huwa inahitaji busara sana, lakini kiujumla hiyo ni picha ya wazi kuwa thamani ya kijana kwa huyo binti imeshuka na hakuna mapenzi tena. Akiweza nadhani wamuzi utakaokuwa mzuri ni kupunguza mapenzi na hatimaye kuachana naye kabisaa. Pole yake na kama ni story pia inafundisha na kujenga uzoefu.
 
asiwe mwepesi sana kuhukumu hebu ajitahidi kupata maelezo kutoka kwa muhusika..najua inauma ila busara inahtajika
 
mkubwa hata kama kusoma hujui basi ona picha... sio swala la busara kaka ila tu ni kuwa huyo msichana wako ana mtu mwingine na inavoonekana mahusiano nae (hayo mapya) hayajaanza muda...maana kipya kinyemi ndo mana siimu masaa, wakishachokana baadae watapunguza...

So mwenzio huyo kifupi ameelekeza macho na masikio yake kule kwingine na inawezekan anakutafutia sababu tu ili muachane...ila uzoefu mwingi inaonyesha tunahangaika badae tunarudi tulipotoka!! huyo mwenzio anahangaika saizi ila atarudi badae akikutana na atakayokutana nayo huko...

Cha kukushauri kama unataka kuhakiki kuwa huna chako lakini kama una moyo pia, pay her a visit, na iwe sudden visit bila kumwambia ikiwezekana usiku na iwe nyumbani kwake...ukifika ongea naye ujue in and out na kama utapata nafasi browse simu yake siku hiyo, nakuambia through the phone utapata majibu unayoyataka!!! wana jf wengi watapinga hili la kubrowse simu maana najua wao pia wanatumia simu zao ndivyo sivyo!!

All in all ukipata ukweli ABSTAIN from her..kama ameanza mapema hivo hafai hata
 
anatumia line gani?itakuwa network mbovu tu
 
duh! ngumu kumesa aisee!! tupa kulee huyooo! wanamchakachua huyoooo....
 
Oya huyo dada asije akawa anatumia mtandao wa tigo ambao network kwao ni issue of contradiction kama serikali ya jk,afu akasingiziwa ana hawara.fanya uchunguz kwanza kabla hujaamua.
 
Yalipotimia majira ya saa 2 kasoro usiku ndipo alipoamua kumpigia tena mpenzi wake wakati huu haikuchukua mda ikapokelewa kabla ya kuzungumza jambo lolote lile akaambiwa "honey nitakutafuta badae kuna kazi nafanya".........

ushauri ni kuwa awe msikivu.................................asubiri atafutwe hapo baadaye asipotafutwa kama alivyoahidiwa ajue..............it is time to pack his bags and move on..........ili ampe mwenzie muda wa kutosha na wa milele wa kumalizia shughuli zake........
 
Hapo panahitajika sana busala na hekima japo inauma ila busala inahitajika sana kuliko nguvu.pole
 
Nilishawahi kukutana na hali hiyo,
Fanya uchunguzi ili uonyeshe busara lakini dalili ya mvua ni mawingu....
 
BASE ON TRUE STORY.

Ilikua mida ya saa 10 alasiri baada ya kujikuta amemmiss mpenzi wake ndipo akaamua kumpigia simu ambayo iliita zaidi ya mara 3 bira ya kupokelewa. Alijaribu tena kupiga baada ya lisaa limoja lakini hali ikawa ile ile ingawa sasa iliita kwa mara 2 tu alipojaribu kupiga mara ya 3 akakutana na ujumbe wa sauti kua namba ya simu anayopiga haipatikani. Hakuhisi jambo lolote lile ingawa halikua suala la kawaida hata kidogo..............

Yalipotimia majira ya saa 2 kasoro usiku ndipo alipoamua kumpigia tena mpenzi wake wakati huu haikuchukua mda ikapokelewa kabla ya kuzungumza jambo lolote lile akaambiwa "honey nitakutafuta badae kuna kazi nafanya".........

Baada ya kuona kimya sana na muda kusogea akaamua kumpigia simu tena safari hii ilikua mida ya saa 4 usiku, alipopiga simu akakutana na ujumbe wa sauti kuwa "simu anayopiga inaongea na simu nyingine hivyo asubiri au akate ajaribu tena baadae" akakata na kujaribu tena baada ya dakika 15 ila akakutana na ujumbe ule ule. Alipojaribu kupiga tena simu kwa mara 3 baada ya dakika kama 6 hivi simu iliita na kupokelewa baada ya salamu ambazo zilidumu kwa sekunde zisizozidi 28 ndipo akaamua kumuuliza kulikoni mbona amemtafuta tangia jioni bila mafanikio? Cha kusikitisha baada ya kukumbana na swali la aina hiyo ndipo akalegeza sauti na kumuambia "swty nimechoka kweli please naomba nilale".........

Baada ya kukata simu kwa hasira huku akitafakari mtiririko wa matukio ndipo alipoamua kumpigia simu tena baada ya dakika kama 12 hivi. Jambo ambalo hakuamini baada ya simu kuita hakakutana tena na ujumbe wa sauti wa sauti kuwa simu anayopiga inatumika ndipo akaamua kukata simu ila alojaribu tena baada ya kama 2 hivi akakutana ujumbe "simu unayopiga haipatikani haipatikani hivyo ajaribu tena badae"

Msaada wako tafadhari

inasikitisha ila imenichekesha sana, mpe pole ila nitarudi tena.
 
Inauma!lakini pia bado ni mapema sana kuanza kufikiria vinginevyo.Hata kama hana mazoea ya kuleta chenga chenga kama hizo lakini hatakiwi kumhukumu mapema,anaweza akafanya yafuatayo:
1.Aandae meza ya mazungumzo ili aweze kumhoji kufahamu nini kilisababisha hali hiyo.
2.Baada ya mazungumzo aingie kwenye zoezi la ujasusi,afanye uchunguzi wa kina atapata ukweli kama ikulu imezingirwa na maharamia ama bado iko salama.
 
Dah kiukweli hizo ni dalili mbaya sana katika mahusiano inabidi jamaa ajiongeze tu,demu ameishaanza kucheza mchezo mchafu
 
Vijana wa hii karne ya technologia ya mawasiliano hatujazoea mafiga matatu. Zamani kabla ya mawasiliano wanawake waliwaburuza sana wazee wetu. Maisha yamebadilika sana. Huyo dada siyo mwaminifu, you are supposed to conduct initial investigation.
 
Piga chini...piga chini hebu niulze tabia hizi wanazo wasichana tu au nawanauume?
 
Back
Top Bottom