Mpenda Haki? Mpenda Amani? Jumapili Tukutane Kwa Gwajima!"

Mpenda Haki? Mpenda Amani? Jumapili Tukutane Kwa Gwajima!"

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
3,499
Reaction score
5,956
Habari ya uzima wana JF,

Sina mengi ya kusema leo, ila niende moja kwa moja kwenye hoja, hakuna neno "amani" bila neno 'haki' nyuma yake.
Kama wewe ni mpenda haki, amani, uhuru na mabadiliko ya kweli katika nchi yetu, basi haya yanayoendelea dhidi ya Kanisa la Ufufuo na Uzima hayapaswi kufumbiwa macho.

Vitendo vinavyofanywa na serikali ni vya hovyo, vya kuvunja katiba, na ni kinyume na misingi ya haki na sheria ya nchi yetu. Naomba viongozi wa dini zote kwanzia Wakristo, Waislamu, Wahindu na Ubudha, kupaza sauti dhidi ya ukandamizaji huu wa uhuru wa mtu kuabudu.

Haijalishi wewe ni Muislamu, Mkristo au mtu asiye na dini iwapo unaamini katika haki, basi sauti yako inahitajika leo. Hakikisha Jumapili hii tarehe 6-7-2025, tunajumuika nao kwa ajili ya kuwatia moyo, kwa maana kanisa si jengo wala eneo, kanisa ni kusanyiko la waumini wanao muabudu Mungu katika roho na kweli.

Tufungue macho na tusimame pamoja, uhuru wa kuabudu ni haki ya msingi kwa kila Raia.
Leo ni wao, kesho inaweza kuwa taasisi yako, dini yako, au hata familia yako.

"May God strengthen you." 🙏📣💪
Gwajima.png
 
1750436197003.jpg
 
FFU. Wanapiga virungu hao, hadi vikojoleo vipate moto
Ndio, wanatumia nguvu sana… lakini nguvu za haki na sauti ya wananchi huwa hazizimwi kwa virungu. Twende tukaabudu kwa pamoja kwa Mungu wa roho na kweli.
 
Sawa mkuu. Mimi kunguru wacha nikawapambanie watoto wangu.
 
Mmeligeuza kanisa la gwajima kuwa eneo la uanaharakati? Mmesahau tena vyama vyenu mmgeukia dhehebu
 
Sawa mkuu. Mimi kunguru wacha nikawapambanie watoto wangu.
Wingi wetu ndio ushindi wetu. Hatuendi kufanya fujo, bali tunaenda kumuabudu Mungu wa kweli na haki na kuwatia moyo ndugu zetu wanaonyimwa haki yao ya kuabudu.
 
Mmeligeuza kanisa la gwajima kuwa eneo la uanaharakati? Mmesahau tena vyama vyenu mmgeukia dhehebu
Kanisa limekuwa sauti ya wasio na sauti tangu enzi za mitume. Kusema ukweli mbele ya dhulma si uanaharakati, ni wito wa kiimani. Tunapopaza sauti kwa haki, hatugeuki kuwa chama wala dhehebu, tunasimamia kweli.
 
Ian Ndlovu alisema Kuna makosa mawili atakayofanya kabla ya uchaguzi mkuu yatakayo mlazimisha kuachia kiti.

Nasubiri kwa hamu nione kabla ya Septemba nini kitatokea.
Hakuna Cha makosa ya Mtu katika hili. Sheria ndio imefungia Kanisa na Sheria hiyo hiyo ndio italifungua Hilo Kanisa. Tusipende madhara ya kujitakia. Tii Sheria bila shuruti.
 
Sawa mkuu. Mimi kunguru wacha nikawapambanie watoto wangu.
Usiangalie leo ya watoto wako, hebu ifikirie kesho yao.....Tulichotofautiana wewe upo kwenye umoja yaani "I" na sisi tupo kwenye wingi yaani "WE". Wewe upo kwenye ngazi ya kifamilia, sisi tupo kwenye ngazi ya Taifa, yaani shina ni moja lakini tumetofautiana mizizi, sisi ni mzizi mkuu na wewe ni sehemu ndogo ya mzizi huo.
 
Kuabudu si kosa, ni haki ya msingi ya kila binadamu. Kutisha watu kwa sababu ya imani yao ni kuvunja utu na sheria. Sauti ya haki huwa haizimwi kwa vitisho.
Kesi ipo
Mahakani subirini uamuzi wa mahaka igeni mazuri mabaya yaacheni
 
Kesi ipo
Mahakani subirini uamuzi wa mahaka igeni mazuri mabaya yaacheni
Mahakama ilishatoa uamuzi kwamba kanisa lilofungiwa sio Kanisa la ufufuo na uzima.

Mahakama imeamuru kanisa kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

Lakini cha ajabu polisi wameendelea kukahidi amri ya mahakama, kwa kuendelea kuzuia shughuli za kanisa na kuabudu kwa raia wema.
 
Back
Top Bottom