Habari ya uzima wana JF,
Sina mengi ya kusema leo, ila niende moja kwa moja kwenye hoja, hakuna neno "amani" bila neno 'haki' nyuma yake.
Kama wewe ni mpenda haki, amani, uhuru na mabadiliko ya kweli katika nchi yetu, basi haya yanayoendelea dhidi ya
Kanisa la Ufufuo na Uzima hayapaswi kufumbiwa macho.
Vitendo vinavyofanywa na serikali ni vya hovyo, vya kuvunja katiba, na ni kinyume na misingi ya haki na sheria ya nchi yetu. Naomba viongozi wa dini zote kwanzia Wakristo, Waislamu, Wahindu na Ubudha, kupaza sauti dhidi ya ukandamizaji huu wa uhuru wa mtu kuabudu.
Haijalishi wewe ni Muislamu, Mkristo au mtu asiye na dini iwapo unaamini katika haki, basi sauti yako inahitajika leo. Hakikisha Jumapili hii tarehe 6-7-2025, tunajumuika nao kwa ajili ya kuwatia moyo, kwa maana kanisa si jengo wala eneo, kanisa ni kusanyiko la waumini wanao muabudu Mungu katika roho na kweli.
Tufungue macho na tusimame pamoja, uhuru wa kuabudu ni haki ya msingi kwa kila Raia
.
Leo ni wao, kesho inaweza kuwa taasisi yako, dini yako, au hata familia yako
.
"May God strengthen you." 🙏📣💪
View attachment 3393700