Hivi unaweza kudate na mpenzi alie bize wiki nzima?
Yani yuko bize kuanzia asubuhi mpaka usiku..hata umtext hajibu,utapiga missed calls hata kumi simu haipokelewi..hata kusema yeye akupe "hi" wala hajisumbui!
Unajiuliza hali?hana mda wa kupumzika? Kwenda chooni?
Hata mda anapanda kitandani aguse simu akutext usiku mwema hana..ni jumatatu mpaka jumapili..asubuhi hadi usiku..usiku hadi asubuhi.
Hata Mungu mwenyewe alivoumba dunia alipumzika siku ya saba jamani...we ni kazi gani za ofisini za kukufanya hivi?
Ukitaka akutext inabidi umsumbue kwa maneno makali ulalamike wee ndo utaona akikujibu.
Basi akikujibu anabembeleza wee na msamaha anaomba..ila akaweka simu pembeni bado Yale Yale yanaendelea.
Unashindwa kuwa na quality time na mpenzi akitekwa na mwingine utasemaje?
Kama mpenzi tu hivi..utaweza kujenga familia?
Hivi mnadili vipi na wapenzi wa aina hii??
Sent using
Jamii Forums mobile app