Mpenzi aliye "busy" siku zote

Mpenzi aliye "busy" siku zote

Ushauri umechukuliwa..
Mara nyingi mtu anajua kuwa hapendwi sema anaukwepa ukweli.
Nadhani aggyjay unaujua ukweli kuwa hakujali/hakupendi na nafikiri baada ya kusoma mawazo ya wengi hapa(na sio yale uliyojiandaa kuyasikia ya kukufariji...) utachukua hatua stahiki.

Anza urafiki kabla ya mapenzi.Wasiliana na mtu vya kutosha kabla ya kuanzisha mahusiano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi unaweza kudate na mpenzi alie bize wiki nzima?
Yani yuko bize kuanzia asubuhi mpaka usiku..hata umtext hajibu,utapiga missed calls hata kumi simu haipokelewi..hata kusema yeye akupe "hi" wala hajisumbui!
Unajiuliza hali?hana mda wa kupumzika? Kwenda chooni?
Hata mda anapanda kitandani aguse simu akutext usiku mwema hana..ni jumatatu mpaka jumapili..asubuhi hadi usiku..usiku hadi asubuhi.
Hata Mungu mwenyewe alivoumba dunia alipumzika siku ya saba jamani...we ni kazi gani za ofisini za kukufanya hivi?
Ukitaka akutext inabidi umsumbue kwa maneno makali ulalamike wee ndo utaona akikujibu.
Basi akikujibu anabembeleza wee na msamaha anaomba..ila akaweka simu pembeni bado Yale Yale yanaendelea.

Unashindwa kuwa na quality time na mpenzi akitekwa na mwingine utasemaje?
Kama mpenzi tu hivi..utaweza kujenga familia?

Hivi mnadili vipi na wapenzi wa aina hii??

Sent using Jamii Forums mobile app
Kakugundua mdangaji kutwa vibomu, mbona mko wengi tuu, simu 50 kwa siku zinafika ukipokea tuu laki imeondoka
 
1:Tambua kwa nini yupo busy/ nini kinachomfanya awe hivyo,.
2:Kuwa mkweli kwake kuwa unateseka kihisia anapokiwa anafanya hivyo ili ajue ni kwa namna gani anatenga mda wakuwasiliana na wewe hata kama yupo busy na kazi.

3:Hakupendi tena ila hajui ni kwa namna gani akuambie,.

4:Wewe ni msumbufu/unapenda kuwa karibu yake san so unamkera ?

5:

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukimwambia ukweli anakasirika anadai wewe ni mlalamishi sana bana kwani muda wote nipo na simu...

Mimi niliachwa kisa ni hicho.
 
Kuna mambo mawili, kwanza, hakupendi kama unavyompenda au ambavyo unatamani akupende. Pili, unamsumbua mara kwa mara. Unajua wakati mwingine wanaume hatupendi usumbufu mwingi hasa tunapokua kwenye mambo mengine yanayohitaji umakini au utulivu, japo haiwi bize kiasi cha hata kutoa salam au kumjulia hali mtu unayempenda.

Nahitimisha jambo moja tu, HAKUPENDI.
Usumbufu kwa mpenzi wako? Wakati wassap unamuona muda wote yuko online! Mpaka unajiuliza hv kumbe mie sina umuhimu wowote kwake eeh
 
Kuna mambo mawili, kwanza, hakupendi kama unavyompenda au ambavyo unatamani akupende. Pili, unamsumbua mara kwa mara. Unajua wakati mwingine wanaume hatupendi usumbufu mwingi hasa tunapokua kwenye mambo mengine yanayohitaji umakini au utulivu, japo haiwi bize kiasi cha hata kutoa salam au kumjulia hali mtu unayempenda.

Nahitimisha jambo moja tu, HAKUPENDI.


sio wanaume tu ....hata wanawake hatupend mausumbufu kwakweli..!
 
Swala sio kuchat mda wote..swala ni kutenga mda kwa ajili yangu.kuwa bize jtatu mpaka ijumaa sawa.basi tenga japo jmos na jpili kwajili yangu..hatabkama wikiendi utakua bize basi huwazi japo niweke SAA moja au mbili kumjulia hali mwenzangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
sawa nimekuelwa aggy nitafanya hivyo na utajisikia malkia
 
Mimi siwezi uvumilivu bizze kwa siku 7
Mimi hata masaa 24 nishakuona ndo wale wale.

Yaan masaa 24 mesej, simu, huzion tu?? Hujashika sim?? Inachukua masaa mangapi kunambia "nipo bize nikiwa free nitakutafuta?"

Eeeeeehhh Mbingu ziendelee kunipa roho hiii hiii

Akikuona wann.. Unamdharau ,unapiga chini. Asepee uko.
 
Back
Top Bottom