Mpenzi uniskize

Mpenzi uniskize

Iwe miaka elfu, kipande cha kusubiri,
Fahamu sinayo hofu, nakuacha ufikiri,
Jibu lako kisharifu, nipa ukiwa tayari.
Maili elfu moja, ni mbali nawe tuyuri,
Nimo njiani nakuja, tena sinaye bairi,
Hata yavimbe mapaja, siachi hii safari.
Wawepo ndege alfu, nakupa moja nambari,
Weye tuyuri furufu, kwako sinayo hiyari,
Utaniingia ufu, jibu likiwa si zuri.
Tamati kikwi si hoja, hili naomba kariri,
Moyo wako naungoja, laili wa n'nahari,
Uje ukae pamoja, na wangu kwenye suduri
 
Back
Top Bottom