Mpenzi wa rafiki yangu kabanwa na pumu akiwa chumbani kwa jamaa

Mpenzi wa rafiki yangu kabanwa na pumu akiwa chumbani kwa jamaa

The Garang

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
2,880
Reaction score
4,830
Habarini za uzima wakuu, rejeaa mada husika hapo juu.

Kumekuwa na misemo mingi inayozungumzia athari za uzinzi ,mmojawapo ni "uzinzi gharama".

Masaa mawili au chini ya hapo Leo tarehe 30 05 2021, roommate wangu kakoswa koswa na balaa la kufiwa na mtoto wa mwenyewe room kwetu.

Ilikuwa majira ya saa 2 na dakika kadhaaa, roomate wangu akanambia , mzee kuna demu anakuja hapa.

Kama unavojua maisha ya chuo kupigana exile ni normal na uzuri room yetu ni watu 4 lakini wawili hawajaripoti , may be wameenda kukaa off campus hadi kipindi cha UE.

Basi muda umewadia jamaaa Kani alert ,oyaaa yuko nje anakuja ,...... kiroho safi nikatoka zangu huyohuyo mdogo mdogo niwaache na privacy yao.

Natoka nje nakutana na wadada wawili wametoka chukua msosi uswazi juu[emoji16][emoji16] (wanaojua wanajuaa namaanisha chuo gani hapa), wakaagana, mmoja wao akakatisha nlikotoka , mie kumbe nampimia tu anavoingia machinjioni ye asijue.

Huyo dada ni mfupi, kavaa mtandio kama sio ushungi na ni almost 22 hivi , certificate au diploma.

Basi wakati huo wote mie nlikuwa naongea na simu, nikisuruhisha kesi nyingine ya jamaa yangu nae , huyu jamaa yangu nae ni mtu wa mademu sana ,kampa mimba binti wa watu ,then baba wa binti kawaka kinoma. Anyway turud kwenye mada.

Nimekaa nje almost saa hivi nikijuaa jamaa anafanya mashambuliz kama Yale ya Man City dhidi ya Mendy, lakini kumbe hali ikawa ndivyo sivyo.

Nimekaa zangu nje pembeni ya room za majiran zetu nakuta jamaa anatoka na dada wawatu akiwa kichwa kainamia chini, LAKINI mdada anakohoaa [emoji38][emoji38] nkasema kashaliwa huyu tayari ,hapo kapulizia pafyumu ya jamaa hajaiozoea ndomana anakohoaaa ,huku akijipepeaa na kimtandio chake.

Wamekaaa basi nje wakipiga stori then jamaa akanipigia simu, ikaita nikajificha asione kuwa nlikuwa nawachora. Ile napokea simu jamaa anaongea sauti ya mtu mwenye hofu sana hadi nkashtuka then akanambia njoo ruum.

Nkabaki nashangaa njoo ruum mara moja wakat namuona pale basi namie nkaenda room, nakuta kitanda chake kimebonyea ,kikionesha kuna watu walikuwa wamekaa palee, nkacheki chini nakuta mate mate kama ya udende mie nikadhani ni ute ute wa genitals zao , siku mind nkaona anakuja room akiwa katokwa na mishipa na mwekundu usoni sabab jamaa ni mweupe haswa, alichonambia ndo hichi sasa

Based on what jamaa kaniambiaa, [emoji28][emoji28]wakat wanaendela na foreplay wapo na nguo za ndani tu ......... Hamadiii!!!! dada wa watu akaanza kupumuaa kwa shida , kadiri muda unavozidi akawa hawez hata kuongea kiurahisi ......... Jamaa kuona vile akapanic , ikabidi amauulize binti nini shidaa.

Binti anafunguka kuwa anapumu inamsumbuaa, jamaa akamuuliza kama anaweza kumpigia roomate wa huyo binti alete dawa, binti akagoma.

Wakati huo jamaa hapo ,mzigo ushanywea na ameshavaa nguo mapema anataka kukimbiaa, Bahati nzuri akili ikamcheza akamvalisha nguo chap mdada, wakatoka nje [emoji28][emoji28][emoji28] eti wapunge upepo wakat baridi na pumu havipatani.

Akaongeza zaidi kuwa kuna siku amelala naee usiku kucha lakini hakusumbuaa kitu.

My take:
Tuache okota okota watu hovyo, mtu hujajuana nae, hujui afya yake then unakuja kumleta gheto unapatwa na maswahibu kama hayo, Jamaa mwenyewe amesema alikuwa anataka amkimbie dada wa watu atoroke kabisa aniachie msala mie[emoji1][emoji1]

Japo nime participate kwenye kuhalalisha hili lakini sikuwa na namna, jamaa amesema anakomaa na Coursework tu saiv[emoji23][emoji23]

Lastly,tujitahidi tuache UZINZI na UASHERATI, Biblia katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana, maandilko yanasema .... Wazinzi, waabudio sanamu, waongo ..... hawata urithi ufalme wa mbinguni.
 
Mkuu hivyo vitu vipo kabisa, tatizo sio kuokota okota kama inavyosema, bali ni kuwekana wazi tu na katika mahusiano.

Kwa ushuhuda nimeshawahi kua na mahusiano na mwanamke mwenye matatizo makubwa ya moyo na nilienjoy maisha mpaka pale aliponiacha.pia hata mwanamke mwenye pumu tena huyu alikua wa moto sana, hadi nikawa tukiwa outings natembea na inhaler.

So kikubwa ni kuwekana wazi mwanzo wa mahusiano itawasaidia sana. Ukisema tuanze kuchunguzana sana itakua ni hatari kwani kuna watu wana changamoto zaidi ya magonjwa, lakini hata wao wanastahili kupendwa na kupenda.
 
Msiwe mnakimbilia kupima ukimwi pekeake anzeni kucheck na magonjwa mengne.
 
Mkuu hivyo vitu vipo kabisa, tatizo sio kuokota okota kama inavyosema, bali ni kuwekana wazi tu na katika mahusiano.

Kwa ushuhuda nimeshawahi kua na mahusiano ma mwanamke mwenye matatizo makubwa ya moyo na nilienjoy maisha mpaka pale aliponiacha.pia hata mwanamke mwenye pumu tena huyu alikua wa moto sana, hadi nikawa tukiwa outings natembea na inhaler.

So kikubwa ni kuwekana wazi mwanzo wa mahusiano itawasaidia sana. Ukisema tuanze kuchunguzana sana itakua ni hatari kwani kuna watu wana changamoto zaidi ya magonjwa, lakini hata wao wanastahili kupendwa na kupenda.
umeongea vyema kaka, lakini pia ni bora wawe wawazi ili kuweza kuepusha athari zitakazoweza tokea
 
Perfume hiyo. Wakati mwingine aache kutumia perfume au mafuta yenye arufu atakuwa anakosa muda wote
ni kweli perfume yake ni Kali sana ,hata mwenyewe nikigongea huwa inakaa muda mrefu hadi itokee ,inaitwa the superman
 
Back
Top Bottom