Mpenzi wa Zamani anaisumbua kichwa yangu!

Mpenzi wa Zamani anaisumbua kichwa yangu!

Jamani wana JF ninaomba msaada wenu,
Kuna binti mmoja nilikuwa namdate tukiwa shule tena O level me nikiwa IV yeye II nilipomaliza tu shule mawasiliano yalikata, imepita miaka 16 toka tulioonana na kuwasiliana mara ya mwisho.
Juzi kwenye sherehe za Mei mosi nilienda morogoro nikakutana naye na tuaongea sana, yeye alizalishwa mtoto miaka nane iliyopita lakini hajaolewa. Mimi nimeona na ninafamilia yangu ila kuna chembe ndogo ambazo bado ninamfeel, anataka tuwe wapenzi, nimeongea nae sana na kuhusu mazingira yanayotuzunguka lakini kang'ang'ania anasema eti mimi ndo wake wa maisha na yuko tayari kuwa back up, Je ndugu zangu mnanishauri vp kuhusu hili suala?
mi nashindwa kuelewa, kwa nini watanzania hatuna akili hata tone! Utakufa we panya na uache mtoto yatima. Unavyosema anakung'ang'ania, nani katengeneza mazingira? Yaani unataka upewe ruhusa ya kufanya uovu, utakapopatwa na madhara nani wakukusaidia? Sisi ndo tutakufunga nepi au? Muonee huruma mtoto wako na mkeo watakapokukosa kwa uppumbavu wako. Ndg yangu badilika, acha tamaa, hazina maana kama unavyofikiri? Mwombe Mungu akusamee na uitendee familia yako haki.
 
Jamani wana JF ninaomba msaada wenu,
Kuna binti mmoja nilikuwa namdate tukiwa shule tena O level me nikiwa IV yeye II nilipomaliza tu shule mawasiliano yalikata, imepita miaka 16 toka tulioonana na kuwasiliana mara ya mwisho.
Juzi kwenye sherehe za Mei mosi nilienda morogoro nikakutana naye na tuaongea sana, yeye alizalishwa mtoto miaka nane iliyopita lakini hajaolewa. Mimi nimeona na ninafamilia yangu ila kuna chembe ndogo ambazo bado ninamfeel, anataka tuwe wapenzi, nimeongea nae sana na kuhusu mazingira yanayotuzunguka lakini kang'ang'ania anasema eti mimi ndo wake wa maisha na yuko tayari kuwa back up, Je ndugu zangu mnanishauri vp kuhusu hili suala?

Unakoelekea sio kuzuri kaka, huyo back up wako ni shetani na pepo mbaya na mwishowe atakuvunjia ndoa. Acha tamaa. Mpende mkeo. Kama kweli alikupenda alikuwa wapi during those 16 years? Ameshapigika huko na wengine, mileage zimekwenda sasa anataka kukufanya emotional punching bag! Man up, brother!
 
Sidhani kama mpenzi wa zamani anakusumbua kichwa.
Mi naona wewe mwenyewe tu unajisumbua kichwa.
Na ukiendelea kuamini kama mpezi wako wa zamani anakusumbua kichwa,
utaendelea kusumbuka daima.
USIJISUMBUWE na achana naye.
 
Huyo mpenzi wako wa zamani kasha fulia kimapenzi ndio maana anataka akuaribie na wewe. Kama wewe ndio wake wa maisha, mbona hakukutafuta, maana sie wanawake tukimpenda mtu, lazma tumtafute na kumfuatilia, miaka 16 imepita nawe unaamini tu asemayo?
 
Huyo mdada ameona maisha yamemgonga anatafuta kivuli apumzike, sasa kama hutafikiria kwa mapana na marefu shauri yako lilikukuta utarudi hapa kuomba ushauri
 
Huyo mdada ameona maisha yamemgonga anatafuta kivuli apumzike, sasa kama hutafikiria kwa mapana na marefu shauri yako lilikukuta utarudi hapa kuomba ushauri

Gaga mwanangu, kama vile signature yako na avatar yako vinaviziana vile
 
Kaka muhurumie mkeo...dont gve a chance to such a harlot vingnevyo kamwe hautakuja kubaki salama,it will be a deadly decision to you and to your entire family.
 
Pole kaka hata kama ni nyumba ndogo wenzio wanachagua. Yaani huyo mdada maisha yamemgonga ndio anajidai kukuganda. Angekuwa wa maana asingejitongozesha. Je unajua ameshawatongoza wangapi au unadhani wewe ni handsome sana? Huyo dada ameshazalishwa si hajabu maisha yanamgonga anakuhitaji wewe kama ATM and watch out you might be one among the list of her financial donors.

hili nalo neno!!!!!

umeonaeee,
lakini kwa kuwa mwili unatamani, atafanyaje?
 
we mpige kisela ila mkeo asijue goma la zaman hilo usiliachie hivhiv ukilemba utapigiwa mkeo
 
Chapa ilale. Kama utamwoa shaurilako na hainihusu ila sipendi sikia unamwacha wife wako original.
 
Chapa ilale. Kama utamwoa shaurilako na hainihusu ila sipendi sikia unamwacha wife wako original.
Simshauri amchape coz hujui miaka yote hiyo alikuwa anafanya nini, mambo ya kujikumbushia haya huwa na madhara makubwa, basi tu huwa hatujifunzi
 
Back
Top Bottom