Mwanamitindo na Muigizaji wa filamu, Kim Porter, ambaye pia alikuwa ni mpenzi wa Mwanamuziki Sean Combs au Puff Daddy (P. Diddy), amefariki dunia nyumbani kwake usiku wa jana (Alhamisi) akiwa na umri wa miaka 47.
Porter na Diddy walifanikiwa kupata watoto watatu katika mahusiano yao yaliyodumu tangu 1994 na kuvunjika 2007. Mtoto wa kwanza akiwa ni Christian mwenye umri wa miaka 20 hivi sasa, na mabinti mapacha wawili wenye miaka 11.
Japo chanzo cha kifo chake hakijaelezwa bado, ila marehemu alikuwa akisumbuliwa na mafua makali yaliyoambanatana na pneumonia.
Mungu ailaze roho ya Kim Porter mahali pema peponi.
Amen!
View attachment 935800View attachment 935801