Mpenzi wako alikwambia au alifanya nini ukasema kimoyomoyo huyu hawezi kuwa mke/mume wangu

Kua na demu Mchafu ni mtihani sana
 
Je tuliotizamwa tukaonekana hatuna vigezo tunacoment wapi😢😢

Anyway... Mimi nilimwambia naacha kazi naenda kusoma madras kidogo, maana bint alionesha dalili za dini sana,,,,, nikasema wacha nichekeche nione yaliyomo. Nikamwambia rizk analeta Mungu tunaweza tusiwe matajiri ila tutakula Kama ndege wa angani bila kupanda🤣🤣... Yani nikampa yale maneno ya kiostadh na mashekh!!

Masaa mawili baadae nikaanza kublue tikiwa, mwisho wakaniblock!!!

Nilidhan kanamaadil ya Mungu kumbe n kajambaz ndani ya ushungi🏃🏃
 
Kuna mwanamke bhana ni mke wa mtu ila waliachana so akawa single maza. Nikaja kutana nae tukaanzq mahusiano nikawa nampa hela ndogo ndogo ef 30,50 zangu kazila nyingi tu. Kuna kipindi hadi nikampa 100k alipo nililia kuhusu shida yake flani. Ajabu ni kwamba nilipo Sogea karibu naye ambapo ndio ilikuwa mda mzuri ata wa kusuuza rungu kwa mara ya kwanza (wkt tunakutana nilikuwa mkoani) matukio yakaanza sasa.

Tukio la kwanza akaniambia J naomba tuachane naona siko sawa kuna mambo yananichanganya. Nikamuuliza mambo gani hayo na mbona gafla hivo majibu yakawa hayaeleweki ila akasimamia msimamo wake tu kuwa nimuache hayuko sawa kwa sasa na kwamba pindi akiwa sawa atanitafuta yeye mwenyewe 😂😂

Baada ya kuchunguza nikagundua kumbe amerudiana na mtu wake bhana dah niliumia sanaa... Sasa ikabidi nimchane ukweli kwa kumwandikia msg maana cm zangu alikuwa hapokei tena. Sasa baada ya kuisoma ile msg ndio akaanza kupokea cm zangu tena na hapo sasa ikabidi anichane live bila chenga kwamba kama niko tayari kushea na mtu wake basi fine ila kama sipo tayari nipite kushoto 😂😂 NB:- kumbuka hapo hata mzigo sijaonja ndugu msomaji na plan ilikuwa kumuweka ndani kabisa la haulaaa....

Itaendelea...
 
Unamkumbusha jinsi alivyongangana kuolewa ili siku nyingine aache kuropoka ujinga
 
Wanawake wanapenda sana mionekano hata sehemu ambazo hazistahili hiyo mionekano
 
dah! Kama haukula mzigo inauma kinoma, Mi siwezi kutoa pesa zote hizo kabla sijila mzigo
 
Wadada wa hivi wananishangazaga kweli, unakuta mdada ameajiriwa, mshahara mnalingana, ila mizinga anayokupiga utafikiri ni jobless, imagine na kwa tabia hizo anategemea kuolewa na wewe wewe anaekupiga mizinga na unakuta kiumri anakaribia 3rd floor au yupo 3rd floor, kimuonekano ni mzuri, shape anayo ila hana mahusiano ya kueleweka.

Sometimes kudate na mdada ambae hana kazi kabisa is cheaper, mwanaume unajua kabisa, my girlfriend hana chanzo cha kipato, umhudumie uwezavyo, kuliko hawa wadada walioajiriwa. kitalembwa binti kiziwi princess ariana happyxxx scolastika
 
Ndio maana we don’t date same age, co-workers na wanaofanana na hao.

Nini kinafanya dada jobless adeserve kupewa hela na dada mwenye kazi asipewe 15k ya kijora????
 
Nini kinafanya dada jobless adeserve kupewa hela na dada mwenye kazi asipewe 15k ya kijora????
Umeuliza swali zuri:

Mimi ninavoona "kuwa supportive" ndo kunafanya mdada jobless a deserve kupewa hela, na mwenye kazi asipewe hela.

Kuna wadada hawana kazi wala tsh 100 mbovu ila wako supportive kwa boyfriends wao kuliko wadada walioajiriwa, bahati mbaya wadada ambao wako supportive mara nyingi wanakutanaga na wanaume wa hovyo, yani mdada hakupi tsh 100 ila kuna vitu anafanya unasema I've someone in my life, anakupa moyo, anakushauri, anakupikia mara moja moja, anakwambia my man let's do this, ukifanya hivi, mimi nitapambana hivi, tununue sofa tuliweke gheto. Unajikuta mwanaume unainuka kiuchumi unanunua na kuwekeza kwenye vitu vya maendeleo ambavyo ungekua single usingevifanya, ungeishia kutapanya hela.

Mdada mwingine una date nae ana mshahara mzuri, ila ndo anazidi kukufanya utapanye hela, mdada atatumia mshahara wake kujenga kwao, atasomesha ndugu zake, atakuacha wewe mwanaume upambane mwenyewe kumhudumia yeye, kujenga, kubuni wazo la biashara etc

Wadada walioajiriwa wa hivyo hata kukununulia na kukupa biskuti ya tsh 500 anaona uchungu rohoni (naongea hivi sio kwamba naongeza chumvi, ila ni uhalisia wa kitu nlichokwishawahi kukiona) ukimuomba kwa kumtega, hata akikupa, unaona kabisa huyu ananipa hiki kitu kwa shingo upande.

Sasa wewe ungekua mwanaume kati ya hao wawili ungempa hela yupi binti kiziwi
 
"Hata ikitokea tumeachana siwez kumwambia mtu kuwa unavuta bangi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…