Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Nilikuwa sijui kuoga wala kuvaa, ila amenipenda hivyo hivyo na sasa najua kuoga na kuvaa.
Nilikuwa na lala njaa, ila akanipenda hivyo hivyo na kunipatia chakula, sasa tunashiba.
Wengine walimuuliza unampendea nini huyu fukara ambaye hawezi hata kuhonga mia mbili? yeye aliwajibu, ni mapenzi tu, huyu ndio chaguo langu.

Baada ya kuanza kung'ara, masista duu wanaanza kunipigia miluzi; Nami ninawajibu, siwataki nyie, nipo na malkia wangu aliyenitoa kwenye shida, na sasa ni wakati wetu kung'ara.
Popoto tuendapo, lazima tuwe wawili wawili.
Hapa sing'atuki ng'ooo.
Nyie mnaotanguliza hela kwenye mahusiano, tengenezeni wa kwenu.