Mpenzi wangu anasita kujenga juu ya kiwanja changu

jannelle

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2020
Posts
824
Reaction score
1,581
Tulianza mahusiano amenikuta na kiwanja kikubwa tu, nikamshauri pesa aingize kwenye ujenzi haina haja ya kununua kiwanja, ila amekuwa mzito kujenga juu ya ardhi ile, anadai siku mambo yakienda ndivyo sivyo atapoteza property. [emoji848]

Sio ubinafsi huo? Na why muwaze kuachana mpaka ugomvi wa mali kuhusishwa? Anyways nimemshauri aangalie namna itakayofaa.
 
Kama kweli wewe una nia nzuri na huyo mwanaume muuzie hicho kiwanja kwa bei nzuri, Alafu ajenge nyumba muishi.... Ukishindwa kufanya hivyo basi yupo sahihi kuwa na wasiwasi
 
Huyo ni mwamba, apewe nyundo yake
 
Bora mwanamke ajenge kwenye kiwanja cha Mwanaume. Ila sio kiwanja cha Mwanamke we mwanaume ukajenge imekula kwako.

Mimi mke wangu ana pesa ila sijawahi mwambia achangie hata ujenzi wala sitaki anichangie hata Ada ya watoto. Hata Chumvi kununua sitaki.

Pesa zake akajenge kiwanja kingine atapangisha apate pesa.

Sitaki dharau mimi😆😆
 
Mpenzi wako yupo njia kuu, nashauri apewe maua yake...🤗
 
Kama una mapenzi hasa na huyo mwanaume badilisha jina la kiwanja lisome lake.

Hapo hata yeye atakuwa na amani kujenga, kinyume na hapo kila mtu abaki na kilicho chake. Yeye abaki na pesa zake na wewe ubaki na kiwanja chako.

Maisha sio rahisi hivyo kama unavyotaka kujiaminisha.

Swali jepesi tu, ingekuwa wewe kakwambia ujenge kwenye kiwanja chake ungekubali?
 
Simple, andikishaneni Prenuptial agreement. Dunia ina mengi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…