Mpenzi wangu anasita kujenga juu ya kiwanja changu

Mpenzi wangu anasita kujenga juu ya kiwanja changu

Tulianza mahusiano amenikuta na kiwanja kikubwa tu, nikamshauri pesa aingize kwenye ujenzi haina haja ya kununua kiwanja, ila amekuwa mzito kujenga juu ya ardhi ile, anadai siku mambo yakienda ndivyo sivyo atapoteza property. [emoji848]

Sio ubinafsi huo? Na why muwaze kuachana mpaka ugomvi wa mali kuhusishwa? Anyways nimemshauri aangalie namna itakayofaa.
Duuh
 
Kama kweli wewe una nia nzuri na huyo mwanaume muuzie hicho kiwanja kwa bei nzuri, Alafu ajenge nyumba muishi.... Ukishindwa kufanya hivyo basi yupo sahihi kuwa na wasiwasi
Naam
 
Kama una mapenzi hasa na huyo mwanaume badilisha jina la kiwanja lisome lake.

Hapo hata yeye atakuwa na amani kujenga, kinyume na hapo kila mtu abaki na kilicho chake. Yeye abaki na pesa zake na wewe ubaki na kiwanja chako.

Maisha sio rahisi hivyo kama unavyotaka kujiaminisha.

Swali jepesi tu, ingekuwa wewe kakwambia ujenge kwenye kiwanja chake ungekubali?
 
Back
Top Bottom