Ila haya mambo yanakatisha sana tamaa.
Hili suala nlihisi kama utani lakini lipo kabisa.
Mosi, miaka kadhaa nikiwa shule kuna jamaa next door ambaye tulikuwa tunaenda kuazima pasi na kuchill huko kama room kwetu kumefungwa. Ilikuwa ijumaa siku ya kwenda kujirusha viwanjani akawa anaongea na simu na mdada, jamaa akamuuliza mmewo atakuwa anakugonga kila, yule binti alimjibu hata hizo nguvu anazo basii, daaah iliniuma kuona mdada uliyeamua kumuoa anakuongelea vibaya kwa watu Baki.
Pili, homeboy wangu aliachana na mpenzi wake sabab ikiwa ni dada kumzingua jamaa, miaka kadhaa dada akaamua kuolewa kwa ndoa ya kanisani na uni graduate mmoja ambae ni braza kwetu, japo dada anamtoto tayari LAKINI Bado anamsumbua kumtaka jamaa kwamba kule hakutak na aliolewa basi tu, jamaa yangu muungwana akaamua kumfungia vioo yule Binti coz mmewe ni jamaa yetu pia na sio uungwana.
Tatu, first love wangu aliolewa, juzi kati kapost status nikacoment japo Sina mawasiliano nae ,inaweza pita miaka 2 tumechat mara 3 haizidi. Nikasema namie nataka unizalie mtoto , [emoji3][emoji3] akasema sio mtoto hata watoto mie nakuzalia.
Nkaogopa Sana haya mambo au namie ntakuwa nafanyiwa hivi hivi.