Mpesa MasterCard Tanzania: Kama unapenda uhakika wa malipo yako mtandaoni USIITUMIE

Pole sana Technology bado haijakaa sawa kwao Mpesa/Vodacom.
 
Mimi nina ishu na Airtel MasterCard tatizo kwa simu 100 lilishindikana so nikaenda shop kwao....Nimeacha maelezo yote now nasubiri muamala uingie..Wasipo tatua suala langu nami naja kuwachafua humu mapovu kama yote 400000+ sio kitu ndogo kuibiwa
 
Pole mleta mada, ila Vodacom acheni dharau,Nyie ndio wakituwekea Tobi kweli,mtu anadai mnamzungusha mwezi mzima? Hivi huko vijijini mnawafikiria kweli?

Hivi kuna sababu ipi hasa ya kumwambia mlalamikaji aandike madai yake kwa kiingereza?Kama mnajua kiingereza si mfunge kampuni Tanzania mpeleke huko wanakozungumza kiingereza Sasa,acheni mambo ya ajabu
 
Inawezekana hata barua uliyoandika ilipelepelekwa ofisi za Master Card Ndo maana wakakwambia uandike kwa kiingereza. Hapo mchawi sio voda, wasiliana na master card wao watakuonyesha kila kitu. Voda anapaswa akuonyeshe Notification ya hela iliyokatwa imeenda kwa nani)Kampuni gani?.. ila info zote watakua nazo MASTERCARD.
 
Haya maswala BOT ipige stop, malipo yanayokwenda nje ya nchi yapitie bank moja kwa moja. Hizi virtual MasterCard zipigwe marufuku.

Japo mimi nililipa karibu 600k bila matatizo, kule nilikokua nalipa waliniambia mfumo ukisema failed nisirudie tena kulipa bali ningojee kama pesa itakatwa kwenye acc yangu. Baada ya muda pesa ikakatwa na wao wakaniambia imefika kwao.
 
Mimi sitazungumzia swala la Mastercard bali Hili swala la Tobi , kwakweli Tobi ni matatizo, Tobi haelewi matatizo ya Tanzania, siku zote huwa namrate worse customer service lakini hakuna hata siku moja voda walirespond kujua tatizo ni nini, wanachojua ni kukata pesa tu, TCRA sijui nao wako wapi, wanatumia hela zetu za payee na VAT kupambana na matatizo yenye mfano wa kina Amber rutty ilihali huku tuna matatizo halisi yanayohitaji intervation kutoka kwenu, nadhani Vodacom wanapunguza gharama za kuwalipa hawa wanigeria wa Ison kwaajili ya watu wa customer services, miezi ya karibuni imekua shida sana kupata solution ya haraka kutoka vodacom. Badilikeni na TCRA amkeni kulishakucha Vodacom Tanzania
 

Nimetumia voda com for the long time now kulipia vitu kibao, no problem and very reliable!

Shida ya Vodacom ni moja, customer care na hawawezi toa jibu la moja kwa moja! Hii ni shida sana
 
Mangula
Pole sana kwa changamoto.Ni software gani ulikuwa unanunua?Mimi nafikir Pesa Imeshakwenda na huko unakotafuta siko ilipo hela yako,System ya Voda inatuma tu Pesa kwenda kwenye ile kadi yako pale inaleta request.Wenye Control ni Master Card ambao sasa sijua mkataba wao na Voda Ukoje

Kwa kiwango hicho cha Pesa nafikiri BOT watakuwa wanaiangalia hio pesa kwa hamu sana.Cha kufanya wewe nenda kwaPayment Process 2 Check out uwape hio risiti ya Vodacom na kuwadai wasolve hio issue.

Ukiweza tuwasiliane PM kwa maongezi zaidi
 
Reactions: Pep
kwanini usitumie paypal... ukilink na card yako ya bank... unairuhusu ifanye malipo direct... pesa ipo kwenye card wewe unajua kulink malipo na paypal... hivi ndivyo nifanyavyo
Ni process moja kote,Paypal wanaongeza tu gharama za kutuma Pesa.Cha Muhimu ni kujua nini unafanya hasa unapolipa zaidi ya Dola 100 ni bora ukatumia kadi ya Benki maana wale wana access ambayo naamini voda hawana na pia utaalamu wa mamabo ya fedha hao wafanyakazi wa Voda hawana watakuhamisha hamisha wee mpaka ususe kama mimi.
 
Mkuu mwenye jukukumu la kuongea na master card ni Vodacom na sio mteja , yeye Kama mteja alitambulishwa bidhaa tu , na sio majukumu makubwa Kama hayo
 
Mbona issue yako ni tofauti? Mdau alihakikishiwa na Vodacom kuwa Ina uwezo wa ku deliver pesa zake kwa merchandise wa huko ulaya , kupitia MasterCard , mdau kakamilisha procedures zote na pesa imetoka kwa akaunti yake Bali haikufika huko ambapo Vodacom walimuahidi wanaweza kuifikisha , kosa ni la Nani hapo? Vodacom wakishatakiwq Kuna makosa ?

Ni Bahati mbaya tu mahakama haziko active kivile , maswala Kama haya ulaya watu wanatajirikia hapo
 
MasterCard hawana mkataba wowote na mteja , wao Wana mkataba na Vodacom, Vodacom ndo wanatakiwa kufanya hustling zote kwa ajilinya mteja wao
It work just like banks cards , mastercard hawanijui Mimi , Ila nikipata tatizo benki yangu ndo inasimama kwa niaba yangu
Matatizo ya ki fail transactions huwa yanatokea sana Ila hakuna siku nmb wameniambia niwasiliane na MasterCard au Visa
 
Duh!! Hivi mtoa mada kaingia makubaliano na mastercard au na voda, anayetakiwa kuwatafuta mastercard ni voda na wala siyo mlaji. Voda ndo wameingia mkataba na mastercard, wameniletea huduma mimi niitumie mimi siwajui mastercard natambua aliyeleta huduma
 
kwanini usitumie paypal... ukilink na card yako ya bank... unairuhusu ifanye malipo direct... pesa ipo kwenye card wewe unajua kulink malipo na paypal... hivi ndivyo nifanyavyo
Hapo unaliwa pesa maradufu, paypal wanakula cha kwao na voda wanakula pesa yao.
Hata hivo tatizo litakuwa bado pale pale, shida ni hizi virtual ndo zinasumbua.
 
Wezi Sana hao.,.juzi voda wamenifungia laini..baada ya kuwaambia hela yangu kwenye master card siioni..
 
Hapo unaliwa pesa maradufu, paypal wanakula cha kwao na voda wanakula pesa yao.
Hata hivo tatizo litakuwa bado pale pale, shida ni hizi virtual ndo zinasumbua.
ni direct from bank account kwa muhusika unayemlipa... malipo yanakuwa linked na paypal... ukiachana na ile ya kujaza pesa kwenye akaunti ya paypal kisha ndio ufanye malipo... ila wanakupa option ya kufanya malipo direct kutoka bank... ni heri hii kuliko vodamastercard
 
Safi sana mkuu. Tunahitaji watu kama wewe, kwanza una data zote. Hakikisha unapata haki yako.
 
Pole sana kwa usumbufu ndugu yangu....kwa kweli hawajakutendea haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…