Mpesa MasterCard Tanzania: Kama unapenda uhakika wa malipo yako mtandaoni USIITUMIE

Sio kweli CVV na password za kujua balance ya master card anazitoa wapi?
Kanusho lako ni TOO GENERAL!!

Chifu, unlike Credit Card, Debit Card isn't that safe!! CVV ataipata wapi?! Kabla hujahoji hilo, ulishawahi kujiuliza wale wanao-hack na ku-take control akaunti ya mtu mwingine ile password wanapata wapi?!

Don't forget, unapofanya online purchase, pamoja na mambo mengine pia una-feed CVV!! Unapofanya hivyo tu tayari unakuwa kwenye risk ya taarifa zako kuwa compromised!!

Ni kutokana na hilo ndio maana kutumia debit card ni risk kwa sababu unline credit card, debit card inakuwa connected na bank account yako! Na kwa kuwa unapojaza taarifa zako online tayari unakuwa kwenye risk ya taarifa hizo kuwa compromised, kwa maana nyingine, hata your bank account inakuwa kwenye risk ya kuwa compromised!
 
Mkuu nadhani tatizo ni kwamba umepigwa na sehemu uliyonunua hio website na pesa imewafikia ila wamekutandika. Sidhani kama vodacom wana tatizo lolote.

Siku nyingine Tumia paypal kulipia vitu online kwa kutumia kadi hii itakuwa ni kama ngao,

Hapo hakuna msaada, Ni vyema tu labda ungeweka wazi ni softwarw gani ulitaka kununua katika website ipi maana kuna wevsites kibao ambazo ni feki.

Binafsi natumia hii huduma kwa muda mrefu tu nmeagiza vitu, Kulipia software, kulipia services kama website na vitu kibao bila tatizo lolote.

Sio kila mtandao wa kulipia kwa kadi bila paypal, Hakikisha unajiunga na paypal kulipia vitu, Ukilipia kwa kadi directly ukipata hasara hio ni juu yako wewe,

Ulinunua softwarw gani kwa hio lako 4 na website ni ipi???
 
Mimi ninaitumia nimenunua sana vitu aliexpress kwa kutumia hii huduma, ila vitu vya dollar ndogo ndogo, nikitaka kununua vitu vikubwa natumiaga paypal au payoneer master card.
Hii huduma yao nadhani iko chini ya BANC ABC
 
Ndiyo maana paypal au skrill ni muhimu katika kufanya malipo maana inasimama katikati haina haja ya kujaza hizo kwenye website usizozijua unless kama haikubari hizo huduma
 
Hapo unaliwa pesa maradufu, paypal wanakula cha kwao na voda wanakula pesa yao.
Hata hivo tatizo litakuwa bado pale pale, shida ni hizi virtual ndo zinasumbua.
kwangu mm it's safe kutumia paypal
 

Kwa case kama ya mshkaji jinsi voda wanavyomzungusha inawezekana akilalamika direct kwa management ya MASTERCARD atapata msaada zaidi / Atasikilizwa. Sababu Voda wameshindwa kumsaidia jamaa ndani ya siku 30.
 
Kiujumla mitandao yote kwenye suala la mastercard wamekurupuka Maana airtel nao ni wezi wanaochipukia tu ni suala la muda nyuzi zitapandishwa humu.
Mfano airtel mda na attach mastercard yao paypal walikula salio la artel money bila taarifa ,Pili mda nafanya malipo kulikua na 12k kwenye account ila kila nlipokua naweka mastercard number ili muamala ufanyike inagoma na inakula 2k ata a time hadi mda wanasema pesa imeisha.
Kuwapigia wakaleta longolongo 😪😪 We have a long way to go by the way
 
Kwa case kama ya mshkaji jinsi voda wanavyomzungusha inawezekana akilalamika direct kwa management ya MASTERCARD atapata msaada zaidi / Atasikilizwa. Sababu Voda wameshindwa kumsaidia jamaa ndani ya siku 30.
Ishu ni kwamba Mastercard wanadili na corporates siyo mtu mmoja mmoja mzee.
Kwanza unaanzaje kuwaandikia Mastercard wakati hela hujawapa wao.
Yeye adili na voda, Mastercard hawamjui wanawaju voda
 
Hii 2k huwa inarudishwa kama refund baada ya 1mn...Hii sihuwa wanakata kujiridhisha kama kadi kweli Ipo hewani hutoa kiasi kidogo 1$ kama temporary na kuirudidha muda huohuo na hii hufanyika pale unapolink kadi mpya hasa unapojaza payment info kwenye account yako kwenye website husika.
 
Tumeini bank kwa shughuli za kifedha. Siku izi mambo rahisi tu. Mfano kufungua akaunti Equity ni kama vile unanunua njungu, kadi yake ya visa unapewa apo apo.
 
We tulia tu hayo maelezo ni bora ungekunywa maji mkuu
 
Asante.....umeshuhudia kwa niaba yangu.......nilidhan ni mm mwenyewe hadi muuzaji mtandaoni kaniblock kwasababu aliona nazingua kuhusu malipo nimeleta hadi uzi humu....ukweli ni kwamba card yao imegoma kulipa mtandaoni!!!!!!wakati hela nimeweka ya kutosha nimepiga simu mpaka nimechokaaa huko watssap nimechat nao lakini hakuna msaada naopewa nimeamua tu nikaifufue kard yangu ya equity!!!!mpesa mastercard ni mavi mavi tu natoa pesa zangu naifutilia mbali wapuuzi kabisa hawa!!!!
 
Mnaotumia Alibaba nisaidieni. Hii mnalipaje? Kwangu inakwama

M-Pesa Mastercard inazingua Alibaba
 
Mimi sina hamu naooooh wameniharibia hadi mahusiano yangu na seller jamaa kaona nazingua na kumpotezea muda tu na akaamua kuniblock!!!Sina hamu na hawa voda kbs!
 
Hawa jamaa sasa ni wakuwapelekea samansi ya mahakama kuwataka kuitikia wito wa kikao cha kesi ya dhuruma kwa mteja.....

Hapo wanakesi ya kujibu na wameshakukosea sana. Ukiwapeleka mahakamani wakakulipa na fidia akili zitawakaa sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…