WanaJf wote wenye Miaka 40+ na walilelewa na Wazee wapenda Soukous lazima wamjue huyu Mzee, aliipa Gittaa mdomo na kuiiimbisha kadri alivyopenda yeye. Apumzike kwa Amani
Dah! Soukouss Stars walitubariki sana vijana wa miaka ya 90! Ile bendi yao, wanamuziki wote walikuwa ni Mastaa kweli! Enzi hizo tunaenda kuangalia video; kabla mkanda wenyewe wa siku hiyo haujaanza, tulikuwa tunaoneshwa kwanza trela!
Hapo ndiyo unakutana na akina Soukouss Stars, Aurlus Maebele na Loketo yake, Pepe Kalle na Empire Bakuba yake, Boziboziana, Wenge BCBG, nk.
Hakika maisha yalikuwa ni matamu sana enzi zile za utawala wa Mzee ruksa.
Hatari sana! Humo ndani unakutana na Yondo Sister, Lokassa ya Mbongo, Balu Canta, Lucien Bokilo, Shimita, Ngouma Lokito, Saladine, na mastaa wengineo!!! Hili kundi lilikuwa ni hatari.
Mara ya mwisho nilikutana nae port matadi akiwa kafika kumuona dada yake mfanyakazi wa bandari miaka ya 90 yule dada aliitwa Danize , nilikua bado yanki kabisa