Mpiga picha wa Diamond atoa machozi baada ya kuzawadiwa gari

Mpiga picha wa Diamond atoa machozi baada ya kuzawadiwa gari

Amini nakwambia mwarabu fighter ña diamond wana historia ndefu hawajajuana juzi hawa nawajua kitambo tu sema nikiongea humu wabongo hawachelewi kusema nataka kiki wakati hata mwarabu mwenyewe anajua kama sinaga tabia ya kujipendekeza nilimthibitishia hilo miaka mitatu iliyopita Arusha..mwenyewe anajua
Ndio unataka kusema nini sasa hapa?
 
Diamond yuko vizuri

Jamaa amefanya vitu vizuri sana Big Up....Ila Akipata Muda Apitie Ujumbe wa Malisa GJ
====================================================================

TUNAJIFUNZA NINI KUPITIA MUZIKI WA DANSI TANZANIA?

By Malisa GJ,

Takwimu za ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zilizotolewa April mwaka jana kwa kushirikiana na UNFPA zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 65% ya watanzania ni vijana wa chini ya umri wa miaka 35. Yani ukikutana na watanzania 10, kati yao 7 watakua chini ya miaka 35 (yani miaka sifuri hadi 34) na watatu tu ndio watakaokua wamezidi umri huo.

Kwahiyo tuna kizazi kikubwa ambacho hakikubahatika kushuhudia mageuzi ya muziki wa dansi nchini. Wengi wamezaliwa enzi za 'Bongofleva' lakini kabla ya Bongofleva kulikuwepo muziki wa dansi.

Muziki huu umepitia vizazi vitatu kabla ya kufubaa. Wapo wazee waliofaidi vizazi vyote vitatu vya dansi, wapo waliofaidi vizazi viwili, na tupo tulioshuhudia kizazi cha tatu kabla dansi haijafubaa rasmi hapa nchini.

#KizaziChaKwanza; ni kuanzia Uhuru hadi mwishoni mwa miaka ya 1970. Huku ndiko unakowapata akina Muhidin Gurumo, Joseph Lusungu, Fredy Ndala Kaseba, Hassan Rehani Bitchuka, Marijani Rajab (jabali la muziki), Mbaraka Mwishehe, Said Abdalah Yazib etc. Pia zilivuma band kama NUTA Jazz kabla haijabadilishwa kuitwa JUWATA Jazz na baadae OTTU Jazz kisha Msondo Ngoma. Ilikuwepo Kilwa Jazz, Cuban Marimba, DDC Mlimani Park kabla haijaitwa Sikinde, Tabora Jazz, Morogoro Jazz etc.

#KizaziChaPili ni kuanzia miaka ya 80 hadi mwanzoni mwa miaka ya 90. Huku unawapata akina TX Moshi Willium, Fresh Jumbe, Hamza Kalala, Nguza Vicking, Tom Malaga, John Ngereza, Remmy Ongala, Selemani Mbwembwe, Shaban Dede, Zahir Ally Zoro, John Kitime, Hemed Maneti etc. Pia zilivuma band kama Ochestra Super Matimila, Les Wanyika, Bantu Group, Vijana Jazz, OTTU Jazz Band, DDC Mlimani Park, Kilimanjaro Band, Inafrica Band etc.

#KizaziChaTatu; ni kuanzia katikati ya miaka ya 90 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000. Hiki ni kizazi ambacho vijana wa rika langu tulikishuhudia na kucheza muziki wake. Pia ndio kipindi ambacho muziki wa dansi ulifika katika viwango vya juu kabisa vya ubora.

Hizi ni enzi za wanamuziki kama Banza Stone, Ally Choki, Muumimi Mwijuma, Saleh Kupaza, Rogert Hegga (Katapila) Mao Santiago, Waziri Sonyo, Badi Bakule, Alan Mulumba Kashama, Ndanda Kossovo, Nyoshi El Sadat, Msafiri Diof, Amina Ngaluma (Mwana mahenge), Luiza Nyoni, Jessica Charless, Abdul Misambano, Kalilo Kitokololo, Greyson Semsekwa etc.

Ni kipindi zilipozaliwa bendi bora za dansi kama African Stars (Twanga Pepeta), TOT Plus (Achimenengule), Beta Musica, FM Academia (Wajelajela Gwa), Stono Musica (Wajelajela Original), African Revolution (wana Tamtam), Mchinga Sound (wana Kipepeo), Diamond Sound (wana Kimalumalu), Akudo Impact etc.

Hakika muziki wa dansi ulikua katika viwango vya 'standard gage' kwa wakati huo. Hapa ulikua unawapata wapiga drums mashuhuri kama Gabi Katanga (Yero Masai), na Abuu Semhando (Baba Diana). Wapiga solo maridadi kama Adolph Mbinga, Ephraim Joshua, Miraji Shakashia, Elly Chinyama na Ally Akida maarufu kama 'Tetenasi ya Jeneva'

Pia unawapata wapiga 'base' hodari kama Joseph Watuguru, Jojo Jumanne na marehemu Msichoke Kombo. Wapo pi wapiga keyboard talented kama Victor Nkambi na Andrew Sekedia. Na wapiga tumba machachari kama Sudi Mohamed maarufu kama 'MCD' na Salum Chakuku.

Muziki wa dansi wa kizazi cha 3 ulinogeshwa zaidi na klabu za watuma salamu mikoani ambao walikua wakizipa klabu zao majina ya bendi wanazozipenda. Kulikua na Tamtam Salam club Arusha, Mchinga Generation salam club, TOT Salam club Tanga etc.

Enzi hizo salamu za kadi zilikua mashuhuri sana. Unanunua kadi (shilingi 300) unajaza majina matatu ya unaotaka salamu ziwafikie, unawapa ujumbe halafu unawachagulia wimbo. Ukimaliza unaweka kwenye bahasha unatuma. Unasubiri kusikilizia radioni siku kadi yako itakaposomwa.

Pia kulikua na salamu kwa njia ya simu. Na walikuwepo manguli wa salamu radioni enzi hizo kama Limonga Justin Limonga (Zanzibar), Kipese Makoye (Tanga), Jumanne Sebarua Tingisha (Mbeya), Chesko Mzee wa matunda (Sinza), McRichard Lyimo (Moshi), Maneno Malisa wa Tamtam Salam club (Arusha), Manka Mushi (Kinondoni), Baba Dulawani (Majani mapana Tanga), Wajadi Fundi (Ikwiriri) etc.

Hawa waliufanya muziki wa dansi kuzidi kuwika, maana akipiga simu Chesko Mzee wa Matunda kama hatachagua 'Kisiki cha mpingo' ya Mchinga Sound basi atachagua 'Kimalumalu' ya Diamond Sound. Na akipiga Kipese Makoye kama hatachagua 'Chozi la Mnyonge' ya FM Academia basi atachagua 'Kisa cha Mpemba' ya Twanga Pepeta. Akipiga Maneno Malisa wa Tamtam salam club obvious atachagua 'Tunda' au 'Maisha Kitendawili' za Tamtam.

Enzi hizo muziki wa dansi ulikua unapigwa redioni, kwenye daladala, night club etc. Usipousikiliza radioni utakutana nao kwenye daladala, ama kwenye kumbi za sherehe. Hakukua na namna ya kuikwepa dansi.

Ukienda Msasani Club utawakuta FM Academia, Mango Garden utawakuta Twanga Pepeta, Meeda Club utawakuta Chuchu Sound, Silent Inn utawakuta Diamond Sound chini ya kiongozi wao Ibonga Katumbi, Elyston Angai na rapa mashuhuri Alan Mulumba Kashama a.k.a 'Mustahiki Meya wa jiji'

Matajiri na 'mapedeshee' wote wali-invest kwenye muziki wa dansi. Kuanzia akina Fikiri Madinda, Juma Banatos (JB), Papaa Musofe, Ndama Mutoto ya ng'ombe, Kajumulo Alex Kajumulo, Fred Rwegasira, Chicago Matelephone, Chief Kiumbe, Mudhamiri Katunzi, Isihaka Kibene, Jack Pemba, Medy Mpakanjia etc.

Walikuwa mashabiki wakubwa wa dansi. Wakienda kwenye show wanafuatana na msururu wa wapambe. Kulipa bill ya vinywani "milioni kadhaa" ilikua kawaida kwao. Kisha wanainuka kuwatunza waimbaji. Vyuma havikuwa vimekaza wala kuhitaji grisi.

Enzi hizo dansi ilikua katika viwango vya juu sana vya ubora. Haikua rahisi kumwambia mwanamuziki mkubwa kama Muumini Mwijuma kwamba zitafika enzi watu hawatakua na muda wa kusikiliza nyimbo zake akuelewe. Enzi hizo dansi ilikua kwenye kilele cha mafanikio.

Nakumbuka mwaka 1999 Twanga Pepeta walikuja Moshi kufanya onyesho wakasindikizwa na escort ya polisi ukumbini. Ulinzi uliimarishwa kama vile Rais Trump ametua Tandahimba ndanindani huko. Ilikua rahisi kumpa mkono RPC Chiko kuliko kumsogelea legend Banza Stone au Ally Choki.

Lakini wengi leo wanaishi maisha ya kawaida sana. Nilikutana na Muumini miaka kadhaa iliyopita anaimba kwenye bar moja pale Morogoro, hakuwa yule muumini wa enzi za Tamtam au Mchinga Sound. Alikua amechoka na haikuhitaji 'degree' kujua maisha hayakua tena kama zamani.

Hii inatufundisha kuwa ni muhimu tuzitumie vizuri fursa zinazokuja mbele yetu. Dont let an opportunity go without left a mark into your life. Fursa uliyonayo leo kuna wakati hutakua nayo, je unaitumiaje ili ikuachie alama?

Una followers laki mbili, laki tatu au milioni je unawatumiaje kwa maslahi ya taifa lako na kizazi chako? Una sauti nzuri ya kuimba nyimbo tamu je unaitumiaje kubadili maisha yako? Una kipaji cha kucheza mpira je unakitumiaje kukutoa ulipo? Una urafiki na viongozi wakubwa je unawatumiaje kubadili maisha ya jamii yako?

Kumbuka hicho ulichonacho leo hakitadumu milele. Ipo siku kitaondoka. Je kitakuacha katika hali gani? Ya majuto au ya furaha? Wazungu husema "every oppirtunity comes with an expiry date" yani kila fursa huja na tarehe yake ya kufubaa.

Ipo siku sauti yako ya mvuto itafubaa na haitamvutia yeyote, hata wewe mwenyewe. Ipo siku uwezo wako mzuri wa kujenga hoja utapotea na hata kuzungumza itakua tabu. Ipo siku kipaji cha uongozi kitatwaliwa na hutaweza kujiongoza hata wewe mwenyewe. Utahitaji kuongozwa kwa kila kitu kuanzia kula, kunywa, hata kuogeshwa. Kama unabisha kamuulize mzee Mandela siku za mwisho za uhai wake zilikuaje. Utapangiwa kila kitu hata muda wa kulala.

Ipo siku kipaji chako cha kucheza mpira hakitakuwepo tena na hata kutembea tu itakuwia vigumu. Ipo siku nguvu ulizonazo leo za kukuwezesha kukimbia hapa na pale kutafuta fursa za maisha kwa ajili ya familia yako hazitakuwepo tena. Kila ulichonacho leo ipo siku kitafubaa. Je kabla ya kufubaa kitakuacha katika hali gani? Tumia vizuri kila fursa inayokuja mbele yako kabla nyakati hizo hazijafika.

Malisa GJ.
 
Mbali hata na Mziki Diamond anamzidi mbali sana yule mshindani wake wa kubebwa na mbaleko.

Yule mshindani wake yeye akishaenda Mombasa kamaliza, Diamond anajua sana kujichanganya na watu wote.

Mzee baba yeye na kitimu chake hata kwenye Mazoezi haonekani sijui alitaka kucheza au!
 
hii imekaa powa... lakini mbona mwarabu kmya sana??
Mwarabu kadondoka na bajaj wakamzira, sa hii kwenye media stunt wanamsimamisha lukamba hata yule kifesi hajaambulia hata baskeli.
Huyu dogo awekeze saana kivyake akae sawa, hawa wapambe wanaompa akili za kilofa hizi hawa kina babutale na huyu bwege sallam sijui nani yule TMK asome vizuri sana.
Wako pale wanapiga chao kesho hao washatoka baru wanatafuta mwingine wampune.
 
Mwarabu kadondoka na bajaj wakamzira, sa hii kwenye media stunt wanamsimamisha lukamba hata yule kifesi hajaambulia hata baskeli.
Huyu dogo awekeze saana kivyake akae sawa, hawa wapambe wanaompa akili za kilofa hizi hawa kina babutale na huyu bwege sallam sijui nani yule TMK asome vizuri sana.
Wako pale wanapiga chao kesho hao washatoka baru wanatafuta mwingine wampune.
mkubwa fella ndo kuu la majambazi..
 
1.Diamond platnumz
2. Lionel Messi
Katika maisha ya hawa jamaa kuna vitu vingi sana vya kujifunza...forever ever these two creatures will remain to be my Icons
 
Mwarabu kadondoka na bajaj wakamzira, sa hii kwenye media stunt wanamsimamisha lukamba hata yule kifesi hajaambulia hata baskeli.
Huyu dogo awekeze saana kivyake akae sawa, hawa wapambe wanaompa akili za kilofa hizi hawa kina babutale na huyu bwege sallam sijui nani yule TMK asome vizuri sana.
Wako pale wanapiga chao kesho hao washatoka baru wanatafuta mwingine wampune.

kifesi gari analo... na alilipata wakati anafanya wcb.. na kasafiri nchi kibao wakati yupo wcb.... mwarabu fighter alisimamishwa kwa kumdhulumu zola d kwa kutumia jina la wcb
 
Ila wanamuziki wanakopeshwa wanalipa kidogokidogo...kama Konde boy alivyompata mzungu akawalipa hela yote cash...mzungu akamnunulia michuma mingine...no free lunch
 
kifesi gari analo... na alilipata wakati anafanya wcb.. na kasafiri nchi kibao wakati yupo wcb.... mwarabu fighter alisimamishwa kwa kumdhulumu zola d kwa kutumia jina la wcb
Zola mbona yuko mtoni kipindi tu, zoezi beach kule zuga tu, alipata blonde mswiss yuko huko mpk leo
 
kuna kitu nimejiuliza sana,ina maana Lukamba sik zote hakuwa na gar licha ya kufanya kazi na mtu mkubwa Afrika? je ina maana yoyote kumzawadia gari jukwaani km tunavyozawadiwa wafanyakazi bora siku ya Mei Moko? kwa jinsi tukio la jana lilivyoteka umma Ali Kiba na kundi lake walikosea timming ya kurelease ngoma yake hadi imedoda huko youtube au alitaka public sympathy kwamba WCB wameaandaa tukio lile kumzima?😁🤕🙌
Hata mimi nimeshangaa kupita maelezo. Zile trips zote za Ulaya halafu hana gari!!!!!!!!!
 
Hata mimi nimeshangaa kupita maelezo. Zile trips zote za Ulaya halafu hana gari!!!!!!!!!

ulaya si anaenda kufanya kazi alioajiriwa ya kumshoot bosi wake for youtube na insta

na lukamba hana hata miaka miwili wcb...

kuna wafanyakazi wangapi wamedumu na waajiri wao miaka 10 au 20 na hata baiskeli hawana

ulaya haendi kucheza anaenda kufanya kazi kama ambavyo anaenda kumshoot tandale
 
Back
Top Bottom