Mpina: ACT Wazalendo tunaenda mahakamani kupinga Sheria ya Fedha 2026

Mpina: ACT Wazalendo tunaenda mahakamani kupinga Sheria ya Fedha 2026

Anachotakiwa kufanya ni sawa kuliko kukaa kimya wawekezaji wanasamehewa kodi kubwa wakati huo huo wanaongeza kodi kwa Wafanyabiashara wadogo kama walitoa mawazo wakapitisha waende court ingawaje ni ya kwao..
 
Mwenye uwezo wa kulipa kodi ati anapewa msamaha wa kodi, asiyejiweza ndiyo anabananishwa alipe kodi...


Cc: Mahondaw
 
Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amesema chama hicho kimepanga kufungua kesi mahakamani kupinga baadhi ya vipengele vya Sheria ya Fedha wa mwaka 2026, kikidai kuwa vinaongeza mzigo wa kodi kwa wananchi wa kipato cha chini huku vikitoa misamaha kwa wawekezaji wakubwa.

Soma: Mpina: Zungu na Kamati ya Bajeti, kukosoa bajeti baada ya kuipitisha ni kuwafanyia 'massage' Watanzania

Mpina amesema ACT-Wazalendo ilifanya uchambuzi wa muswada huo na kutoa mapendekezo 18 ya marekebisho, lakini serikali ilikubali kurekebisha maeneo sita pekee, huku maeneo 12 yakibaki bila mabadiliko. Amesema chama hicho kitapinga mahakamani kuanzishwa kwa baadhi ya kodi mpya pamoja na misamaha ya kodi iliyopendekezwa na serikali.

 
Back
Top Bottom