Mpina yuko salama sana, kila nikitazama future yake kama mwanasiasa namuona ameshajijengea heshima kubwa kwa wakati huu.
Mpina tayari ni shujaa miongoni mwetu, lakini isipokuwa kwa wachawi wachache sana, hii Tanganyika ya sasa sio ya wajinga ni ya werevu, wanauona werevu wa Mpina na ujinga wa Tulia na Samia, hawayumbishwi.
Namuheshimu sana Mpina, ameyaweka rehani maslahi yake yote kisiasa kwaajili ya kuipigania Tanganyika na rasiliamali zake, kumpigania mtanganyika na kodi na tozo zake, kumnyooshea kidole huyu ni dalili ya kwanza ya uchawi.
Napoona mtu kama Mwigulu akipiga makofi kwa nguvu kushangilia hatua aliyochukuliwa Mpina na Dr. Tulia, nazidi kupata nguvu za kusimama na Mpina, bungeni kuna blood suckers wasiojali chochote kuhusu hali ya mtanganyika, kama yule shetani aliyewahi kutuambia tuhamie Burundi.