GE2025 Mpina awekewa pingamizi na mwanachama mwenza kugombea urais kupitia ACT WAZALENDO

GE2025 Mpina awekewa pingamizi na mwanachama mwenza kugombea urais kupitia ACT WAZALENDO

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hawatakujibu hili.Wameukimbia uzi,nyumbu
Huez mjua mtu kwa haraka ivo, pia ishu ya mbowe kuna namna ulikua unaona anamaanisha hasa kipind cha magufuli but kilivyokuja kipind cha pwani ndipo watu wakaanza kugundua rangi yake ingawa pamoja na hayo wapo ambao hawalioni hilo!! But LISSU aliona hilo that's why hata alidiriki kusema walama asali!!!
 
Nami nakujibu, Wana Chadema mnasema Mbowe ni pandikizi la CCM baada ya Mbowe kuwa Mwenyekiti kwa miaka 20 mkimchagua ninyi wenyewe. Je, miaka yote hiyo hamkujua hadi mmekuja kujua leo?

Nasubiria majibu.
Mkuu hao Maprofesa washauri wa chama akina Profesa Baregu na wengine ndani ya chama kwa kipindi chote hawakuona hiyo kasoro bali Lissu makamu mwenyekiti eti ndio aliona mara tu alipoamua kugombea nafasi ya mwenyekiti. Hakuna ushaidi wa kudhibitisha kama Mbowe aliongwa na CCM au serikali ya CCM ni hearsay tu,kama kawaida porojo za Bongo.
 
Uzuri ni kwamba Hilo pandikizi Mbowe tumeliondoa CHADEMA, mlichukue huko CCM .
 
Mkuu hao Maprofesa washauri wa chama akina Profesa Baregu na wengine ndani ya chama kwa kipindi chote hawakuona hiyo kasoro bali Lissu makamu mwenyekiti eti ndio aliona mara tu alipoamua kugombea nafasi ya mwenyekiti. Hakuna ushaidi wa kudhibitisha kama Mbowe aliongwa na CCM au serikali ya CCM ni hearsay tu,kama kawaida porojo za Bongo.
Akina Lissu ni wanasiasa wajinga. Huyo Makamu Mwenyekiti wake John Heche ni mtu corrupt sana.
 
View attachment 3442992
View attachment 3442991

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo, Monalisa Ndala amepinga uamuzi wa chama hicho, kumteua Luhaga Mpina kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, akidai amekosa sifa.

Kada huyo amedai kanuni za chama hicho, zimekiukwa katika uteuzi wa Mpina, kinyume na taratibu na sheria ya uchaguzi inayoelekeza mtia nia anayependekezwa na chama cha siasa, kukidhi taratibu za kimchakato za ndani za chama husika.

Kutokana na hilo, jana terehe 14 Monalisa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu akimtaarifu kwamba Mpina hajakidhi kanuni za kudumu za uendeshaji wa hicho, toleo la mwaka 2015.

Katika barua hiyo, Monalisa amesema vipengele kadhaa vya kanuni namba 16 inayozungumzia sifa za mgombea ndani ya chama na wanaomba kuteuliwa kugombea ACT Wazalendo, vimekiukwa.

Soma Pia: Mpina ahamia rasmi ACT Wazalendo, kumvaa Rais Samia Oktoba 29, 2025

Akinukuu vipengele hivyo, Monalisa amesema,“Kanuni namba 16(4) mgombea urais / viongozi wa chama ngazi ya Taifa, lazima awe mwanachama wa ACT Wazalendo kwa muda usiopungua mwezi mmoja kabla ya tarehe ya mwisho ya uteuzi ya mgombea wa chama,”

Ameongeza kuwa, “Mgombea wetu aliyejiunga siku mbili kabla ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais baada ya kuenguliwa kuwania ubunge kwa chama chake cha zamani [CCM] Julai 28, 2025,” ameeleza Monalisa ambaye ni mwenezi wa ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha Monalisa ameendelea kusema kuwa Mpina amepingana na kanuni namba16 (4) (iii) inayosema awe tayari kutangaza mali binafsi na vyanzo binafsi kabla ya kuteuliwa kugombea kwa kufuata utaratibu ulioanishwa sehemu ya (vii) ya nyongeza ya Katiba ya ACT Wazalendo.

“Kwa bahati mbaya au makusudi mgombea wetu amevunja kanuni hii kwa kuwa hadi anatangazwa kuteuliwa kuwa mgombea, hakuna pahala popote ameonyesha kutangaza mali zake,” amefafanua Monalisa katika barua hiyo ambayo nakala imeenda Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).

Katika barua hiyo, Monalisa amedai kuwa Mpina amekiuka kanuni muhimu namba 16 (4) (iv)inayomuhitaji kuelewa itikadi, falsafa, misingi na sera za ACT Wazalendo kama inayosomea ‘awe ni mtu aliyethibitika kuielewa itikadi, falsafa, misingi na sera za ACT Wazalendo

USSR

Chama chenyewe cha CCM !!! toeni maigizo hapa
 
Swali lako nje ya kile ulichoelezwa hapo juu, Mimi naongelea mambo halisi wewe unaongelea hisia. Kwamba Bwana Mohamed alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar ni kweli, kwamba Maulida alikuwa kwenye Bodi ya wadhamini ni kweli na kwamba Bwana Lembrus Mchome hakuudhuria kikao Cha Baraza Kuu CHADEMA ni kweli.

Sasa wewe unaleta mambo ya hisia ya Mbowe kuwa pandikizi la CCM ambapo sio suala halisia Bali hisia za baadhi ya wanachama.
Mpina kawekewa pingamizi , hiyo ni game tuu.
Msajili wa vyama hawezi kuchukuwa hatua yoyote.
Maana CCM pia Samia kawekewa pingamizi.

Sasa Amuache mpina na amuche Samia.
Akimshitaki Mpina basi itabdi amshitaki Samia
 
Kweli leo ndio nimeamini Ndala ni Ndala tu ndio maana zikaitwa Malapa
 
Mpina kawekewa pingamizi , hiyo ni game tuu.
Msajili wa vyama hawezi kuchukuwa hatua yoyote.
Maana CCM pia Samia kawekewa pingamizi.

Sasa Amuache mpina na amuche Samia.
Akimshitaki Mpina basi itabdi amshitaki Samia
Walikua wanasubiria dakika ziishe tu waweke mpira kwapani
 
Back
Top Bottom