PostGE2025 Mpina: Hongera Gen Z, Historia ya Taifa haitawasahau Mashujaa wa Maandamano ya Oktoba 2025

PostGE2025 Mpina: Hongera Gen Z, Historia ya Taifa haitawasahau Mashujaa wa Maandamano ya Oktoba 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776

"Hongera sana Gen Z, hongera sana waandamanaji wote. Mmejitoa bila kujibakiza kwa taifa lenu; wengine mmepoteza maisha, wengine mmepoteza viungo vya miili na kuwa na ulemavu wa kudumu. Historia ya nchi yetu haitawasahau. Orodha yenu ipatikane na iunganishwe kwenye mashujaa wengine waliopigania taifa letu.

Watanzania wanahitaji viongozi weledi na wenye uwezo wa ziada, yaani willpower, kuwapeleka kwenye mafanikio ya kweli. Maandamano ya Oktoba 2025 ni ishara ya Watanzania kuchoshwa na serikali iliyoshindwa kuwajibika kikamilifu na ndio maana wakasikika wakiimba na kusema, 'Hatutaki Mama Samia, hatuitaki CCM, tumechoshwa na ufisadi nchini. Tunataka nchi yetu.' Wengine walisikika wakisema, 'Ndugu zetu wametekwa sana, wameuawa sana, na wengine hawana familia.' Tukaona Watanzania kwa pamoja tuungane tushirikiane, 'Hatumtaki Rais Samia, tunataka nchi yetu.'
 
Back
Top Bottom