Mpina: Kifungu kilichotumiwa na Spika Tulia kunituhumu na kunihukumu hakipo!

Mpina: Kifungu kilichotumiwa na Spika Tulia kunituhumu na kunihukumu hakipo!

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Luhaga Mpina alipewa adhabu na Bunge Juni 24, 2024 baada ya kwenda kinyume kwa kuwasilisha taarifa yake kwa wananchi mara baada ya kuikabidhi katika Kamaati ya Bunge. Zaidi soma - Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15

Usiku huu tukio linarushwa live mpina akiongelea suala hilo kwa mara ya kwanza baada ya adhabu yake kuanza rasmi. Fuatilia uzi huu kwa updates zaidi.

====

Screenshot 2024-06-30 031208.png

Kamati iliongeza mashtaka tofauti za aliyoagiza Spika - kwenda kinyume na kufungu cha 29 D na E na kifungu cha 34(1) G cha Sheria na Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge sura ya 296 na siyo tuhuma zilizokuja kuongezwa baadaye kwamba ni kifungu Kifungu cha 26 D na E na Kanuni ya 84(1) J na K.

Kifungu cha 29 D na E cha Sheria na Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge sura namba 296 ambacho Spika alirejea kumtuhumu nayo hakiendani na maudhui ya tuhuma zilizotolewa katika taarifa ya Spika, kifungu hicho kinazungumzia makosa ya Waandishi wa Habari wanapoingia katika vikao vya Bunge bila kufuata utaratibu!

Kifungu hicho hakitengenezi kosa la kijinai wala kinidhamu kwa Mpina, hivyo haikuwa sahihi kwa Spika kumtuhumu kwa makosa yaliyokwa kwaajili ya waandishi wa habari akijiua fika Mpina ni Mbunge.

Hivyo kifungu hicho alichotumia Spika kumtuhumu na kumhumuku hakipo na kwa makosa ya nidhamu ambayo hayapo!

Vilevile Kifungu cha 34(1) G nacho hakihusiani na machapisho ya kila taarifa bali kinahusu kosa la kuchapisha kwa umma taarifa zilizoandaliwa mahususi kwaajili ya kuwasilishwa bungeni. Kifungu hiki hakihusiani na kosa la kinidhamu bali ni kosa la jinai kwa mtu yoyote atakayechapisha taarifa hizo tajwa ambapo ni taafira/nakala mahususi/rasmi kwaajili ya kupelekwa bungeni.

Wasilisho la Mpina kwa Spika alilotoa kuwasilisha vielelezo vya ushahidi kikanuni haliwezi kuwa taarifa rasmi ya bunge, ni mawasiliano ya kawaida ambayo yanawezwa kufanywa kati ya mbunge na mbunge, Rais au taasisi nyingine.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 70, toleo la 223 inabainisha kuwa uthibitisho wa uongo siyo jambo la siri, linaweza kutolewa bungeni ambapo vyombo vya habari vipo na wananchi wanafuatilia. Hakikatazi kama Spika atatoa muda zaidi wa uwasilishaji huo, kwa Mpina kuongea na wanachi kabla au baada ya uwasilishaji huo kwa Spika.

Lakini pia upo ushahidi wa Wabunge ambao wamewahi kutoa ushahidi huo ndani ya bunge mbele ya waandishi wa habari na mijadala kuendelea hata nje ya bunge lakini hawajahi kushughulikiwa kinidhamu kwa kuliingilia bunge! Mfano tar 3 Juni, 2024 Mbunge Ole Sendeka alitoa ushahidi bungeni na kwenda mbali zaidi na kusoma baadhi ya barua bungeni ambapo waandishi wa habari walichukua tukio hilo, lakini hakuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu.

Mpina anaujulisha umma kuwa hakutenda kosa lolote au kuvunja kipengele chochote cha kanuni ya 70 toleo la 223 ambacho ndiyo msingi wa agizo la Spika la la tar 14, Juni 2024.

Hata hivyo vielelezo ambavyo Mpina aliwasilisha kwa Spika hakuvitoa na kuvichapisha kwenye vyombo vya habari kwakuwa alijua huenda baadaye vitatumika kwaajili ya Kamati, Mahakamani au Bungeni.

Misingi ya mabunge yote Duniani imejegwa kwa uwazi, ukweli, uwajibikaji na Demokrasia, Mpina anasema inashangaza kuona Spika ambaye anasisitiza mambo kufanyika gizani

Kanuni ya 83(2) toleo la 2023 Taarifa ya spika imeeleza adhabu iliyopo katika kanuni ya 83(1) - wakati spika anaongea alisema apewa adhabu katika kanuni ya 83(2)
a) Kumuonya mbunge na kutaka ajirekebishe
b) Kumuamuru mbunge huyo kutoka nje ya ukumbi mara moja au abaki huko kwa muda wa kikao uliyosalia
c) Kumsimamisha kuhudhuria vikao visivyozidi 10 mfululizo

Kwa Spika kuruka adhabu za mwanzo na kwenda moja kwa moja kwenye adhabu ya 3, inaleta tafsiri kuwa Spika alikuwa akielekza kamati adhabu gani iamuliwe. Kaulli hiyo inafanya kamati ikose uhuru wa aina gani ya adhabu itolewe kutemea na ukubwa wa makosa.

Katika taarifa ya Spika hakuna mahala popote alipoweka rejea ya Mpina kuvunja kanuni yoyote ile ya bunge wakati akitoa taarifa yake bungeni.

Kifungu cha 26(D) na (E) sura 296 kilichoongezwa, kinatumika tu pale ambapo wasilisho la Mpina lingekuwa linamlenga Spika. Lakini je, wasilisho la Mpina dhidi ya waziri Bashe lililoisha kwa pongezi kwa Spika kwa uzalendo wake linahusika vipi vipi na kumvunjia heshima Spika?

Kitendo cha Mpina kufichua Waziri waliyekuwa amevunja Sheria za Bunge ilikuwa ni kitendo cha kulinda Heshima za Bunge, na siyo kubadilisha aliyefichua kuwa ndiyo mwenye makosa kwa kulidhalilisha bunge.

Spika alisema kosa lizingatie kanuni ya 83 lakini kamati ikazingatia kanuni ya 84, na hivyo kuleta kosa jingine ambalo Spika hakulitaja kwenye taarifa yake.

Kwa Spika kupeleka mashtaka na kutoa hukumu haikuwa sawa, kwa kufanya hivyo amesababisha haki isitendeke. Ambapo Mpina alihukumiwa bila kusikilizwa jambo ambalo linaenda kinyume na Katiba ya nchi.

Mbunge Mpina anasema alitegemea Spika angechukizwa Waziri Bashe pamoja na Waziri Mwigulu kutokana na ushahidi uliyopelekwa mbele yake, ambapo angetoa msimamo wa bunge, badala yake akachukiwa yeye aliyepeleka ushahidi.

Kasoro zilizojitokeza katika mjadala wa azimio la bunge 24 June, 2024
1. Taarifa ya Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge haikuwa sehemu ya shughuli za bunge (order paper) ya 24 June, 2024 hivyo kufanya wabunge wengi kutokuwa na taarifa ya kuwasilishwa kwa hoja hiyo.

2. Spika hakutoa utaratibu wa mwongozo wa namna ya kuchangia taarifa ya Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge badala yake alisema anayo orodha ya majina ya wabunge watakaochangia bila kueleza orodha hiyo ameipataje.

3. Spika aliwaruhusu baadhi ya wabunge kutumia maneno ya kutweza utu na lugha zisizo ruhusiwa bungeni kinyume na kanuni ya 71(1) I na J ya kanuni za kudumu za bunge toleo la 2023, wabunge waliopata nafasi ya kuchangia waliacha hoja ya msingi na kumshambulia Mpina huku Spika akiacha hali hiyo iendelee na kushindwa kutoa uamuzi kinyume na kanuni ya 78 ya kanuni za kudumu za bunge huku akijua ni kinyume na kanuni.

4. Spika hakumpa Mpina nafasi ya kuchangia hoja hiyo na kutolea ufafanuzi hata kwa baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yakipotoshwa

5. Wabunge waliochangia hawakuwa na taarifa za kutosha kuweza kutoa maoni yao, sababu taarifa ilitolewa kwa kifupi bila kuwa na upande wa mpina pamoja na vielelezo alivyowasilisha.

6. Baadhi ya wabunge walisema wao ni Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM na kwamba watenda kumshtaki kwenye vikao vya NEC kwa kutoa uthibitisho wa ulaghai na rushwa pamoja na uvunjifu wa sheria, badala ya waziri husika kuchukuliwa hatua. Waliingiza mambo ya chama kwenye mambo ya kiserikali huku wakijua ajenda za vikao vya NEC huwa ni za siri

7. Kitendo cha kumsimamisha mbunge vikao 15 mfululizo ilipaswa kujiridhisha pasi na mashaka ama bunge kuziona kasoro hizo zilizosababishwa na mbunge

Mpina awahakikishia wananchi kuwa haya yote yaliyotokea na aliyotendewa hayawezi kumtoa kwenye mstari wala kumrudisha nyuma katika harakati za kuhakikisha kwamba maendeleo yanapatitaka

Mpina aazimia yafuatayo;
- Kupeleka malalamiko yake ya kuondolewa bungeni kwa uonevu na kutokutendewa haki na Spika wa Bunge kwenye vyombo vya sheria ili vikapime na kutoa haki kwa mujibu wa katiba ya Tanzania na sheria za nchi

- Kumpeleka mahakamani waziri wa kilimo ndg Hussein Bashe na bodi ya sukari chini ya ibara ya 26 na 27 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kitendo cha kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha sheria na kulisababishia taifa hili hasara kubwa

- Kuyafikisha hakamani makampuni yote yaliyojihusisha na ungizaji wa sukari nchini kinyume cha sheria.

====

Pia soma: Mpina kuwapelea Mahakamani Waziri Bashe na Bodi ya Sukari kwa kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha Sheria
 
Attachments

Wakuu,

Luhaga Mpina alipewa adhabu na Bunge Juni 24, 2024 baada ya kwenda kinyume kwa kuwasilisha taarifa yake kwa wananchi mara baada ya kuikabidhi katika Kamaati ya Bunge. Zaidi soma - Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15

Usiku huu tukio linarushwa live mpina akiongelea suala hilo kwa mara ya kwanza baada ya adhabu yake kuanza rasmi. Fuatilia uzi huu kwa updates zaidi.

Kamati iliongeza mashtaka tofauti za aliyoagiza Spika - kwenda kinyume na kufungu cha 29 D na E na kifungu cha 34(1) G cha Sheria na Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge sura ya 296 na siyo tuhuma zilizokuja kuongezwa baadaye kwamba ni kifungu Kifungu cha 26 D na E na Kanuni ya 84(1) J na K
 
Wakuu,

Luhaga Mpina alipewa adhabu na Bunge Juni 24, 2024 baada ya kwenda kinyume kwa kuwasilisha taarifa yake kwa wananchi mara baada ya kuikabidhi katika Kamaati ya Bunge. Zaidi soma - Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15

Usiku huu tukio linarushwa live mpina akiongelea suala hilo kwa mara ya kwanza baada ya adhabu yake kuanza rasmi. Fuatilia uzi huu kwa updates zaidi.

====

Kamati iliongeza mashtaka tofauti za aliyoagiza Spika - kwenda kinyume na kufungu cha 29 D na E na kifungu cha 34(1) G cha Sheria na Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge sura ya 296 na siyo tuhuma zilizokuja kuongezwa baadaye kwamba ni kifungu Kifungu cha 26 D na E na Kanuni ya 84(1) J na K

Kifungu cha 29 D na E cha Sheria na Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge sura namba 296 ambacho Spika alirejea kumtuhumu nayo hakiendani na maudhui ya tuhuma zilizotolewa katika taarifa ya Spika, kifungu hicho kinazungumzia makosa ya Waandishi wa Habari wanapoingia katika vikao vya Bunge bila kufuata utaratibu!

Kifungu hicho hakitengenezi kosa la kijinai wala kinidhamu kwa Mpina, hivyo haikuwa sahihi kwa Spika kumtuhumu kwa makosa yaliyokwa kwaajili ya waandishi wa habari akijiua fika Mpina ni Mbunge.

Hivyo kifungu hicho alichotumia Spika kumtuhumu na kumhumuku hakipo na kwa makosa ya nidhamu ambayo hayapo!

Vilevile Kifungu cha 34(1) G nacho hakihusiani na machapisho ya kila taarifa bali kinahusu kosa la kuchapisha kwa umma taarifa zilizoandaliwa mahususi kwaajili ya kuwasilishwa bungeni. Kifungu hiki hakihusiani na kosa la kinidhamu bali ni kosa la jinai kwa mtu yoyote atakayechapisha taarifa hizo tajwa ambapo ni taafira/nakala mahususi/rasmi kwaajili ya kupelekwa bungeni.

Wasilisho la Mpina kwa Spika alilotoa kuwasilisha vielelezo vya ushahidi kikanuni haliwezi kuwa taarifa rasmi ya bunge, ni mawasiliano ya kawaida ambayo yanawezwa kufanywa kati ya mbunge na mbunge, Rais au taasisi nyingine.

Moto!
 
Back
Top Bottom