Mpina kuwapeleka Mahakamani Waziri Bashe na Bodi ya Sukari kwa kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha Sheria

Inavyoonekana hujamsikiliza Mpina kwenye taarifa yake, anadai kuhukumiwa Kwa vifungu vya kanuni za bunge au Sheria ambazo kimsingi hazipo au haziapply kwenye tafsiri ya msingi ya kosa lake la kumdharau speaker/kupoka mamlaka ya speaker na hadhi ya bunge. Suala la kuwasilisha nyaraka za ushahidi wake Kwa speaker na wakati huo yeye kufanya press release kwa vyombo vya habari ya ushahidi huo huo Kwa maelezo yake yalipaswa kufanyiwa tathmini na tafasiri ya kisheria na kikanuni kama amefanya kosa na siyo kwa hisia. Mimi nadhani Kwa taarifa yake Kwa Sasa si busara kumhukumu bali vyombo na mamlaka husika za serikali na bunge kuingia kazini kupitia tafasiri za kikanuni za bungez Sheria na katiba ya nchi ili mamlaka hizo kuja na majibu ya kiupembuzi yakinifu ili kuondoa hisia za Mpina kuonewa kama mwakilishi na mtanzania anayelindwa na haki za raia wa nchi hii.
 
Mpina hiyo System mliokuwa mkiipigia Meza kwasababu inadili na kuumiza Wapinzani sasa ndio utaenda kuielewa na ni kwanini sisi tunadai KATIBA MPYA.

Hakuna Mahakama Hakuna Bunge vyote ni Matawi ya CCM.
 
MPINA sio mwanasiasa wa Njaa .

Rejea rekodi zake huko nyuma nahata Sasa.



MPINA hapiganii Supadoli, anapigania wale Wakulima wa Miwa, wapatao elfu 13+
Ni mwanasiasa FISADI ndiyo maana hana njaa. Umesema vizuri.

Kama rekodi yake ni nzuri tuambie aliwezaje kumiliki ekari zaidi ya 1,000 huko Morogoro kwa mshahara wa Ubunge/ Uwaziri
 
Mni mwanasiasa FISADI ndiyo maana hana njaa. Umesema vizuri.

Kama rekodi yake ni nzuri tuambie aliwezaje kumiliki ekari zaidi ya 1,000 huko Morogoro kwa mshahara wa Ubunge/ Uwaziri
CCM wote Mafisadi
 
Mni mwanasiasa FISADI ndiyo maana hana njaa. Umesema vizuri.

Kama rekodi yake ni nzuri tuambie aliwezaje kumiliki ekari zaidi ya 1,000 huko Morogoro kwa mshahara wa Ubunge/ Uwaziri
Kwanini wewe uliwezaje kumiliki. Yale mapepo yako
 
Nakubaliana na wewe serikali ilipaswa kuchukua hatua za dharura kuinusuru nchi Kwa tatizo la upungufu wa sukari uliokuwepo. Lakini swali la msingi ni je, serikali ilishindwa kuchukua hizo hatua za dharura wakati huo ikizingatia Sheria zilizopo??? Nadhani hiyo ndo concern kubwa ya Mh. Mpina. Huwezi ukadeal na dharura wakati huo unatumia njia ambazo ni questionable zenye harufu ya rushwa na ufisadi. Tukiruhusu mazingira ya namna ya kutozingatia utawala Bora wa Sheria, taratibu na kanuni baadhi ya viongozi watatumia udhaifu huo kufanya ufisadi wa kujinufaisha na jamaa zao wachache Kwa mgongo wa dharura za kutengenezwa/manipulation. Haijarishi ni dharura lkin Sheria lazima zizingatiwe na kama Sheria zilizopo zikionekana zina udhaifu ktk kukabiliana na dharura basi schedule of amendments ya kipengele hicho ijadiliwe na bunge na kuridhiwa, mtu mmoja hawezi akabadili Sheria na tukachukulia poa.
 
Mpina anajiamini sana, sema yuko vizuri upande wa pili, watu wanaotokea kanda ya ziwa wameshanielewa
 
umejieleza taratibu vizur sana aise gentleman

katika hali ya dharura ndipo mpina anaenda kukwamia mahakamani
 
Niwakumbushe kwa sasa ndio Bunge liko kwenye vikao vya kutunga sheria kuruhusu bodi ya Sukari kununua Sukari. In any way lazima mtu aje aende jela kwa ufisadi huu
Kuna mkanganyiko mkubwa wa kimamlaka na majukumu ya NFRA(National Food Reserve Agency), board ya sukari na sheria zake ndo maana hata speaker alitoa mwongozo juu ya uhalali wa NFRA kununua sukari ya reserve na kuitoa wakati wa upungufu Ili kuweza kustabilize inflation. Inabidi wabunge wawe makini ili kusitengenezwe Sheria ambazo mwisho wa siku zitawapa mafisadi mianya ya kuzitumia ndivyo sivyo Kwa maslahi ya wachache
 
Sababu ya kujadili hili ni kama wanahangaika ku counter hoja za Mpina.

But for me kila atakaye taka kufanya cover up kosa la Bashe anakuwa anajiingiza kwenye mtego wa kisheria

Wabunge wetu ni wajinga au wanauwezo mdogo wa kujadili mambo mazito.

Wanaamini kuingiza Sukari nyingi kutasaidia kushuka kwa Sukari wakati soko siku zote huongozwa na supply and demand and profit.

Suluhu ya Sukari ni uzalishaji wa ndani uwe mkubwa na Kodi ziwe chini
 
Kwaio mkuu mpina Hana hoja yeyote ??!
inaonekana ana malalamiko, kinyongo na chuki binafsi kwa muda mrefu sana, ndio maana anaweza kukiri kukosea halafu hapohapo akadai kuonewa

hata hivyo katika hali ya dharura ambayo ingeweza kuleta matatizo nchini, halafu ati ulete chuki na vinyongo
vyako binafsi mahakamani? mahakama itamtuliza tu, ataondoka kanywea kama sio yeye vile
 
Ukisha ona watu wapo ODDS AGAINST ONE
Bora akae kwa kutulia kabisa kabisaa maana atapata MATATIZO
 
Kwann asihutumie muda huu kukaa karibu na wapiga kura wake ? Kuliko kushindana na serikali,anaamini ataishinda huko mahakamani? Kama wabunge wote pamoja na kwamba wa chama chake hawakumuunga mkono
Mbunge anawajibika Kwa wananchi wa Jimbo lake, chama chake na Taifa kwa ujumla. Sheria anazoshiriki kupitishwa bungeni si tu kwa maslahi ya watu wa jombo lake bali kwa wananchi wote wa JMT, Kwa msingi huo basi bado Mpina ni wa maana na mhimu kabisa Kwa watanzania wote ili mradi anaweka maslahi ya waTz mbele. Haijalishi hoja zake akipeleka mahakamani hatashinda lkn atakuwa ametimiza wajibu wake kwa misingi ya haki na Sheria za nchi. Anachotaka ni tafasiri ya kisheria ambazo mamlaka za bunge zimemtuhumu ili kupata ukweli au udhaifu uliojitokeza dhidi ya makosa yake na hoja zake za kumtuhumu waziri husika, tuache mihemuko na kupre-empty matokeo ya mhimili wa mahakama itakayosikiliza hilo Sheria, hakuna mamlka iliyo juu ya Sheria mind you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…