GE2025 Mpina na Kalikawe ni wagombea urais kupitia Act Wazalendo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Uhuni tu wa Zitto na ccm.
Mpina kumbe ni Zoba kiasi hiki?
 
Uhuni tu wa Zitto na ccm.
Mpina kumbe ni Zoba kiasi hiki?
Zitto atakuwa kamuingiza Kingi.

Au Labda kaahidiwa fungu nono.

Kwa sababu anajua wazi kuwa hawezi kupewa urais hata kama akipata kura asilimia 99.

Jamaa kajimaliza kisiasa kushiriki "kumtakatisha" bi mkubwa katika uchaguzi wa kimagumashi.
 
Halmashauri Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo kwenye kikao maalum kilichofanyika jana tarehe 5 Agosti 2025 kwenye ukumbi wa Hakainde Hichilema pamoja na mambo mengine ilipendekeza majina ya wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa Shangwe Ayo, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo, kwa upande wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, majina yaliyopendekezwa ni;

1. Aaron Kalikawe

2. ⁠Luhaga Mpina

Kwa upande wa Urais wa Zanzibar Halmashauri Kuu imependekeza jina la Ndugu Othman Masoud Othman ambaye ndiye mwanachama pekee aliyechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.

Ndugu Othman Masoud Othman pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Majina ya wagombea yaliyopendekezwa yatawasilishwa kwa Mkutano Mkuu Taifa kwa ajili ya kupigiwa kura.

Katika hatua nyingine, Halmashauri Kuu ilipokea na kuridhia hatua ya mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Dorothy Jonas Semu kujitoa kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kwenye maelezo yake mbele ya Halmashauri Kuu Ndugu Dorothy Semu ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo aliieleza Halmashauri Kuu kuwa alichukua hatua hiyo katika kutekeleza wajibu wake wa kiuongozi wa kukiwezesha Chama kutekeleza wajibu wake wa kimapambano wa kuiondosha CCM madarakani kwenye Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuzingatia mazingira ya kisiasa ya sasa nchini.
 
Ila vyama vya upinzani vinayumba Sana. Mtu anajiunga Leo Kisha anapewa ugombea urais. Huu ni udhaifu mkubwa Sana.
Sasa kama mfadhiri amewataka wafanye hivyo, maana hata Mimi nashangaa hizo sera za Chama na itikadi zake kajifunza lini. Mpina naye kumbe hovyo tu. Hicho Chama nacho hovyo tu, waache waendelee kusindikiza, Chama sindikizi
 
Mpina Bora angeomba kugombea ubunge angeeleweka kiurahis ila hapo ameyabananga tu
 
Deal Done, huku ACT kule Chauma.
Taifa stars watashinda na hata kuchukua ubingwa, October hii hapa Iyena Iyena, TL anachiliwa.

ACT na Chauma watakuwa bungeni, CDM inakuwa crippled with financial crisisand some top dogs will run to either ACT or Chauma, and others will decide to remain silence, game over.

ndani ya mitaa Kabul Afghanistan.
 
M
Mpina kwisha habari yake,nibora angeligombea ubunge angeliweza kutetea kiti chake kwa Urais ni maji marefu.
 
Moja ya wrong approach inayotumiwa na CDM ni kutegemea EU na US, na hapa ndio ninapowaona bado watoto sana.

EU na USA wako kimaslahi, wanapopata maslahi yao wanakaa hata upande wa shetani, kwasasa huwezi kuwaweka EU na USA nje ya CCM maana wanapata kila kitu kupitia CCM.

ndani ya mitaa ya Kabul Afghanistan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…