Mpina na watu wengine wenye kariba kama yake wasisumbuke, ni bora wakae kimya

Mpina na watu wengine wenye kariba kama yake wasisumbuke, ni bora wakae kimya

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Mpina hana Back up laiti angezaliwa Kenya angekuwa na kundi la watu milion 1 nyuma yake hao ni active, Kwa Bongo Mpina yuko mwenyewe sana sana ana Keybord Worrior nyuma yake wengi sana kama milion 3 hivi.

Ushauri wangu kwa Mpina na watu wengine wenye kariba kama yake wasisumbuke, kutetea Maiti, ni bora wakae kimya au wapiganie ugali wa watoto wao ila sio kutetea wajinga wa hii nchi. Au basi akateta hata Tembo wasiuwawe anaweza pata thawabu kutoka kwa Mungu.

Kuwa mwanaharakati Tanzania ni ujinga bora kuwa mwana harakati wa kutetea mbwa wa mtaani na Paka ila sio kutetea Wabongo. huwa nawashangaaa sana wanao watetea wabongo nawashangaaa sana tena mno.

Bora kama inawezekana vuka mipaka kawatetee hata Wakenya au Waganda ila sio Wabomgo.

PIA SOMA
- Spika Tulia amburuza Luhaga Mpina Kamati ya Maadili

- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya

- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia

- LIVE - Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15
 
Watanzania hatupendi ukwel ila katika hili Bashe yupo sahihi sema bas tu alizingua kwenye baadhi ya utaratibu, hawa wafanyabiiashara wa sukari ni mashetani
 
Kwahiyo unasema Mpina awe CHAWA?

Sijasikia Maria, Upinzani, Shangazi, sijui Mange wala nani kumpa sapoti Mpina au kupaza sauti kwa maslahi mapana ya wasio na vipaza sauti nchini hapa!

Ngoja izungumzwe URAIA PACHA sasa, wazazi kuwekwa kwenye kona n.k, hutoamini hizo kelele zao
 
Tanzania inahitaji kumpata Jerry Rawlings... awafungie mule ndani afanye kazi yake halafu national reconciliation ndo Ianze.. labda ndio akili zitakuja...
 
Kwahiyo unasema Mpina awe CHAWA?

Sijasikia Maria, Upinzani, Shangazi, sijui Mange wala nani kumpa sapoti Mpina au kupaza sauti kwa maslahi mapana ya wasio na vipaza sauti nchini hapa!

Ngoja izungumzwe URAIA PACHA sasa......, wazazi kuwekwa kwenye kona n.k, hutoamini hizo kelele zao
Kwa sababu Maria na Mange ndio wamezaliwa kwa kazi hio, si ndio?
 
Mimi nakumbuka Mh Mpina alisema huu ni mwanzo tu, nasubiri ashushe nondo zaidi haijalishi ni wangapi wapo nyuma yake lakni ujumbe unafika
 
  • Thanks
Reactions: I M
Mimi nakumbuka Mh Mpina alisema huu ni mwanzo tu, nasubiri ashushe nondo zaidi haijalishi ni wangapi wapo nyuma yake lakni ujumbe unafika
Ili muwe mnakaa nyuma ya keybord kumpigania? hatafanikiwa kamwe na anahatarisha unga wa watoto wake, bora akawapiganie Mbwa wa mtaani
 
Back
Top Bottom