Mpina hakutetea wananchi bali alitetea viwanda vya ndani vya sukari, Sheria na taratibu kufuatwa. Bashe ndiyo aliyetutetea Ili wananchi tupate sukari ya bei nafuu.
Binafsi nasema hivi kama kweli bashe alifanikisha kuingiza sukari na sisi wananchi tukaipata Kwa bei nafuu basi naungana na bashe, kamwe siwezi kuungana na mtu anayetaka nitumie pesa zangu nyingi Kwa kitu ninachoweza kukipata Kwa bei nafuu.
Ujinga wa kutetea viwanda vya ndani wala siuafiki hata kidogo. Inakuwaje sukari kutoka nje tena ina gharama ya usafiri inakuwa na bei ndogo kuliko ya ndani? Kama tatizo ni teknolojia kwanini wasitafute teknolojia wanayotumia wenzao huko kuzalisha?
Huu ujinga wa kutetea viwanda ipo siku mtasababisha watanzania wakose nguo za kuvaa na watembee uchi, nchi ikose mafuta ya kula na vinginevyo. Kamwe viongozi hawapaswi kuvibeba viwanda ambavyo havibebeki tutaumia wananchi, haiwezekani soko lipo kubwa halafu unashindwa kufanya biashara wakati wengine wanatafuta wateja