johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 841
- 909
Najaribu kukumbuka tu. Katika historia ya bunge letu, hakujawahi kutokea mbunge kama Chrisant Majiyatanga Mzindakaya mbunge wa Kwela mkoani Rukwa.
Sio tu kwamba ni mbunge aliyekaa bungeni kwa miaka 45, bali alipelekea mawaziri kadhaa kujiuzulu kubwa ikiwa ni kashfa ya Sukari.
Mpina sio mbunge wa kwanza kukabiliana na kashfa ya sukari, Mzindakaya maarufu mzee wa mabomu, alimlipua waziri wa Viwanda na biashara Idd Simba kwa kutoa vibali vya kuagiza sukari kwa makampuni kinyume cha sheria.
Kama alivyo mpina, mzee huyo wa mabomu pia alimg'oa waziri wa fedha Prof. Simon Mbilinyi kwa kashfa ya minofu ya samaki.
Anachofanyaa leo mpina, ni matokeo ya ufisadi uliodumu tangu zama hizo ndani ya serikali, kampuni ya simu kupewa zabuni ya kuingiza sukari!
Najua, Mpina atapitia tanuri la moto kwa hata watu wake wa karibu kumzodoa na kumpiga, lakini inajulikana sifa za ukweli kuwa atapingwa lakini mwisho wa siku, ukweli utasimama.
Go go go Mpina, yawezekana Mzandakaya amefufuka.