Aliyekuwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amelituhumu Bunge na Spika kwa kupitisha Sheria ya Fedha ya Mwaka 2026 na bajeti ya Tsh. Trilioni 62.33 bila kufanya mabadiliko yoyote, licha ya uwepo wa malalamiko makubwa kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma.
Mpina amebainisha kuwa bajeti hiyo imetenga matumizi makubwa kwa ajili ya shughuli za anasa, ikiwemo kiasi cha Tsh. Trilioni 1.03 zilizotengwa kwa ajili ya kugharamia safari za viongozi wa serikali.