Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 7,207
- 17,674
Tarehe 4, july, 2024 nikiwa kwenye treni ya umeme (SGR)ya Dar - Morogoro ambapo abiria wanatumia saa moja na dakika 49 tu kufika, hivyo kuokoa muda mwingi wa uzalishaji uliokuwa unapotea barabarani kwenye foleni, kwenye siti pembeni yangu alikaa kijana ambaye kwa muonekano yupo umri wa above 25 ambaye muda wote alionekana mwenye huzuni sana na majuto mengi.
Baada ya kufika kituo cha Soga mkoani Pwani nikamuona kijana ameanza kuangua kilio na ndipo ilibidi nimuhoji na abiria wenzangu wakataka kujua ni nini kinamsibu kijana huyu, kijana alieleza kuwa nafsi inamsuta kupanda hii SGR kwani alipinga ujenzi wake akiongozwa na Tundu Lisu na Chadema kwa ujumla alishiriki kumtukana hayati Rais Magufuli na kumkejeli pale alipoanzisha ujenzi wa reli ya umeme wakati huo ikiwa awamu ya tano!
Kijana anasema sasa analia na kusaga meno kwani Magufuli hayupo tena duniani na hajui atamuombea wapi msamaha ili nafsi yake iwe huru kwani mradi wa sgr Dar - Moro umekamilika na kuwa wenye manufaa makubwa kwa watanzania masikini na matajiri bila kujali vipato vyao.
My take
Kwa maoni yangu vijana wa namna hii wako wengi wanapanda ndege, treni, flyover na kuwasha umeme wa bwawa huku nafsi zao zinawasuta sana maana walidanganywa na wanasiasa matapeli wasio na maono wala uzalendo wowote kwa taifa la Tanzania wakaishia kumtukana hayati Magufuli kwamba ni mshamba badala ya kutumia nguvu zao kuungana na Magufuli kujenga nchi wao wakatumia nguvu zao kumtukana na sasa wanajuta.