Mpinzani halisi wa Alikiba ni MarLaw, sio Diamond...

Mpinzani halisi wa Alikiba ni MarLaw, sio Diamond...

Tunaokumbuka, tunakumbuka.

Muziki na ushindani wa kweli ulikuwa enzi za Alikiba na Marlaw kwa upande wa nyimbo za kuimbaimba. Ni miaka ya 2009 kurudi nyuma huko. Kabla ya Belle 9 na kina Ben Pol kutengenezwa kimkakati kisha kuja Diamond baadaye.

Alikiba na Marlaw walichuana kwenye ligi moja na kina Z-Anto, Matonya, MB Doggy, Sumalee, Pingu na Deso, 2 Berry, AT, PNC, Q-Jay, Makamua, Kassim Mganga, Joslin na wengine wengi.

Marlaw, kama wasanii wengine wengi, walidrop kuanzia 2010. Bahati mbaya wengi walihusisha kudrop kwake kimuziki na siasa za uchaguzi kwa kuwa yeye alikuwa msanii namba 1 kwa wakati ule. Tulitafakari vizuri hapa mwaka 2015 tukaona sio kweli. Mjadala huo upo hapa > Je! Ni kweli Msanii Marlaw alipotezwa na Siasa?

Kwa sababu zozote zile, hazibadilishi ukweli kwamba Marlaw mpaka leo hii ni msanii anayependwa na kumissiwa zaidi na mashabiki kuliko msanii yeyote wa wakati wake. Huo ndio ukweli. Pita mitaani na mitandaoni halafu azungumziwe hata kwa bahati mbaya, maoni ya watu yatathibitisha.

Ni muda mrefu sasa tumekosa ladha ya mchuano wa vipaji halisi kwa sababu ya mambo mengi yaliyotokea kwenye industry ya muziki wa Bongo Fleva kwa miaka hii michache. Lakini shilingi si imeshageuka sasa? Kama Ally Kiba alipotea na kurudi, why not Marlaw?

Tumeona Ally Kiba tangu arudi amekuwa akipata ushindani usiofanana nae. Diamond sio muimbaji mzuri kama Ally Kiba. Japo ni the best kwenye anachokifanya. Marlaw ndiye muimbaji anayeweza kumchalenji zaidi Ally Kiba kwa sasa, kama ilivyokuwa zamani.

Nasisitiza, Marlaw ndio mtu sahihi wa kushindanishwa na Ally Kiba kimuziki. Aliyemshauri Marlaw kujipanga upya na kurudi kwenye game alifanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Kurudi kwake kutaanza kurudisha uhondo wa ushindani wa kweli wa muziki huu tulitotoka nao mbali.

Nimefurahi kuona Master Jay kupitia Marco Chali (MJ Records) nao wameshiriki kwenye movement hii ya kumtengenezea wimbo wake mpya aliochagua kurudi nao. Mpaka sasa wimbo unakimbia sana huko YouTube. Sijapata ripoti za kwenye redio na Bodaboda. Social media umeanza kuzunguka. Mpaka kuona mtu kama Maxence Melo anaposti cover ya Marlaw, inaleta picha gani?

Marlaw - Taa (with lyrics)

Namshauri Ally Kiba asichukulie vibaya kurudi kwa ushindani huu kati yake na Marlaw. Wote wana nidhamu na sio watu wa show off na drama. Amuache Diamond apambane na wengine akiwemo Harmonize wake.

Team Diamond na WCB msinielewe vibaya!
Diamond hakuna wakushindana nae Tanzania na hatatokea kamwe ko wewe alikiba kaa na hiyo miaka 40+ ukauze nguo kariakooo ebooooooh.
 
Well, am not sure why was it crucial to have diamond name on your thread title if your intention were to only say marlaw is of the same class as kiba.

I mean.. Must you write his name if he ain't good at music as you're preaching?? You could have just ignored him.. Clearly, there is no point in whatever you said. I don't see nothing but crap on the whole post.
I am afraid you misinterpreted the message here. Please take your time up, and read again.
 
Umeona Uzi wako utachacha Bila kumtaja diamond platnumz si ungezungumzia huyo marlaw na alikiba Bila kumuhusisha msanii wa kimataifa diamond watu wangekuelewa
Ali Kiba na Diamond ndio big names kwenye industry hivi sasa. Hata nisingemtaja Diamond, kuna watu wangekuja kumtaja tu humu. Hakwepeki!
 
Write your reply...ni kweli Daimond sio wakufananisha au kumlinganisha na na mwanamuziki yeyote ndani ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla,,,
Mwache alikiba ashindanishwe na Marlow
Hoja sio Ali Kiba au Marlaw ni bora kuliko Diamond..

Hoja ni Marlaw ndiye mshindani halisi wa Alikiba. Sio Diamond.

Sababu nimezieleza vizuri tu!
 
Kumshindanisha Diamond na mwanamziki yoyote Tanzania ni ujinga, si kwa waliopo au waliokuwepo. Bahati nzuri mi ni mtu wa zamani, najua wale wa zamani na wa sasa.
Ukiweka ushabiki pembeni, kuna wale wasiojua biashara ya muziki(showbiz) wanabaki kusema Diamond alikuwa zamani enzi za "nenda kamwambie" and the likes lakini hawajui dogo amebadilika kulingana na soko, internationally na local(kwa wale wa amsha amsha), muziki wa kuchezeka na ambao unaweza kumfurahisha hata asuyejua Kiswahili.
Kwa sisi tunaoishi na watu wasiojua Kiswahili hauwezi kumshawishi mtu asikilize nyimbo za kina Kiba/Marlaw ambazo wanaimba visauti kama wanaimba taarabu, hakuna mwenye uelewa wa kinachoimbwa na haiwezekani ukamshawishi apende nyimbo za aina hiyo.
Kuwashindasha Kiba na Marlaw inaweza kuwa sawa lakini kumtaja, I mean hata kumtaja tu Diamond katika wanamuziki wa level hizo ni makosa na ni kama kunakuwa na makusudi flani kwani ndiye mtu anayepaisha jina la Tz internationally katika sekta ya burudani.
Angalia fans hata maoni tu popote kwenye social media, angalia impact ya shows zake, angalia endorsements na matangazo na vyote hivi havikuja kwenye silver plate bali ni matunda ya mafanikio katika biashara ya burudani(kuimba vizuri, kujibranda vizuri, kumantain kwenye level ya juu kwa muda mrefu, kufanya kazi kwa bidii, kushikamana na timu yake bila ya majivuno kujiona yeye ndiyo kila kitu).
Hawa nyota wengine wa muziki(Bongo flavour) wangekuwa kiwango cha Diamond hata kufanya nao interview ingekuwa ni shida, kuwa humble pia kunambeba sana, kuushikilia ule Utandale kunamsaidia pia ndiyo diehard fans wake asilimia kubwa ni wale wa uswazi.
Wa kushindanishwa locally waendelee, nyota wanaopaisha jina la nchi kimataifa washindanishwe/walinganishwe na international artists.
 
Una mawazo mazuri lakini umeteleza kudhani muziki mzuri unatokana na lugha.

Wahindi wana nyimbo nzuri na zinatamba almost dunia nzima na watu hawaelewi hata wanachoimba. Wakongo na wale kina Despacito vile vile.

Hayo mengine ya kusema Diamond ni mkali kuliko wasanii wengine sio lengo la uzi huu.
 
Back
Top Bottom