Tunaokumbuka, tunakumbuka.
Muziki na ushindani wa kweli ulikuwa enzi za Alikiba na Marlaw kwa upande wa nyimbo za kuimbaimba. Ni miaka ya 2009 kurudi nyuma huko. Kabla ya Belle 9 na kina Ben Pol kutengenezwa kimkakati kisha kuja Diamond baadaye.
Alikiba na Marlaw walichuana kwenye ligi moja na kina Z-Anto, Matonya, MB Doggy, Sumalee, Pingu na Deso, 2 Berry, AT, PNC, Q-Jay, Makamua, Kassim Mganga, Joslin na wengine wengi.
Marlaw, kama wasanii wengine wengi, walidrop kuanzia 2010. Bahati mbaya wengi walihusisha kudrop kwake kimuziki na siasa za uchaguzi kwa kuwa yeye alikuwa msanii namba 1 kwa wakati ule. Tulitafakari vizuri hapa mwaka 2015 tukaona sio kweli. Mjadala huo upo hapa >
Je! Ni kweli Msanii Marlaw alipotezwa na Siasa?
Kwa sababu zozote zile, hazibadilishi ukweli kwamba Marlaw mpaka leo hii ni msanii anayependwa na kumissiwa zaidi na mashabiki kuliko msanii yeyote wa wakati wake. Huo ndio ukweli. Pita mitaani na mitandaoni halafu azungumziwe hata kwa bahati mbaya, maoni ya watu yatathibitisha.
Ni muda mrefu sasa tumekosa ladha ya mchuano wa vipaji halisi kwa sababu ya mambo mengi yaliyotokea kwenye industry ya muziki wa Bongo Fleva kwa miaka hii michache. Lakini shilingi si imeshageuka sasa? Kama Ally Kiba alipotea na kurudi, why not Marlaw?
Tumeona Ally Kiba tangu arudi amekuwa akipata ushindani usiofanana nae. Diamond sio muimbaji mzuri kama Ally Kiba. Japo ni the best kwenye anachokifanya. Marlaw ndiye muimbaji anayeweza kumchalenji zaidi Ally Kiba kwa sasa, kama ilivyokuwa zamani.
Nasisitiza, Marlaw ndio mtu sahihi wa kushindanishwa na Ally Kiba kimuziki. Aliyemshauri Marlaw kujipanga upya na kurudi kwenye game alifanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Kurudi kwake kutaanza kurudisha uhondo wa ushindani wa kweli wa muziki huu tulitotoka nao mbali.
Nimefurahi kuona Master Jay kupitia Marco Chali (MJ Records) nao wameshiriki kwenye movement hii ya kumtengenezea wimbo wake mpya aliochagua kurudi nao. Mpaka sasa wimbo unakimbia sana huko YouTube. Sijapata ripoti za kwenye redio na Bodaboda. Social media umeanza kuzunguka. Mpaka kuona mtu kama
Maxence Melo anaposti cover ya Marlaw, inaleta picha gani?
Marlaw - Taa (with lyrics)
Namshauri Ally Kiba asichukulie vibaya kurudi kwa ushindani huu kati yake na Marlaw. Wote wana nidhamu na sio watu wa show off na drama. Amuache Diamond apambane na wengine akiwemo Harmonize wake.
Team Diamond na WCB msinielewe vibaya!