Mpira muda mwingine haupo fair, pole Wilfred Ndidi

Mpira muda mwingine haupo fair, pole Wilfred Ndidi

Nabii kibonge

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2018
Posts
277
Reaction score
310
Maisha yanaenda kasi sana, juzi tu hapa tumetoka kumskia Wesley Sneidjer akisema anaamini kwamba angeweza kutajwa katika daraja moja na Cristiano Ronaldo pamoja na Lionel Messi kama angekuwa amejituma zaidi. Huyu apa “ Niwe mkweli na nikiri kwamba ningeweza kutajwa katika daraja moja na Ronaldo pamoja na Messi kama ningejituma kwa asilimia 100, najua hilo . Lakini sikutaka kufanya hivyo na sina majuto.Sio kwamba sikuwa na uwezo bali sikutaka tu “

Pengine inachekesha kidogo kama humjui Sneidjer, lakini tunaomjua sneidjer wa inter milan na timu ya taifa ya Uholanzi tunaona kuna kaukweli kidogo.

Achana na hayo 2016 may kulikuwa na shangwe sana katika mji wa leicester.Naam ni watoto wa King Richard III (1452-1485), nazungumzia mashabiki wa leicester city walipobeba ndoo ya EPL. kikosi chenye watu kama Ng'olo Kante, Riyad Mahrez pia striker Jarmie Vardy.

Mda kama huo club ya KRC Genk ya Ugelgiji walkuwa wanaanza kuona kwa mbaaali faida au matunda ya kijana wao wa academy toka mitaa ya Abuja mda huo akiwa na miaka 20 tu na baada ya miezi wababe wa kingpower wakamchukua kwa dau la paund milioni 17 huku wakiwa wanahaha kutafuta mrithi wa Ngolo Kante ambae wengi waliamini pengo lake haizibiki kamwe.

Miaka imesogea bwana na sasa misimu miwili baadae tuna Ngolo kante huku Chelsea na huku tuna Wilfred Ndidi Leicester, na utofauti ni mmoja tu huyu anaheshimika kweli kweli wachambuzi wakimwita world class midfielder na mwingine anaonekana ni mchezaji wa kawaida kama walivyo wachezaji wa timu ndogo za England.

Kikibwa kinachompa heshima kante ni ule ubingwa wa 2016.Kante ni jina kubwa sana kwenye viunga vya stamford pia utalisikia jina hilo kwenya midomo ya wachambuzi uchwara kina Steve Macmanaman kina Phil Nevile na Kina Jim Caragher.

Lakini ukienda kwenye dimba mambo ni tofauti kidogo utamwona mtoto wa Abuja akilimudu vyema dimba la kati, utamwona akiicheza kwa ufasaha mipira ya juu, utamwona akikokota mipira na kupiga pasi kwa ufasaha, utamwona akiclear mipira na pia utamwona akipiga tackles pale mambo yakienda kombo. Huku akiwa kinara wa tackles kwa viungo pale England.

1574775072038.png

Tofauti ni moja tu kante alicheza Leicester iliyopata mafanikio na Ndidi anacheza Leicester iliyoyumba kidogo na utofaut hauko kwenye perfomance kwa maana tuna vitu vingi vya kuangalia kila weekend ya EPL toka kwa Ndidi na chama lake la wana na sio tena Kante na viungo wenzie feki kina Jorginho.

1574775137197.png

Anachokifanya Ndidi ni kile anachofanya kante lakini ndidi anafanya kwa ufasaha zaidi kwa maana kwamba ni extra odinary, kante usitegemee lolote kwa mipira ya juu pia usijidanganye utamwone akipandisha mashambulizi kwa kukokota mipira kuifkisha kwa strikers.

Ndidi anafanya yote hayo akiwa na umri wa miaka 22 tu . 22 ndio usishangae. Mda kama huu kante alikuwa ufaransa ligi za madaraja ya chimi anacheza mpira viwanaja vinafanana na Nangwanda sijaona. Kante anamiaka 28 sasa umri ambao tunasema ni peak na usitegemee chochote kipya toka kwao kwa maana hamna cha ziada ataonyesha kwa maana umri unazidi mtupa mkono.

Ndidi anamiaka sita zaidi ya kucheza kufikia umri wa kante, Je atakuwaje akigikia umri huo kamuulize Wesley Sneidjer atakupa jibu.

Sneidjer tumemuelewa maneno yake kwa sababu ni Sneidjer ambae ofisi ya intermilan hazikosi kumbukizi yake kwa alichowafanyia. Ambae aliwafungashia virago Brazil 2010 chini ya usimamizi wa mchezaji wa zamani Captain Dunga .Sneidjer ambae aliongoza hukumu kali kwa mabingwa watetezi wa kombe la dunia naam ni spain.Lakini kauli hiyo hiyo akisema Kante nafkiri Giroud atatakiwa awe na ballon d o 3
 
Umeharibu kuita wezako hawajui kitu akati wewe hujui lolote.kante habari nyingine
 
Mkuu kuna kitu kimoja kwenye comparison yako hakipo sawa, unamcompare Ndidi na Kante wa sasa, Kante hajakuwa maarufu kwa perfomance ya 2019/20 bali amekuwa maarufu perfomance yake ya ubingwa.

Ni vyema data za Kante ziwe za msimu ule.
 
comparison ni based in general bado naamini ndidi ni bora kwa misimu yote japokuwa apo ni msimu mmoja tu
 
comparison ni based in general bado naamini ndidi ni bora kwa misimu yote japokuwa apo ni msimu mmoja tu
Mkuu sina muda ila ningekupa detailed comparison, Kuna vitu Ndidi yupo Vizuri kama Tackling (average 5 kwa 4.7 ya kante wa 2016 ila kuna vitu still bado anapitwa kama Interception Kante ni 4.3 vs 3.1 ya Ndidi. Huyu kante wa siku hizi ambae sometime anachezeshwa hadi pembeni si yule wa 2016.
 
mkuu interception kwa mda gan huo??pia hujaongelea kuhus passing pia aeril duels ndidi ana advantage kubwa kwa sababu ya height yake
 
Ndidi ana goal ngapi mwaka huu na kacheza match ngapi ukimlinganisha na Kante?
 
mkuu interception kwa mda gan huo??pia hujaongelea kuhus passing pia aeril duels ndidi ana advantage kubwa kwa sababu ya height yake
hizo ni avearge per match, hivyo zipo fair kwenye hio interception

kuhusu pasi kante wa leicester hakuwa mzuri sana kwenye pasi ila kante wa chelsea ni way better kushinda ndidi
hizi pass accuracy za ligi za kante kuanzia 2016 mpaka msimu huu

2015/16 ni 81.6%
2016/17 ni 88.8%
2017/18 ni 89.3%
2018/19 ni 87.9%
2019/20 ni 81.3%

ukija Ndidi yeye ni kama hivi
2016/17 ni 75.9%
2017/18 ni 76.1%
2018/19 ni 79.9%
2019/20 ni 84.2%

hivyo unaona kante by far ni mpigaji mzuri wa pasi,

na Aerials won by far ndidi ni mzuri misimu yote ana average zaidi ya moja na Kante hafikishi moja.
 
Mimi alipotumia neno "anaamini" nikaona nikae kimya kubishana na mtu juu ya "imani" ni kutafuta ugomvi usio na sababu.
Mkuu kuna kitu kimoja kwenye comparison yako hakipo sawa, unamcompare Ndidi na Kante wa sasa, Kante hajakuwa maarufu kwa perfomance ya 2019/20 bali amekuwa maarufu perfomance yake ya ubingwa.

Ni vyema data za Kante ziwe za msimu ule.
 
Kama unamwita Steve macmanaman mchambuzi uchwara wewe tukuitaje?.Pamoja na kwamba tunatizama mipira kwenye TV huyo dogo bado sana kufikia kiwango cha kante.
 
Kama unamwita Steve macmanaman mchambuzi uchwara wewe tukuitaje?.Pamoja na kwamba tunatizama mipira kwenye TV huyo dogo bado sana kufikia kiwango cha kante.
huo ndo ukwel waongeaji tu wale huwa wanaurahisisha sana mpira tumeona walivotutajia kikosi bora cha decade hamna lolote hadi bale yumo
 
hio ni pass accuracy tu ambayo basically kante anapiga acuracy kubwa ila anapiga back pases tu hazina impact yoyot 2018/2019 back pas 260+ pia ukija 2017/2018 kazpiga km 390+ hicho ni kigezo cha pass lakini bado vingi tu ndidi anamzidi kama tackling dribling na muhim san ni uwezo wa kcheza mipira ya juu hyo inampa nafas nzuri kumudu eneo la holding

Back
Top Bottom