Mpira wa TZ bado saana

Mpira wa TZ bado saana

Pole mkuu naona unajitahidi kueleza hisia zako juu ya ndala fc... Ule mpira yanga hawakupiga pasi nyingi kama simba. Wao walikuwa wanapiga mipira mirefu na kwakuwa haikufika kwa walengwa walionekana kama wanabutua tu usijipe upofu kisa ushabiki mkuu timu zote zilikuwa hovyo ila kusema yanga alimzidi simba pasi umedanganya kweupe
tupimane HISIA HAPA
takwimu%2Bsimba%2Bna%2Byanba%2Bfirst%2Bhalf.jpg
 
Natazama Simba na Yanga

wachezaji wanatoa pasi za upofu sana
yaaani mchezaji anapeleka pasi eneo ambalo hakuna mchezaji wa timu yake

kingine naona jinsi ya ku cover nafasi ni kama wachezaji wetu hawajui
mtu yuko nyuma ya mchezaji pinzani halafu anaomba pasi
na ajabu zaidi anapelekewa pasi pia...

mpira wetu baado saana

na Rafu nyingi tu za red card refa kazichunia
Afu unakuta wanajirundika tu pamoja. Yaani hadi najiuliza au viwanja vyetu vidogo ukilinganisha na vya Ulaya. Kwa kweli juzi nilikuwa disappointed sana na mpira wetu. Watu wanafukuza mpira badala ya kufungua nafasi. Wanataka wamulikwe na kamera.
Tusahau kabisa kuja kucheza kombe la dunia.
So brother you did very good observation.
 
Sasahivi mi nafatilia mpira wa bongo kujua matokeo tu, mpira hauvutii kabisa pia uko slow sana hauna kasi kama mipira ya wenzentu, pasi za chini hatuwezi, kutuliza mpira kwa mchezaji ni tatizo mwisho wa siku karedio flani kapo kumsema malinzi tu
 
Hilo halina ubishi mpira wetu ni hovyo kabisa binafsi bora niangalie ndondo mtaani kuliko kuangalia match za VPL kwenye TV.

Kingine ni afya za wachezaji wetu hawana athletic body Bali wamekonda hadi wanatia huruma. Huwa naona picha zao eti wanapata breakfast chai na vitumbua viwili, kwa mwendo huo hawawezi kuwa na miili ya ushindani kama hawatozingatia diet.
 
Natazama Simba na Yanga

wachezaji wanatoa pasi za upofu sana
yaaani mchezaji anapeleka pasi eneo ambalo hakuna mchezaji wa timu yake

kingine naona jinsi ya ku cover nafasi ni kama wachezaji wetu hawajui
mtu yuko nyuma ya mchezaji pinzani halafu anaomba pasi
na ajabu zaidi anapelekewa pasi pia...

mpira wetu baado saana

na Rafu nyingi tu za red card refa kazichunia
Mkuu.. Soka bado kwa mambo mengi sana hasa ukizingatia TFF nao wamo katika kudidimiza mpira, usimamizi wao kuhakikisha kila timu inakuwa na timu ya vijana ni butu

Lakini kwa mpira wa Simba na Yanga au hapa Tanzania Simba SC ndo timu inayocheza kandanda la ufundi na kufurahisha ila wakikutana na Yanga ile butuabutua yao inaharibu kabisa mipango ya Simba.
 
Ni wachache sana wataelewa huu Uzi..

Frankly speaking bongo mpira bado..

1.Poor ball possession
2.Poor dribbling
3. Poor pass accuracy


Kila kitu hovyo hovyo hovyo... Kibaya zaidi ni mashabiki wa team hizi kuaminishwa team zao ni bora.. Magazeti yanaandika timu hizi ni bora wakati kiuhalisia hakuna lolote uwanjani...


Ni Tanzania tu gazeti linaweza kuandika Barcelona haichezi vizuri lakini likaandika simba na yanga ziko vizuri.. Means waandishi wa habari wa nchi yetu ni rahisi kukosoa team za nje kushinda za ndani hususani simba na yanga, mwisho wa siku nikuzaa kizazi cha mashabiki vilaz.a kazi kushabikia kila kitu hata kama team inacheza hovyo
 
Natazama Simba na Yanga

wachezaji wanatoa pasi za upofu sana
yaaani mchezaji anapeleka pasi eneo ambalo hakuna mchezaji wa timu yake

kingine naona jinsi ya ku cover nafasi ni kama wachezaji wetu hawajui
mtu yuko nyuma ya mchezaji pinzani halafu anaomba pasi
na ajabu zaidi anapelekewa pasi pia...

mpira wetu baado saana

na Rafu nyingi tu za red card refa kazichunia
Unatuliza Moira kusini lakn linaenda mpka kaskzn
 
Unazungumzia mpira mbali kote uko wakati michezo kama kuogelea na riadha imetushinda wakat kuna wambulu na masai kibao na vijana kibao wanaoweza kuogelea.Kwaiyo tatizo letu sio kukosa vipaj bali akili zetu wenyewe ndo maana ukimsikiliza kashushu wakati anachambua mpira kwaumaridadi utakua na maswali mengi sana kuhusu soka letu.
 
ndio maana kunakua na ubao wa tathmini wakati wa mapumziko na baada ya mechi ambao pia una maana nyingi sana..............kama uliangalia tathmini ya kipindi cha kwanza waka hutobisha tena ila nakubaliana na wewe kwamba kiujumla timu zote zilikua hovyo
Nilichopinga mkuu nikuwa yanga walikuwa zaidi ya simba maana takwim za first half yanga alimzidi simba na kipindi cha pili simba alizidi yanga labda faulo nyingi ndo yanga aliongoza mwanzo mwisho [emoji2] [emoji2]
 
Mpira ni mwepesi ukiwa nje ya uwanja ingia Kati uone shuguli yke na hakuna kz nyepesi km kukosoa ata mtt mdgo anaweza kosoa....
na ufahamu wote tukicheza football itakuwa nonsense... hamna soccer bila shabiki
 
Sikutarajia tufikie Ulaya but kidogo hata Waafrica wenzetu
Ukitazama derby ya Al-Ahly na Zamalek....ni kiwango kikuubwa mno
sisi hata pasi tano tu shida
Mkuu bora kukubaliana na hali hii ilivo Watanzania kila sector hatuwezi kufanya la maana. Tuko nyuma kila mahali
 
Back
Top Bottom