DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Msanii maarufu wa vichekesho, Mpoki, ameilaumu Jeshi la Polisi akishangazwa na kutokamatwa kwa watuhumiwa wa mauaji ya MC Pilipili hadi sasa. Akihoji kwa masikitiko, alisema:
"Wakati nasikiliza ile ripoti nilitegemea kwamba tunapomzika leo, tayari watuhumiwa wangekuwa rumande. Siingilii kazi ya Jeshi la Polisi, lakini anzeni kwa kumchunguza yule aliyepigiwa simu na MC Pilipili kabla ya tukio." Msanii Mpoki
Aidha, akizungumzia upande wa uongozi, Mpoki alisema kuwa kuna kipindi MC Pilipili alikumbana na changamoto lakini baadhi ya viongozi walionekana kukaa mbali badala ya kumsaidia. Aliongeza kuwa:
"Baadhi ya viongozi, wakati wasanii wanawapigia simu, pokeeni simu zao. Msiache kupokea. Tunawasaidia mpaka mnapokaa kwenye hivyo viti.". Msanii Mpoki
Pia Soma: Polisi: MC Pilipili alifariki dunia kwa kipigo. Mwili ulikuwa na majeraha