Mpya: Askari polisi wa kituo cha Mbalizi Mbeya wafanya Ibada kituoni kuomba Mungu atuepushie janga la Corona

Nivema kama hayo maombi waliyofanya yanaakisi matendo yao katika kutimiza wajibu wao
 

Mkuu jitahidi kutenganisha ibada za Mungu na huu uhuni+ ujinga unaoendelea hivi sasa. Ndio maana wakati wa ule utapeli wa kikombe cha babu watu wenye elimu na heshima zao walienda, na watu wengi waliishia kupoteza ndugu zao. Hiki kinachoendelea sasa hivi ni kuonyesha jinsi gani watu ni wajinga kwa kichaka cha imani.
 
Umeongea kwa hisia sana mkuu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yesu alisema......." Mkutanikapo watu wawili au zaidi kwa jina langu mimi nipo katikati yenu"

Ile Ibada ilikuwa halisi, Mungu wa mbinguni ambariki afande Lusekelo na vijana wake!

Ile sio ibada, bali ni uhuni wa ibada ndani ya kituo cha polisi.
 
Jeshi la polisi halina dini lakini nashangaa wanageuza kituo cha polisi kuwa kanisa nina uhakika ingekuwa waislamu ndio wamefanya hayo kelele zingekuwa nyingi sana, waache upuuzi siku nyingine wakitaka kumuomba huyo wanayemuita Yesu waende kanisani
Unauhakika gani mkuu kama kulikuwa na sehemu mbili za maombi chombo cha habari kikaonesha sehemu moja tu kutokana na ufinyu wa muda..
 
Ataacha kucheka wakati anajua kabisa ni futuhi kama la kina Masanja? Maana polisi sio nyumba ya ibada, na serikali haina dini, ilikuwaje mpaka camera zikaletwa kwenye huo uhuni?
Mkuu wa Wilaya bhana...natamani siku moja muongozwe na watu wenye akili sana
 
1.Kwa mtu yoyote aliyetambua tatizo hili lipo na ni kubwa yupo katika nafasi ya kujiandaa kujilinda

2. Kuna baadhi yetu hatujajua kabisa kinachoendelea na kufanya kama ni kamchezo kwenye kuvaa barakoa na kuqamini ni ka fashion kamekuja tu

3.Kuna wanaoulizia ni wangapi leo bila kujua kesho yeye anaweza kuwa ni mmoja wa hao wangapi wanauuliziwa ama ndugu yake ama rafiki yake waliokutana naye hivi karibuni.

4. Hawa makamanda wameshaliona tatizo mpaka kuamua kufanya ibada kituoni jambo ambalo sii la kawaida.

5. Hawa kama walivyo wahudumu wa afya wapo katika risk na wakati mgumu sana kwenye janga hili kwani tumeona duniani kote nao wakiwa mstari wa mbele katika kuokoa na kuhudumia

6. Tuungane nao katika maombi na kusaidiana kwa hali na mali katika elimu, vifaa tiba na vifaa jikinga katika jmii yooote

7. Tuchukue taadhari zote za wataalamu wa afya tusidharau wala kukebehi # TANZANIA BILA CORONA INAWEZEKANA#
Urbi et Orbi
 
Duh!...anawacheka wenzake?
Maombi yameingia Kwenye siasa hapo hakuna la maana zaidi ya kupiga kelele mbele za MUNGU
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mie mwenyewe ningecheka kwanguvu
Wakokole ukiumwa kichwa wanaanza kukemea mapepo utasukumwa bichwa had utie adabu...ndo km hao
Ataacha kucheka wakati anajua kabisa ni futuhi kama la kina Masanja? Maana polisi sio nyumba ya ibada, na serikali haina dini, ilikuwaje mpaka camera zikaletwa kwenye huo uhuni?
Wapi pictures please...

Sent using Jamii Forums mobile app
Hadi kufikia kesho asubuhi kavideo ka hio ibada hakajapandishwa hapa basi utakuwa umbeya tu
habari bila picha hainogi
Wewe umeona wapi picha,wengine twaingoja kwanza tena usiwe Photoshop.

Sent using Jamii Forums mobile app
Subiri taarifa ya habari ya saa usiku kituo cha ITV ili ujionee huo uhuni.
ANZIA DK YA 6


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahabusu walitakiwa kupigwa chips kuku katika siku tatu hizi za maombi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…