Mr. Blue na Baki na Mimi

Fid anajua sana, tatizo hajui kufreestyle...ndo maana nimeamua kumkubali MBISHI badala ya fid.
mkuu hata Pac free style amna kitu....Jay Z ndio kabisa sifuri na hao pia huwakubali?!
 
blue ni mkali ila Baki na Mimi amna kitu...ni wimbo wa kawaida mno
 
Nampenda Mr. Blue,
Msanii pekee asiyechuja,
Msanii anayewika bila dili la matangazo,
Hana rafiki Paparazi ili jina lake liwe juu.

Kiufupi Blue hata aimbe Mabata madogo madogo me nitapenda na nitaimba nae.
...wapigie wazazi wako wambie uko na mimi! .....
 
blue ni habari nyengne namkubali kweli, kwa namkubali kwa ile stail ya kipekee namkubali sana
 
Blue ni kati ya wasanii tallented kupata kutokea kwenye game ya bongofleva, anauwezo mkubwa wa kurap na kuimba, huyu ni jamii za kina Ngwea. Furaha tele,....tele, wambie wakina... Leo siku ya vigelegele...
Mr umemaliza. Uko sahihi kabisa. Bongofleva wengi ni ama kuimba tu au Kuchana tu lakini Blue kama alivyokuwa Ngwea (R.I.P) anakupa vyote. Iwe ngoma za kibishoo au za kisela kama za BoB micharazo zote anaweza. Yuko vizuri.
 
Blue ni mfano wa wasanii wachache walioweza kulinda heshima yao kwenye game tangu wanatoka hadi leo, tofauti na wale waliovuma na kushindwa kurudi kushika namba.

Aina ya wasanii walioweza kukamata kitambo na mpaka leo wakishindana na watoto wa sasa ni:

Blue

Fid q

Professor j

Nyandu toz

Joh makin

Kiba

Diamond

Hao ni mfano tu ila wapo wengi waliotamba kwa nyakati zao ila mpaka leo wapo kwenye chati.

Afande Sele aliwahi kuulizwa kuwa kwa nini Blue na Diamond wanajiita simba wakati yeye ndiye anaetambulika kama simba zee, akajibu......wanastahili kujiita hivyo kwa kuwa simba ni mpambanaji na wao wamepambana na kupendwa tangu nyimbo zao za mwanzo mpaka leo wanakamata soko
 
Ni kweli matusi sikatai angeimba mwingine isingesikika sababu Blue ana swagger zake zilizopelekea nyimbo ibambe...
Ana style za kipeke yake sana. Namkumbuka huyu dogo tangu anaimba freestyle hana hata singo 1.ali washaghairi moto siku moja pale vijana club sio mango balaa. Kulikua na mashindano ya rap.
Ilikua 1999-2000 hivi
 
Inasemekana Blue alikuwa inspired kufanya mziki na kaka zake wakubwa. Cha ajabu hao wakubwa zake sijawahi kuwaona wala kuwaskia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…