Mr Blue ndio Nyani Mzee kwenye tsnia ya muziki bongo

Dr.adams faida

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
1,888
Reaction score
3,352
Khery Sameer Rajab a.k.a MR BLUE au KABAYSER ni moja wa Wanamuziki bora kabisa wa muda wote katika Muziki wa kizazi kipya.

Tumeshuhudia Wasanii wengi wanaingia kwenye Game na kupotea lakini yeye yupo vilevile...kila nyimbo anayotoa ni Hit! Kuanzia Blue blue..Mapozi..Tabasamu na mpaka leo Mboga saba!....this is one of the Best Talent ever!..anaimba, ana-rap, ..style yake ni kuchana taratiibu wala hana haraka...ni kama anapaka siagi kwenye mkate.

Blue ali-inspire vijana wengi wadogo kufanya muziki,na wengi wanaoimba leo wamemkuta kwenye game,..Always Blue yupo peace na hana ugomvi wala bifu na mtu, na hata hivi karibunj baada ya kusikia Diamond anatumia nick name yake ya "Simba"...Blue ameamua kumuachia jina hilo na sasa anajiita "Nyani Mzee" akimaanisha Ukongwe wake katika game.

Na ipo wazi sana kwamba blue ni mmoja wa wasanii bora kabisa ktk Collaboration..yeye pamoja na Komando Lady jay dee ni wasanii ambao wana historia ya kushirikishwa na kumpoteza mwenye Nyimbo...Moja ya nyimbo ambayo Blue alizua Gumzo ni "NILIKATAA" ambayo baada ya TID na Q Chillah kuimba ktk Beti ya kwanza na ya pili..Blue alikuja na Rhymes zake kwenye beti ya tatu na kufunika kabisa hao wakali wa Masauti kisha akapotelea zake Tabata.

Na kali kuliko zote ni Walipokutana Wakali wa kupoteza wenzao kwenye Collabo, yaani Lady jay dee Ft Mr Blue katika nyimbo "Wangu"....hapa Dada Yetu Commando alikiri kwamba ile Verse ya Mwisho Blue alifunika.

ikumbukwe Kabayser ndio kwanza ana miaka 29 tu na tayari ni legend wa muziki huu na still ana Muda mrefu wa kuwepo kwenye game kama hatojichanganya na akizingatia weledi na nidhamu ya game...inshaAllah Mungu amjaalie uzima na familia yake.

Nami nichukue fursa hii kujisikia Faraja kumuandika Mkongwe huyu ningali bado hai na kalamu yangu...na yeye angali bado hai anaimba,..With a degree of Appreciation....Thanks.

[HASHTAG]#Pio[/HASHTAG] pius
 
Blue ni Legendary.

Wasanii wale aliokuwa anatamba nao miaka ile wote wamepotea wengine kila wakitoa ngoma boko ila blue bado yupo kwenye ubora ule ule.

Roho Zinawauma ndio wimbo Mkali zaidi kutoka Kwake kwa upande wangu.
Huyu bwana huwa hakosei kiukweli.
 
Dunia hii watu kama wewe lazima muwepo mkuu, ila kiufupi jamaa namkubali tu kwa kazi zake nasivingenevyo.
Kumkubali mkubali tu, haukatazwi! Lakini usiudanganye umma kuhusu Blue!
 
Well said mkuu.
Huyu ni young Legend hasa..
[HASHTAG]#GoodmusicTz[/HASHTAG]
 
Blue ni Legendary.

Wasanii wale aliokuwa anatamba nao miaka ile wote wamepotea wengine kila wakitoa ngoma boko ila blue bado yupo kwenye ubora ule ule.

Roho Zinawauma ndio wimbo Mkali zaidi kutoka Kwake kwa upande wangu.
Mimi mapozi..
Sema ana roho nzuri wimbo nitakufa na wewe ulivyokuwa mkali vile bado akampa ab skills
 
Blue ni Legendary.

Wasanii wale aliokuwa anatamba nao miaka ile wote wamepotea wengine kila wakitoa ngoma boko ila blue bado yupo kwenye ubora ule ule.

Roho Zinawauma ndio wimbo Mkali zaidi kutoka Kwake kwa upande wangu.
Tabasamu is my best
 
Kumbe msukule wa tabata ukiweka pembeni ubashite unaweza kuandika point
 
Blue ni legend, I agree kwamba ni one of the best talents ambazo tumewahi kuwa nazo kwenye bongofleva, namuheshimu sana mtu aliye perfect kwenye both kuimba na kuchana. Na ni wachache sana wanaoweza kumaintain kufanya hivyo kwa zaidi ya miaka 10
 
Upo sawa mkuu jamaa mpaka leo akipanda stejini show zake watu huzikubali anajua njisi gani acheze na mashabiki.
 
Nikosoe wapi nimedanganya weka ukweli wako hapa mkuu wala sio ugomvi.
Ili umpate Blue, inabidi utaje malegendary 10, ukitaja wa5 Blue hatii sio pua tu, hata kamasi! Ona hawa hapa:
1. Joseph Mbilinyi
2. Fareed Kubanda.
3. Joseph Haule.
4. Juma Mchopanga.
5. Albert Mangair.
Kama hutaki sikulazimishi, kaa na ubishi wako!
 
Nafikiri kinachosababisha Blue aonekane legendary ni kwa sababu alianza muziki akiwa kinda huku mashabiki wanaomshabikia wakiwa makinda pia.

Maana yangu ni kua Blue amekua umri sawa na mashabiki zake, yaani tangu anatoa blue blue mpaka leo ni mashabiki wake wale wa umri wake.

Nature kibla, Prof j, Mandojo Na Domokaya n.k walikua na mashabiki wengi sana lakini mashabiki hao umri ushawatupa mkono hawawezi tena kuingia jf na kukumbusha kua Lil Kim alipofanya Show Tz ilibidi amtaje Nature kila muda ili mashabiki wasiondoke.
Au Mandojo na Domokaya na Nature walivyoifanya single ya Niaje, wimbo ambao kila mstari uliishia na herufi 'i'

Hivyo hili kundi la Blue, litakwenda na maji kisha watakuja mashabiki wa Youg Killer ambao miaka 7 mbele na wenyewe wataandika kama kilichoandikwa hapa.
 
Blue ndio nani nchi hii mimi nawajua leka tutigite pekee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…