mjukuum
JF-Expert Member
- Dec 8, 2014
- 5,258
- 2,842
Tid na qchifu walijuta kumshilikisha kwenye ile songiKhery Sameer Rajab a.k.a MR BLUE au KABAYSER ni moja wa Wanamuziki bora kabisa wa muda wote katika Muziki wa kizazi kipya.
Tumeshuhudia Wasanii wengi wanaingia kwenye Game na kupotea lakini yeye yupo vilevile...kila nyimbo anayotoa ni Hit! Kuanzia Blue blue..Mapozi..Tabasamu na mpaka leo Mboga saba!....this is one of the Best Talent ever!..anaimba, ana-rap, ..style yake ni kuchana taratiibu wala hana haraka...ni kama anapaka siagi kwenye mkate.
Blue ali-inspire vijana wengi wadogo kufanya muziki,na wengi wanaoimba leo wamemkuta kwenye game,..Always Blue yupo peace na hana ugomvi wala bifu na mtu, na hata hivi karibunj baada ya kusikia Diamond anatumia nick name yake ya "Simba"...Blue ameamua kumuachia jina hilo na sasa anajiita "Nyani Mzee" akimaanisha Ukongwe wake katika game.
Na ipo wazi sana kwamba blue ni mmoja wa wasanii bora kabisa ktk Collaboration..yeye pamoja na Komando Lady jay dee ni wasanii ambao wana historia ya kushirikishwa na kumpoteza mwenye Nyimbo...Moja ya nyimbo ambayo Blue alizua Gumzo ni "NILIKATAA" ambayo baada ya TID na Q Chillah kuimba ktk Beti ya kwanza na ya pili..Blue alikuja na Rhymes zake kwenye beti ya tatu na kufunika kabisa hao wakali wa Masauti kisha akapotelea zake Tabata.
Na kali kuliko zote ni Walipokutana Wakali wa kupoteza wenzao kwenye Collabo, yaani Lady jay dee Ft Mr Blue katika nyimbo "Wangu"....hapa Dada Yetu Commando alikiri kwamba ile Verse ya Mwisho Blue alifunika.
ikumbukwe Kabayser ndio kwanza ana miaka 29 tu na tayari ni legend wa muziki huu na still ana Muda mrefu wa kuwepo kwenye game kama hatojichanganya na akizingatia weledi na nidhamu ya game...inshaAllah Mungu amjaalie uzima na familia yake.
Nami nichukue fursa hii kujisikia Faraja kumuandika Mkongwe huyu ningali bado hai na kalamu yangu...na yeye angali bado hai anaimba,..With a degree of Appreciation....Thanks.
[HASHTAG]#Pio[/HASHTAG] pius
Kumbuka pia ile ya dully na josilin kariakoo aliwavuniki ikasemekana dully alitumia utundu kuongeza vase ya nne namjubali mno huyu kijana