Mr Blue ndio Nyani Mzee kwenye tsnia ya muziki bongo

Mr Blue ndio Nyani Mzee kwenye tsnia ya muziki bongo

Khery Sameer Rajab a.k.a MR BLUE au KABAYSER ni moja wa Wanamuziki bora kabisa wa muda wote katika Muziki wa kizazi kipya.

Tumeshuhudia Wasanii wengi wanaingia kwenye Game na kupotea lakini yeye yupo vilevile...kila nyimbo anayotoa ni Hit! Kuanzia Blue blue..Mapozi..Tabasamu na mpaka leo Mboga saba!....this is one of the Best Talent ever!..anaimba, ana-rap, ..style yake ni kuchana taratiibu wala hana haraka...ni kama anapaka siagi kwenye mkate.

Blue ali-inspire vijana wengi wadogo kufanya muziki,na wengi wanaoimba leo wamemkuta kwenye game,..Always Blue yupo peace na hana ugomvi wala bifu na mtu, na hata hivi karibunj baada ya kusikia Diamond anatumia nick name yake ya "Simba"...Blue ameamua kumuachia jina hilo na sasa anajiita "Nyani Mzee" akimaanisha Ukongwe wake katika game.

Na ipo wazi sana kwamba blue ni mmoja wa wasanii bora kabisa ktk Collaboration..yeye pamoja na Komando Lady jay dee ni wasanii ambao wana historia ya kushirikishwa na kumpoteza mwenye Nyimbo...Moja ya nyimbo ambayo Blue alizua Gumzo ni "NILIKATAA" ambayo baada ya TID na Q Chillah kuimba ktk Beti ya kwanza na ya pili..Blue alikuja na Rhymes zake kwenye beti ya tatu na kufunika kabisa hao wakali wa Masauti kisha akapotelea zake Tabata.

Na kali kuliko zote ni Walipokutana Wakali wa kupoteza wenzao kwenye Collabo, yaani Lady jay dee Ft Mr Blue katika nyimbo "Wangu"....hapa Dada Yetu Commando alikiri kwamba ile Verse ya Mwisho Blue alifunika.

ikumbukwe Kabayser ndio kwanza ana miaka 29 tu na tayari ni legend wa muziki huu na still ana Muda mrefu wa kuwepo kwenye game kama hatojichanganya na akizingatia weledi na nidhamu ya game...inshaAllah Mungu amjaalie uzima na familia yake.

Nami nichukue fursa hii kujisikia Faraja kumuandika Mkongwe huyu ningali bado hai na kalamu yangu...na yeye angali bado hai anaimba,..With a degree of Appreciation....Thanks.

[HASHTAG]#Pio[/HASHTAG] pius
Tid na qchifu walijuta kumshilikisha kwenye ile songi

Kumbuka pia ile ya dully na josilin kariakoo aliwavuniki ikasemekana dully alitumia utundu kuongeza vase ya nne namjubali mno huyu kijana
 
Attachments

  • Screenshot_20170219-003828.png
    Screenshot_20170219-003828.png
    20.3 KB · Views: 30
Ili umpate Blue, inabidi utaje malegendary 10, ukitaja wa5 Blue hatii sio pua tu, hata kamasi! Ona hawa hapa:
1. Joseph Mbilinyi
2. Fareed Kubanda.
3. Joseph Haule.
4. Juma Mchopanga.
5. Albert Mangair.
Kama hutaki sikulazimishi, kaa na ubishi wako!
Mkuu hilo sibishi sasa wewe unakurupuka tu unakuja kuovertake thread mimi nimemzungumzia blue sasa hao uliowataja wamo kwenye uzi huu ingependeza ungesema achilia mbali blue kuna hawa ndo ukataja hiyo orodha yako hayupo anayekupinga upo sawa mkuu.
 
Imenibidi nimutumie Msanii Nikki mbishi katika moja ya mistari yake anasema-
"Usisubiri Mpaka nife ndio unisifu uandike Wasifu,nizikwe nisahaulike zipite siku"

Hiki ulichofanya "Dr.adms" ni kitu safi sana, Sifa inapendeza mtu akiwa hai.
Binadamu watukupa sifa ambazo unasitahili ukiwa kaburini.

Mr.blue yupo vyema sana kadumu katika ngumu hili sio jambo la kubeza hata kidogo.

-Heshima kwake!
 
Mkuu hilo sibishi sasa wewe unakurupuka tu unakuja kuovertake thread mimi nimemzungumzia blue sasa hao uliowataja wamo kwenye uzi huu ingependeza ungesema achilia mbali blue kuna hawa ndo ukataja hiyo orodha yako hayupo anayekupinga upo sawa mkuu.
Sawa Mr. Blue. Wee mkali.
 
Ili umpate Blue, inabidi utaje malegendary 10, ukitaja wa5 Blue hatii sio pua tu, hata kamasi! Ona hawa hapa:
1. Joseph Mbilinyi
2. Fareed Kubanda.
3. Joseph Haule.
4. Juma Mchopanga.
5. Albert Mangair.
Kama hutaki sikulazimishi, kaa na ubishi wako!
Kula likes kumi
 
Nafikiri kinachosababisha Blue aonekane legendary ni kwa sababu alianza muziki akiwa kinda huku mashabiki wanaomshabikia wakiwa makinda pia.

Maana yangu ni kua Blue amekua umri sawa na mashabiki zake, yaani tangu anatoa blue blue mpaka leo ni mashabiki wake wale wa umri wake.

Nature kibla, Prof j, Mandojo Na Domokaya n.k walikua na mashabiki wengi sana lakini mashabiki hao umri ushawatupa mkono hawawezi tena kuingia jf na kukumbusha kua Lil Kim alipofanya Show Tz ilibidi amtaje Nature kila muda ili mashabiki wasiondoke.
Au Mandojo na Domokaya na Nature walivyoifanya single ya Niaje, wimbo ambao kila mstari uliishia na herufi 'i'

Hivyo hili kundi la Blue, litakwenda na maji kisha watakuja mashabiki wa Youg Killer ambao miaka 7 mbele na wenyewe wataandika kama kilichoandikwa hapa.
Mandojo na domokaya hawa watu nawakubali mno!

Hasa nikiusikilza wimbo wa "Dingi" .
 
Ili umpate Blue, inabidi utaje malegendary 10, ukitaja wa5 Blue hatii sio pua tu, hata kamasi! Ona hawa hapa:
1. Joseph Mbilinyi
2. Fareed Kubanda.
3. Joseph Haule.
4. Juma Mchopanga.
5. Albert Mangair.
Kama hutaki sikulazimishi, kaa na ubishi wako!
toa mmoja weka necha kwny top 5
 
i like nyimbo yake inaitwa "nipo nilikuwepo na nitakuwepo " ni bonge la song
 
Nafikiri kinachosababisha Blue aonekane legendary ni kwa sababu alianza muziki akiwa kinda huku mashabiki wanaomshabikia wakiwa makinda pia.

Maana yangu ni kua Blue amekua umri sawa na mashabiki zake, yaani tangu anatoa blue blue mpaka leo ni mashabiki wake wale wa umri wake.

Nature kibla, Prof j, Mandojo Na Domokaya n.k walikua na mashabiki wengi sana lakini mashabiki hao umri ushawatupa mkono hawawezi tena kuingia jf na kukumbusha kua Lil Kim alipofanya Show Tz ilibidi amtaje Nature kila muda ili mashabiki wasiondoke.
Au Mandojo na Domokaya na Nature walivyoifanya single ya Niaje, wimbo ambao kila mstari uliishia na herufi 'i'

Hivyo hili kundi la Blue, litakwenda na maji kisha watakuja mashabiki wa Youg Killer ambao miaka 7 mbele na wenyewe wataandika kama kilichoandikwa hapa.
Ahsante sana. Umenijuza tofauti yangu na mtoa mada.

Ngoja nikupe mfano. Wakati SUGU anahit, anakuja kutuimbia shule za Moro town back in mid 1990s pale Forest Hill, Kigurunyembe, Moro Sec, n.k Sijui Blue alikuwa wapi!

SUGU anapanda jukwaani, MANGO GARDEN, analipwa, mtoto wa kitaa AFANDE SELE, anapewa MIC na SUGU anaimba bure ili tu atoke!

AFANDE anaandika, anaimba anatuskilizisha ngoma huku tukimpamba, hatimaye SUGU anambeba ktk ngoma MIKONONI MWA POLISI, Afande anarudi Morogoro anasimulia mtaa mzima!

Nilikuwa DSM wakati Prof Jay anaazima koti la Jeshi la mchizi wake RAMADHANI baharia wa CAPE TOWN, akapande nalo stejini wakati albam ya kwanza hata haijakamilika, RAMADHANI anatukusanya madogo wa kitaa tukamshangilie prof jizze, Blue sijui alikuwa wapi!

Nikiwa kidato cha 5, Fa alikuwa kidato cha 6 PCM. wakati Fa anaruka fence usiku kwenda makumbusho kupiga tizz na akina Juma Mchopanga, anakuja kutoka na INGEKUWA VP, Blue simjui!

Kwa umri wangu ukintajia Malegendary nitakuelewa ukitaja kizazi hiki! Lakini hawa watoto wa Mulugo wapo sahihi kumtaja Blue kama legendary wao!
 
Ili umpate Blue, inabidi utaje malegendary 10, ukitaja wa5 Blue hatii sio pua tu, hata kamasi! Ona hawa hapa:
1. Joseph Mbilinyi
2. Fareed Kubanda.
3. Joseph Haule.
4. Juma Mchopanga.
5. Albert Mangair.
Kama hutaki sikulazimishi, kaa na ubishi wako!
Acha wivu mkuu..mkubali mtu kwa kazi yake,jamaa kasema ni mtu ambaye mpaka leo akitoa ngoma bado blue anakubalika tofaut na hao uliowataja wew..ata ukienda kwenye show blue anakubalika kwa sasa kuliko hao..hao uliowataja kweli ni malegendary wa music ila ni blue ni legendary mpaka leo mm mwenywe namkubali kazi zake hajachuja kama hao uliowataja
 
Mr Blue si nimeshakukubali Mkuu. Watu wa hipo hop hatuna roho hizo jamaa!
 
Huo moto si mchezo yaani zile vesi zilikua zinatiririka hadi unasahau kama hizi ni tatu ndani ya moja.
Mpaka Sasa huo wimbo huwa sichoki kuusikiliza,
Wasanii wa kipindi cha nyuma walikuwa wanaandika nyimbo nzuri sana na zenye Jumbe zilizo shiba sana.
 
Back
Top Bottom