Mr Blue ndio Nyani Mzee kwenye tsnia ya muziki bongo

Mr Blue ndio Nyani Mzee kwenye tsnia ya muziki bongo

Ahsante sana. Umenijuza tofauti yangu na mtoa mada.

Ngoja nikupe mfano. Wakati SUGU anahit, anakuja kutuimbia shule za Moro town back in mid 1990s pale Forest Hill, Kigurunyembe, Moro Sec, n.k Sijui Blue alikuwa wapi!...
Hahahaha mkuu hapa sasa kingojewe kizazi cha Young Killah...kije kusema jamaa ni Legendary.
 
Khery Sameer Rajab a.k.a MR BLUE au KABAYSER ni moja wa Wanamuziki bora kabisa wa muda wote katika Muziki wa kizazi kipya.

Tumeshuhudia Wasanii wengi wanaingia kwenye Game na kupotea lakini yeye yupo vilevile...kila nyimbo anayotoa ni Hit! Kuanzia Blue blue..Mapozi..Tabasamu na mpaka leo Mboga saba!....this is one of the Best Talent ever!..anaimba, ana-rap, ..style yake ni kuchana taratiibu wala hana haraka...ni kama anapaka siagi kwenye mkate.

Blue ali-inspire vijana wengi wadogo kufanya muziki,na wengi wanaoimba leo wamemkuta kwenye game,..Always Blue yupo peace na hana ugomvi wala bifu na mtu, na hata hivi karibunj baada ya kusikia Diamond anatumia nick name yake ya "Simba"...Blue ameamua kumuachia jina hilo na sasa anajiita "Nyani Mzee" akimaanisha Ukongwe wake katika game.

Na ipo wazi sana kwamba blue ni mmoja wa wasanii bora kabisa ktk Collaboration..yeye pamoja na Komando Lady jay dee ni wasanii ambao wana historia ya kushirikishwa na kumpoteza mwenye Nyimbo...Moja ya nyimbo ambayo Blue alizua Gumzo ni "NILIKATAA" ambayo baada ya TID na Q Chillah kuimba ktk Beti ya kwanza na ya pili..Blue alikuja na Rhymes zake kwenye beti ya tatu na kufunika kabisa hao wakali wa Masauti kisha akapotelea zake Tabata.

Na kali kuliko zote ni Walipokutana Wakali wa kupoteza wenzao kwenye Collabo, yaani Lady jay dee Ft Mr Blue katika nyimbo "Wangu"....hapa Dada Yetu Commando alikiri kwamba ile Verse ya Mwisho Blue alifunika.

ikumbukwe Kabayser ndio kwanza ana miaka 29 tu na tayari ni legend wa muziki huu na still ana Muda mrefu wa kuwepo kwenye game kama hatojichanganya na akizingatia weledi na nidhamu ya game...inshaAllah Mungu amjaalie uzima na familia yake.

Nami nichukue fursa hii kujisikia Faraja kumuandika Mkongwe huyu ningali bado hai na kalamu yangu...na yeye angali bado hai anaimba,..With a degree of Appreciation....Thanks.

[HASHTAG]#Pio[/HASHTAG] pius
Mkuu kiboko wa yote ni dully sykes yeye ndo hachuji kabisa yani
 
Imenibidi nimutumie Msanii Nikki mbishi katika moja ya mistari yake anasema-
"Usisubiri Mpaka nife ndio unisifu uandike Wasifu,nizikwe nisahaulike zipite siku"

Hiki ulichofanya "Dr.adms" ni kitu safi sana, Sifa inapendeza mtu akiwa hai.
Binadamu watukupa sifa ambazo unasitahili ukiwa kaburini.

Mr.blue yupo vyema sana kadumu katika ngumu hili sio jambo la kubeza hata kidogo.

-Heshima kwake!
Kwel mkuu jamaa amejitahidi kukomaa kwenye game.
 
Ahsante sana. Umenijuza tofauti yangu na mtoa mada.

Ngoja nikupe mfano. Wakati SUGU anahit, anakuja kutuimbia shule za Moro town back in mid 1990s pale Forest Hill, Kigurunyembe, Moro Sec, n.k Sijui Blue alikuwa wapi!

SUGU anapanda jukwaani, MANGO GARDEN, analipwa, mtoto wa kitaa AFANDE SELE, anapewa MIC na SUGU anaimba bure ili tu atoke!

AFANDE anaandika, anaimba anatuskilizisha ngoma huku tukimpamba, hatimaye SUGU anambeba ktk ngoma MIKONONI MWA POLISI, Afande anarudi Morogoro anasimulia mtaa mzima!

Nilikuwa DSM wakati Prof Jay anaazima koti la Jeshi la mchizi wake RAMADHANI baharia wa CAPE TOWN, akapande nalo stejini wakati albam ya kwanza hata haijakamilika, RAMADHANI anatukusanya madogo wa kitaa tukamshangilie prof jizze, Blue sijui alikuwa wapi!

Nikiwa kidato cha 5, Fa alikuwa kidato cha 6 PCM. wakati Fa anaruka fence usiku kwenda makumbusho kupiga tizz na akina Juma Mchopanga, anakuja kutoka na INGEKUWA VP, Blue simjui!

Kwa umri wangu ukintajia Malegendary nitakuelewa ukitaja kizazi hiki! Lakini hawa watoto wa Mulugo wapo sahihi kumtaja Blue kama legendary wao!
Totally wrong;
Malegendary bongo fleva wapo wengi sana, kwa hiyo kumuita Blue legend haimaanishi hao wengine sio malegend. Kila mmoja amefanya kazi nzuri kwa wakati wake na ndo maana leo Cr7 ni legend pale Madrid lkn hiyo haimaanishi Raul au R9 au Zidane sio malegend au useme watoto wa siku hizi wanamuona Robben Legend tu kwa sababu hawakuwahi kuwaona akina Bergkamp na Kluvert.
Mtazamo wako bro hauko sawa kabisa, Blue atabaki kuwa legend na hao kina Nature, Sugu, Afande nao pia ni Malegend, kila mmoja ana yake ya kujivunia.
By the way ukiacha story zako za kitaani sijui Profesa kaomba gwanda za jeshi,sijui afande akapewa lift na sugu, nyimbo zao zilizowatoa nilikuwepo na nilizisikia lakini bado naamini Blue ni moja ya malegend bongo fleva
 
Ahsante sana. Umenijuza tofauti yangu na mtoa mada.

Ngoja nikupe mfano. Wakati SUGU anahit, anakuja kutuimbia shule za Moro town back in mid 1990s pale Forest Hill, Kigurunyembe, Moro Sec, n.k Sijui Blue alikuwa wapi!

SUGU anapanda jukwaani, MANGO GARDEN, analipwa, mtoto wa kitaa AFANDE SELE, anapewa MIC na SUGU anaimba bure ili tu atoke!

AFANDE anaandika, anaimba anatuskilizisha ngoma huku tukimpamba, hatimaye SUGU anambeba ktk ngoma MIKONONI MWA POLISI, Afande anarudi Morogoro anasimulia mtaa mzima!

Nilikuwa DSM wakati Prof Jay anaazima koti la Jeshi la mchizi wake RAMADHANI baharia wa CAPE TOWN, akapande nalo stejini wakati albam ya kwanza hata haijakamilika, RAMADHANI anatukusanya madogo wa kitaa tukamshangilie prof jizze, Blue sijui alikuwa wapi!

Nikiwa kidato cha 5, Fa alikuwa kidato cha 6 PCM. wakati Fa anaruka fence usiku kwenda makumbusho kupiga tizz na akina Juma Mchopanga, anakuja kutoka na INGEKUWA VP, Blue simjui!

Kwa umri wangu ukintajia Malegendary nitakuelewa ukitaja kizazi hiki! Lakini hawa watoto wa Mulugo wapo sahihi kumtaja Blue kama legendary wao!
Kwani unachobisha ni nini mkuu? ?kaongelewa Mr blue hapa mtoa maada hajasema kama blue ni bora kuliko hao uliowataja sasa nashangaa unabishana bishana
 
Ili umpate Blue, inabidi utaje malegendary 10, ukitaja wa5 Blue hatii sio pua tu, hata kamasi! Ona hawa hapa:
1. Joseph Mbilinyi
2. Fareed Kubanda.
3. Joseph Haule.
4. Juma Mchopanga.
5. Albert Mangair.
Kama hutaki sikulazimishi, kaa na ubishi wako!
kigezo gani kinatumika kumpa mtu cheo cha u-legendary?
 
Ahsante sana. Umenijuza tofauti yangu na mtoa mada.

Ngoja nikupe mfano. Wakati SUGU anahit, anakuja kutuimbia shule za Moro town back in mid 1990s pale Forest Hill, Kigurunyembe, Moro Sec, n.k Sijui Blue alikuwa wapi!

SUGU anapanda jukwaani, MANGO GARDEN, analipwa, mtoto wa kitaa AFANDE SELE, anapewa MIC na SUGU anaimba bure ili tu atoke!

AFANDE anaandika, anaimba anatuskilizisha ngoma huku tukimpamba, hatimaye SUGU anambeba ktk ngoma MIKONONI MWA POLISI, Afande anarudi Morogoro anasimulia mtaa mzima!

Nilikuwa DSM wakati Prof Jay anaazima koti la Jeshi la mchizi wake RAMADHANI baharia wa CAPE TOWN, akapande nalo stejini wakati albam ya kwanza hata haijakamilika, RAMADHANI anatukusanya madogo wa kitaa tukamshangilie prof jizze, Blue sijui alikuwa wapi!

Nikiwa kidato cha 5, Fa alikuwa kidato cha 6 PCM. wakati Fa anaruka fence usiku kwenda makumbusho kupiga tizz na akina Juma Mchopanga, anakuja kutoka na INGEKUWA VP, Blue simjui!

Kwa umri wangu ukintajia Malegendary nitakuelewa ukitaja kizazi hiki! Lakini hawa watoto wa Mulugo wapo sahihi kumtaja Blue kama legendary wao!
mkuu mbona kama ulikuwa unatafuta upenyo wa kuonesha umeanza kusikiliza mziki kitambo?
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] wabongo tuna shida sana
 
Dogo namkubali sana yupo vizuri naona kustiki katika imani yake na kuwa kifamilia zaidi vimemshape kimaadili na kulinda kitu kinacho mpa ugali wa kila siku ambacho ni mziki asimame vivyo hivyo.
 
Blue ni legend, I agree kwamba ni one of the best talents ambazo tumewahi kuwa nazo kwenye bongofleva, namuheshimu sana mtu aliye perfect kwenye both kuimba na kuchana. Na ni wachache sana wanaoweza kumaintain kufanya hivyo kwa zaidi ya miaka 10
Kama Chid Beenz angepunguza ujuaji na yeye angekuwa kwenye level hizi.

Kuanzia Mwaka 2006 Kwa upande wangu sijaona Rapper mpya mkali kuliko Chid Beenz
Ili umpate Blue, inabidi utaje malegendary 10, ukitaja wa5 Blue hatii sio pua tu, hata kamasi! Ona hawa hapa:
1. Joseph Mbilinyi
2. Fareed Kubanda.
3. Joseph Haule.
4. Juma Mchopanga.
5. Albert Mangair.
Kama hutaki sikulazimishi, kaa na ubishi wako!
Mkuu sikupingi ila kila mtu na mtazamo wake hasa zinapokuja list kama hizi.

Jamaa kwa upande kwenye list kama hiyo lazima blue angekuwepo...Na mimi kwa upande wangu lazima Joh Makini angekuwepo so we not the same Mkuu.
 
bashite alitaka kumuangusha lakini bado Ana shine
 
Nafikiri kinachosababisha Blue aonekane legendary ni kwa sababu alianza muziki akiwa kinda huku mashabiki wanaomshabikia wakiwa makinda pia.

Maana yangu ni kua Blue amekua umri sawa na mashabiki zake, yaani tangu anatoa blue blue mpaka leo ni mashabiki wake wale wa umri wake.

Nature kibla, Prof j, Mandojo Na Domokaya n.k walikua na mashabiki wengi sana lakini mashabiki hao umri ushawatupa mkono hawawezi tena kuingia jf na kukumbusha kua Lil Kim alipofanya Show Tz ilibidi amtaje Nature kila muda ili mashabiki wasiondoke.
Au Mandojo na Domokaya na Nature walivyoifanya single ya Niaje, wimbo ambao kila mstari uliishia na herufi 'i'

Hivyo hili kundi la Blue, litakwenda na maji kisha watakuja mashabiki wa Youg Killer ambao miaka 7 mbele na wenyewe wataandika kama kilichoandikwa hapa.
Mkuu kinachotokea ni kuwa huyo Young Killer ataweza kubaki pale halipo kwa miaka yote hiyo?!

Maana kuna wasanii kibao waliotoka pamoja na Blue wakati ule ila speed zao zimekata njiani.

Kama unakumbuka mtu kama Bab Lee,Ab skills,Hakeem 5,Joselin na hapa juzi kati Chid Beenz wote wamepotea ila Blue bado yupo.

Mimi nadhani haiusiani na shabiki peke yake na msanii Ana nafasi kubwa zaidi.
 
Castr Kumbukumbu zinanionyesha miaka ambayo wakina Mandojo walikuwa wakikimbiza ndio miaka ambayo Mr. Blue aliibuka, just imagine hao wakina Mandojo wamepotea lini? Tukubali tu dogo kaweza kamaintain kwa mda mrefu kitu kinachowashinda wengi, ishu sio umri.Na sio kweli kwamba watu tuliofatilia bongofleva tangu enzi za kina 2 Proud (Sugu) hatumo humu, tupo wengi, ukitaka kujua hilo fungua thread inayohusu wasanii wa zamani uone raia wanavyofunguka
 
Kumbukumbu zinanionyesha miaka ambayo wakina Mandojo walikuwa wakikimbiza ndio miaka ambayo Mr. Blue aliibuka, just imagine hao wakina Mandojo wamepotea lini? Tukubali tu dogo kaweza kamaintain kwa mda mrefu kitu kinachowashinda wengi, ishu sio umri.
Wengi tu walikuwepo wakina Bab Lee,Jebby,Joselin,Ab skills na hapo juzi kati wakina Chid Beenz ila wote wamepotea Heri Samir bado yupo kwenye chart.

kumkataa jamaa ni kujinyima raha tu Mkuu.
 
Busy kwenye game huyu jamaa safi sana kinachofanya azidi kuheshimika ni roho yake nzr, I mziki mzr bila kiki, kajiolea zake warda hatak scandal na ule ubishow wakijanja sio wakujiskiaa
 
Back
Top Bottom