Ahsante sana. Umenijuza tofauti yangu na mtoa mada.
Ngoja nikupe mfano. Wakati SUGU anahit, anakuja kutuimbia shule za Moro town back in mid 1990s pale Forest Hill, Kigurunyembe, Moro Sec, n.k Sijui Blue alikuwa wapi!
SUGU anapanda jukwaani, MANGO GARDEN, analipwa, mtoto wa kitaa AFANDE SELE, anapewa MIC na SUGU anaimba bure ili tu atoke!
AFANDE anaandika, anaimba anatuskilizisha ngoma huku tukimpamba, hatimaye SUGU anambeba ktk ngoma MIKONONI MWA POLISI, Afande anarudi Morogoro anasimulia mtaa mzima!
Nilikuwa DSM wakati Prof Jay anaazima koti la Jeshi la mchizi wake RAMADHANI baharia wa CAPE TOWN, akapande nalo stejini wakati albam ya kwanza hata haijakamilika, RAMADHANI anatukusanya madogo wa kitaa tukamshangilie prof jizze, Blue sijui alikuwa wapi!
Nikiwa kidato cha 5, Fa alikuwa kidato cha 6 PCM. wakati Fa anaruka fence usiku kwenda makumbusho kupiga tizz na akina Juma Mchopanga, anakuja kutoka na INGEKUWA VP, Blue simjui!
Kwa umri wangu ukintajia Malegendary nitakuelewa ukitaja kizazi hiki! Lakini hawa watoto wa Mulugo wapo sahihi kumtaja Blue kama legendary wao!