Mr Blue ndiye msanii mwenye uwezo mkubwa kwenye stage kuliko wasanii wote wa bongo fleva Tanzania?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam wana jamvi

Pamoja kuwa tumezawadiwa wasanii wengi sana wa muziki wa kizazi kipya nchini lakini ni wachache sana ambao kila mtu angependa kuwasikiliza au kuwasubiria watafanya nini wakiwa kwenye stage au wakiwa mbele ya mashabiki.....
Wasanii wetu wengi ni wajuvi wa kuimba kwenye radio tuu lakini wakiwa kwenye matamasha hutamani kuendelea kuwasikiliza kwani wengi wao pamoja na kuwa na nyimbo zinzo tamba lakini wakiwa kwenye stage wanakuwa wamepoa sana na huwaboa mashabiki sana tena sana na unaweza fikiri labda mashabiki hawamfahamu muhuisika....

Mr Blue ni mmoja ya wasanii ambao pengine wanaweza wasiwe wana sikika sana radioni au kutotoa nyimbo kila leo radioni lakini ukweli ni kwamba ana nguvu kubwa sana tena sana kuliko hata wasanii ambao kila leo husikika na nyimbo mpya radioni......

Nilipata wasaha kumshuhudia kwenye TV -E kwenye tamasha la komaa na mziki mnene yanayo andaliwa na E-fm kwakweli ni ukweli usiopingika kuwa Mr Blue ndiye msanii pekee wa bongo fleva anayeweza kupambana na wasanii wa singeli kwenye kuwapagawisha mashabiki kwenye matamasha......

Mr Blue ni msanii mwenye nguvu sana stageni kwakweli mwanzo nilikuwa nashangazwa na yeye kupewa show kila mara pamoja na kutokuwa na nyimbo mpya nyingi radioni au kutosikika sana radioni...... kwa jicho langu nimethibitisha ni msanii mkali sana stageni ukiwaacha wa singeli ambao kwakweli wanatoa upinzani mkubwa sana kwa wasanii wa bongo fleva.

Wasalaaam
 
Nifanye nini ili unielewe,
Nifanye nini ili niwe na wewe,
,
,
, eti mapozi na we, mapozi na we
,
,sijui nini na nini huko aiseee yule ndo alikuwa Mr.Blue lakini sio huyu wa sasa anayebebwa na muonekano na khariba yake.
 
Unamjua diamond platinumz wewe?ambaye Rita paulse akiwa kwenye BSS anamtumia Kama reference ya stage master artist kwa washiriki.
 
Unamjua diamond platinumz wewe?ambaye Rita paulse akiwa kwenye BSS anamtumia Kama reference ya stage master artist kwa washiriki.
Mada ni MR. BLUE soma vizuri Kichwa cha habari huyo mtafutie uzi wake.
Kwa Sasa hivi ambapo amejikita utimu kiba ndo anakuja kuisha kabisa na amevyonenepeana ana ata pumzi now days.
Pumzi kama anayo au hana hayo anayajua MKEWE,
Ila kwa kutawala stage jamaa hana mpinzani.

Kama unahisi kumkubali Kiba ndio atapotea pole yako inaonesha umechelewa kuja town.
 
upo sahihi mkuu,nimepata kuona kwenye tv na pia live show zake,jamaa hana mpinzani hata media zinajua na wasanii pia wanajua.kuna show moja nilikua na wasanii backstage,blue aliposhuka alishangiliwa vibaya mno na kina darasa nk baada ya kuua show kinoma.
 
maisha ni kupanda na kushuka
jana tulishuka cheki leo tunapanda
nimepata idea ya kusambaza kanda
nimepata show za kenya na uganda
burundi na rwanda
 

Juma nature ndio fundi mkuu kwenye stage.
 
Jamaa kinachofurahisha akipanda stejini ana energy sana na vibe ambayo inafanya hata asiyekubali muziki wake afurahie show na kile kibesi chake sijui alikitoaga wapi[emoji3]. Amekuwa mkombozi wa show za Clouds kama alivyokuwa Nature enzi zile
 
Umevuta bange mbichi? Siku nyingine bangi vutia mdomoni siyo kwenye matundu mengine.
 
Jamaa kinachofurahisha akipanda stejini ana energy sana na vibe ambayo inafanya hata asiyekubali muziki wake afurahie show na kile kibesi chake sijui alikitoaga wapi[emoji3]. Amekuwa mkombozi wa show za Clouds kama alivyokuwa Nature enzi zile
Ana pumzi sana....nilicheki clip moja akiwa kule tabora na EFM aisee jamaa ni hatari...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…