Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Mfanyabiashara, Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr. Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kufanya biashara ya haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za Umma zaidi ya Tsh. 17 bilioni.
Machibya ambaye ni mkazi wa Oysterbay amesomewa mashtaka yake leo 10/08/2020 na Wakili wa Serikali muandamizi mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Godfrey Isaya. Akisomewa mashitaka yake, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi na 60/2020, kati ya mashitaka hayo 7 yapo ya kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu, kupokea maingizo ya fedha za umma bila ya kuwa na leseni na kutakatisha fedha.
Mfahamu zaidi Mr. Kuku:
Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?
Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku