Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17



Mfanyabiashara, Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr. Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kufanya biashara ya haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za Umma zaidi ya Tsh. 17 bilioni.

Machibya ambaye ni mkazi wa Oysterbay amesomewa mashtaka yake leo 20/08/2020 na Wakili wa Serikali muandamizi mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Godfrey Isaya. Akisomewa mashitaka yake, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi na 60/2020, kati ya mashitaka hayo 7 yapo ya kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu, kupokea maingizo ya fedha za umma bila ya kuwa na leseni na kutakatisha fedha.

Mfahamu zaidi Mr. Kuku:
Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?
Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku

Hiyo tarehe vipi? leo 20/8/2020?...huwa hata sipotezi kuhusu huu upuuzi,ukipigwa kiivyo ni uzembe.
 
Hahaha watanzania wanapenda sana hizi, waweke pesa mahala wao wakalale wakingoja faida.

Hakuna mtu wa kukufanyia kazi ukiwa umelala nyumbani, ona sasa pesa inaenda kutaifishwa na serikali na hamtalipwa, labda mfungue kesi ya madai.
 
Kwa hali hii CCM itaendelea kuitawala hii Nchi kwa miaka mingi sana.

Ukiona Wananchi wanakimbilia kwenye njia za mkato ili kujipatia kipato/fedha za haraka/ utajiri, ujue kuna mahali Serikali imeshindwa kutimiza wajibu wake aidha kwa makusudi au hata kwa bahati mbaya.
 
Hahaha watanzania wanapenda sana hizi, waweke pesa mahala wao wakalale wakingoja faida.

Hakuna mtu wa kukufanyia kazi ukiwa umelala nyumbani, ona sasa pesa inaenda kutaifishwa na serikali na hamtalipwa, labda mfungue kesi ya madai.
Hivi zile za DECI zilisherudi?
 
Na duniani wajinga hawaishi.

Hata kama wasingepigwa na Mr. Kuku wangepigwa na mwingine.

Kuna watu hata uwa-alert vipi hawatakuelewa, wataendelea kupigwa tu.
HUWA NASEMAGA WAJINGA HAWAISHI LABDA BAHARI IKAUKE.....
Alafu waajiriwa wakaa ofisini ndy wamepigwa sana
Maana wanapenda urahisi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Hiyo inaitwa ponzi scheme, ukijipanga bizuri lazima uwashike watu sema mwisho lazima ilipuke halafu, unakuta yeye hapo alipo hata b1 moja kwenye account hana.
Yap ndo inavyotakiwa kwa maana lazima uwe na plan b ili likibuma uwe na upenyo mwingine sio unakuwa mjanja mjanja then mzigo wote upo kwenye akaunt utakuwa fala sana
 
Back
Top Bottom