Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Mrangi kuna watu wanasema jamaa angesepa mapema... kwa uzoefu wako na kwa ukubwa wa hii figure 17b unadhani serikali ya wanyonge isingemfuata hukohuko alikokimbilia?
Kuna nchi za kwenda babu huyo pusi mkuu hakupati na majibwa yake. Ontario mpaka leo anadunda. Inahitajika international standard criminal mind.
 
Bado wale wa QNET. Afu waalimu wa serikali ni wengi sana huko qnet na AIM GLOBAL....
WAZEE wa GUDIMONINGI
 
Sasa kama upatu ni sio haramu kwanini hii taarifa inakuza msamiati huu "Akiwa anaendesha upatu" mpaka mentally ukimuuliza mtu upatu ni nini atasema utapeli, kwaninj wasiseme "akiwa anaendesha Biashara bila leseni.

Kuna vitu vinakera.
Angeendesha upatu kwa leseni isingeitwa upatu wangeita hisa(shares) ila amefanya bila leseni basi ni UPATU yaani ni kama tofauti ya CHALESI na CHAZI au Maiko na MISHELI.
 
Kuna bush lawyer wanajipa moyo eti kesi nyepesi atatoka 😆😆😆
Kesi nzito sana ya uhujumu uchumi hiyo ndugu zake na wapanda mbegu wajiandae kisaikolojia tu wakifanya haraka miaka mitatu ndio inaweza kutoka hukumu.
 
Kuna nchi za kwenda babu huyo pusi mkuu hakupati na majibwa yake. Ontario mpaka leo anadunda. Inahitajika international standard criminal mind.
Hahahahahaha pusi mkuu.!!!! Kuna mdau kataja Namibia ila naona kama Afrika ni kama sio salama.
 
"Ukiitwa kwenye fursa ujue wewe ndo fursa yenyewe" katika sauti ya Joti aliyekuwa mshehereshaji wa tangazo
Kabisa mkuu nature ya binaadamu tumeumbwa na umimi kama sehemu kuna ulaji utataka kula peke yako ila ukishirikishwa na kuambiwa deal za kupata pesa kirahisi rahisi basi jua unaingizwa 18 aka unaelekezwa kibla uchinjwe.
 
Wawekezaji ( investors) wakimsubiri Mr Kukus wavunje kibubu[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji39][emoji111]
1596399117928.jpeg
 
Sasa kama upatu ni sio haramu kwanini hii taarifa inakuza msamiati huu "Akiwa anaendesha upatu" mpaka mentally ukimuuliza mtu upatu ni nini atasema utapeli, kwaninj wasiseme "akiwa anaendesha Biashara bila leseni.

Kuna vitu vinakera.
Upatu (Pyramid scheme) ni haramu. Actually ni kosa la jinai.
 



Mfanyabiashara, Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr. Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kufanya biashara ya haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za Umma zaidi ya Tsh. 17 bilioni.

Machibya ambaye ni mkazi wa Oysterbay amesomewa mashtaka yake leo 10/08/2020 na Wakili wa Serikali muandamizi mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Godfrey Isaya. Akisomewa mashitaka yake, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi na 60/2020, kati ya mashitaka hayo 7 yapo ya kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu, kupokea maingizo ya fedha za umma bila ya kuwa na leseni na kutakatisha fedha.

Mfahamu zaidi Mr. Kuku:
Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?
Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku
Hii 60/2020 ina maana gani?
 
Hiyo 60/2020 maana yake ni case namba 60 ya mwaka 2020. Kwa kifupi ni kuwa tangu mwaka huu uanze,mahakama hiyo imekwisha sajili kesi 60 za uhujumu uchumi.
Ahsante kwa ufafanuzi.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yani watu wamepigwaa parefu mamaee...! Sema jamaa akitafuta wakili imara anaweza chomoa hii kesi alafu akasepa na Mpungaa..
thubutu [emoji3]
 
Hahahahahaha pusi mkuu.!!!! Kuna mdau kataja Namibia ila naona kama Afrika ni kama sio salama.
Huyo anayeitaja Namibia kama ni mhalifu bado amateur. Namibia si salama kabisa. Hizi nchi za SADC sio. Kuna nchi bara Asia huko na visiwa. Hawakupati milele. Na unakwenda kabisa kufanya na plastic surgery ya sura. Kuna nchi hazina mafungamano na Tanzania na hakuna masuala ya interpol.
 
Back
Top Bottom