Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Huyu jamaa si aliwapa akina joti tenda yakutangaza biashara yake itakua kavuna pesa nyingi sana
Kabisa mkuu..Joti anatangaza kazi za makampuni makubwaa tu sasa ukiona anatangaza kazi ya Mtu binafsi jua mpunga wa maana umetokaa..
 
Huyo anayeitaja Namibia kama ni mhalifu bado amateur. Namibia si salama kabisa. Hizi nchi za SADC sio. Kuna nchi bara Asia huko na visiwa. Hawakupati milele. Na unakwenda kabisa kufanya na plastic surgery ya sura. Kuna nchi hazina mafungamano na Tanzania na hakuna masuala ya interpol.
Pesa nyingi bila uhuru bora kuwa masikini, Financial freedom ndio lengo la kuwa na pesa nyingi nijichimbie nibadili sula yaani waliokuwa wananishuudia kwenye msoto siku nikioita na Roll Royce mtaani hawanijui shits.
 
Mtu Binafi ??

Kwani sio kampuni ile.
Kampuni ya Mr.Kuku mbona pale kakamatwa mtu mmoja[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yeye ndo mmiliki wa hiyo unayoiiya kampuni wengine vibara tu so Mr Kuku kampuni yake kuwa na uwezo wa kumlipa Joti sio kitoto
 
Kampuni ya Mr.Kuku mbona pale kakamatwa mtu mmoja[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mkuu kakamatwa au anashitakiwa ??

Ok mbona tuna muonaga Max pekeeyake mahakamani.
 
Pesa nyingi bila uhuru bora kuwa masikini, Financial freedom ndio lengo la kuwa na pesa nyingi nijichimbie nibadili sula yaani waliokuwa wananishuudia kwenye msoto siku nikioita na Roll Royce mtaani hawanijui shits.
Nyinyi ndiyo akina Kasusura au wale wa kampuni ya ulinzi walioenda kukaa Mbagala ili wawatambie wananzengo.
 
Mambo mengine jamani, unaanzaje kufanya biashara bila kufahamu sheria ya nchi juu ya biashara husika inasemaje!

Halafu hawa celebrity entrepreneur hawa, binafsi siamini mtu kufanya biashara na kujinadi huku na kule, lazima kuna ka kitu ana kaanda.

Hawa vijana wana akili sana, hawajachagua kuzitumia vizuri na kwa usalama wao.
 
Haya makampun ya kitapeli yamejaa,kuna moja inaitawa VKP INVESTMEST wauza viwanja kwa mkopo,watu tuliwaamini sababu ni registerd tumemaliza mikopo hakuna cha viwanja,mashamba wala kurudishiwa hela mwaka wa tatu kesi ipo mahakamani zaidi ya bilioni moja watz tumepigwa watu zaidi ya 300.Mmiliki wa kampuni hana pesa wala kiwanja cha kumpa mtu.
Mmiliki anaitwa Yona? Mafaili yake nimeshayaona.
 
Huyu mtu anawekeza, haibi cha mtu. Ukifika shambani kwake unaona kabisa mabanda na kuku zaidi ya laki mbili. Ana masoko ya uhakika, anakusudia kujenga kiwanda cha kusindika nyama, kiwanda cha kutengeneza vyakula vya mifugo, zote hizo ni ajira kwa watanzania.

Pesa yote haiendi nje inabaki humuhumu. Sasa nyie mnaosema ni tapel, mmeifanyia nini nchi hii? Wazo gani la kuinua jamii mmeanzisha na likakubaliwa? Kumlinga mr Kuku na Ontario siyo sawa. Hata Ontario, unapoteza pesa kwa kukiuka misingi na tamaa

Hivi ni kwanini mnakuwa wazito kuwatumia graduates wa sheria waliojazana mitaani ili wawasaidie kutafsiri sheria za biashara za nchi hii?

Ulishawahi kutafuta wawekezaji wa nje ya nchi hasa za magharibi? Kitu cha kwanza atakuuliza ni kuhusu sheria na sera za nchi yako juu ya uwekezaji mnaotaka kuufanya. Siamini bado kuwa hujaelewa ni kwani Mr.Kuku ana kesi ya kujibu.
 
Duuh msala sanaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Hii Bongo leo hii ukitoa hata Mil 100 na huna vithibitisho vya biashara inayoendana na pesa hizo msalaaa.

Wala si bongo tu, sehemu zote kuna sheria ya pesa, ndio maana kuna backup ya black market huko unaweza kuzungusha fedha utakavyo, ukitaka mambo legal lazima uweze kujustify mambo kadha wa kadha. Kuzunguka zunguka na mahela ambayo huwezi kuyatolea ufafanuzi ni kutokuwa smart enough.
 
daa atakuja mwingine na Mr Mbuzi ataendelea kuwapiga tena mang'ombe hayaishi mjini kila siku yanazaliwa upya na hasa yale mavivu ya kufanya kazi...
 



Mfanyabiashara, Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr. Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kufanya biashara ya haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za Umma zaidi ya Tsh. 17 bilioni.

Machibya ambaye ni mkazi wa Oysterbay amesomewa mashtaka yake leo 10/08/2020 na Wakili wa Serikali muandamizi mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Godfrey Isaya. Akisomewa mashitaka yake, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi na 60/2020, kati ya mashitaka hayo 7 yapo ya kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu, kupokea maingizo ya fedha za umma bila ya kuwa na leseni na kutakatisha fedha.

Mfahamu zaidi Mr. Kuku:
Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?
Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku


Me naona cha muhim ni watanzania kuwa na subira kuliko kuanza kutoa shutuma za utapeli juu ya Mr kuku, maana katika mashtaka aliosomewa hakuna shitaka la kushindwa kulipa wawekezaji wake, na pia kama biashara watamfungia basi inabid waifungue account ya crdb ili iweze kurejesha pesa za wawekezaji maana zile pesa za umma
 
Back
Top Bottom