sasa si kanisani wanaendaga asubuhi, usiku anakuwa hapao masai, na mimi nilimuona last week hapo Masai. Mbona wa kuokoka kihivyo wapo wengi tu, huwa ninakutana maskani moja na dokta remmy ongala, napiga zake urabu na bangi kisha anafanya na yale mamabo yetu kisha asubuhi anaenda kanisani kuchapa misa.
Mbona nimesoma jana tu kwenye magazeti kuwa ameanzisha bendi kama jibu kwa watu wanasambaza taarifa kuwa amefulia!!!!????
Aliyekua muimbaji wa Dansi nchini Lucas Mkenda au Mr. NICE kama anavyojulikana na wengi amempa Yesu maisha yake tangu mwezi wa nane mwaka huu. Anahudhuria ibada, maombezi na tayari amebatizwa. Chanzo cha habari kinasema anaabudu Kawe kwa GeoDavie jijini Dar-es-salaam, tayari ana nyimbo nne za kusifu na kumuabudu Mungu. Amekua akitoa ushuhuda wake kwamba Mungu amemponya na kuyaokoa maisha yake.
Source:http://strictlygospel.wordpress.com/2009/10/12/mr-nice-ameokoka/
samahani nje ya mada kidogo!burn vipi tunaweza kuwasiliana?mimi ni msela tu wala usijali.ai mini mimi si yudabliyutiii.unaweza ni pm namba zako?mimi huwa najivuta pale mara moja moja
MN,
Habari uliyoinukuu hapa kuwa jamaa ana bendi imeandikwa na gazeti la Nipashe la tarehe 24/10/2009 na ninayo nakala yake. Jamaa kaanzisha bendi na yuko mbioni kutoa albamu mbili mpya akiwa na bendi yake hii. Sasa hizi habari za kwamba kaokoka tangu mwezi wa nane zinashangaza kidogo!
Ufafanuzi tafadhali!
KILA JUMANNE:huwa anatumbuiza MASAI CLUB pale karibu na mango-garden.halafu jamaa anaongoza kwa kuomba bia mazee!yani akishaingia tu inabidi wadau tujifiche,maanake ni kama luba.
kwa mfanu jumanne iliyopita alikunywa sana konyagi.............
anaebisha tukutane nae kesho club masai
Mimi naomba kuuliza swali...Kila siku nasoma post za watu humu ndani kuna hili neno "FULIA"...Linatumika sana lakini hata sijui maana yake ni nini?...kama kwenye hii topic limetumika 10 Times....na kila nikijaribu kusoma sentensi nashindwa kuelelewa maana ya Fulia naomba msaada please anayejua maana yake.....
Neno "Fulia" lina maana kuwa umeloweka nguo kwenye maji (suruali, shati e.t.c) na kuanza kufua (weka sabuni na pikicha), na ghafla unagundua kuwa katika ile nguo (baada ya kusuuza na kuanika) kulikuwa na kitu chako cha maana (pesa, saa, e.t.c) na tayari kimelowana na kuaharibika.
Kwa sentensi unaweza sema "Nimefulia hela yangu kwenye shati". . .
Lakini sasa katika harakati ya kutafuta uwezo wa kwenda "******" waigizaji wa vicheckesho wa television wametumia neno "fulia" wakimaanisha "kuishiwa pesa" kwa mtu ambaye hapo awali alikuwa nazo.
Thank you Baba_Enock.....so kufulia ni kuishiwa i will keep that in mind.....
Mkuu, nini Mr.Nice...wanafanya kufuru kina J-zee,P.Diddy na wenzao...kuna kundi la akina dada linaitwa Pussy cate dolls, hawa uchawi wao hauna kificho hata kidogo, wapo Black eyed pies,wanatisha hata sura zao...mkienda katika kumbi za starehe..muwe waangalifu kuna mambo ya ajabu ajabu...yanakirihisha hata kuyasema hapa utatishika tu...kuna bendi Tz inatumia mtindo wa 'sayansi' ya kinu na mchi...hawa wana mizimu yao Ifakara huko...hata aondoke nani hawashuki.ina maana MR nice mziki wake ulikuwa unaenda na ushirikina
looh maybe ndo maana kaamua kurudi kundini
Mkuu, nini Mr.Nice...wanafanya kufuru kina J-zee,P.Diddy na wenzao...kuna kundi la akina dada linaitwa Pussy cate dolls, hawa uchawi wao hauna kificho hata kidogo, wapo Black eyed pies,wanatisha hata sura zao...mkienda katika kumbi za starehe..muwe waangalifu kuna mambo ya ajabu ajabu...yanakirihisha hata kuyasema hapa utatishika tu...kuna bendi Tz inatumia mtindo wa 'sayansi' ya kinu na mchi...hawa wana mizimu yao Ifakara huko...hata aondoke nani hawashuki.
Pesa iko kanisani kwa waimbaji! Waimbaji mnaokazania kuimba kwenye maholi ya muziki hamjui wapi iko sukari.Aliyekua muimbaji wa Dansi nchini Lucas Mkenda au Mr. NICE kama anavyojulikana na wengi amempa Yesu maisha yake tangu mwezi wa nane mwaka huu. Anahudhuria ibada, maombezi na tayari amebatizwa. Chanzo cha habari kinasema anaabudu Kawe kwa GeoDavie jijini Dar-es-salaam, tayari ana nyimbo nne za kusifu na kumuabudu Mungu. Amekua akitoa ushuhuda wake kwamba Mungu amemponya na kuyaokoa maisha yake.
Source:http://strictlygospel.wordpress.com/2009/10/12/mr-nice-ameokoka/
This is good marketing strategy for Mr. Nice, kaona kurudi juu tena haitawezekana,njia pekee iliyobaki ni kupitia "gospel", ila sijuwi kama ile miiko ya kiganga ndo imekwisha na jamaa yupo "free" sasa au vp, maana sifikirii kama gospel inaendana na uchawi.
Duh mzee umewaza mbaaalli. lakini inaweza tokea bwana mana shetani ana njia nyingi.Natamani awe ameokoka kweli-kweli lakin wasiwasi wangu anaweza kuwashambulia kondoo wa Bwana kwa staili ya ajabu mmh1
Hayakuhusu baba, wewe nenda vacation yako makka. Usipookoka huko basi jua utakanyagwa kanyagwa kama unyasi wakurudishe hoi. Usimchezee Yesu. Fanya utani na Mwamedi tu.Muongo mkubwa huyu BAZAZI baada ya kujiona KAFULIA ndio ameamua kuokoka.